Ni watu gani wanaotakiwa kwenda kwa Makonda kulalamika kutelekezwa?

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
11,143
18,774
Ningependa kuelimishwa. Hivi hasa ni watu gani wanatakiwa kwenda kwa Makonda kulalamika kutelekezwa;
  1. Wanawake wenye watoto wadogo chini ya miaka 18 wanaohitaji msaada toka kwa wanaume waliowatelekeza kulea watoto waliozaa nao
  2. Wanawake waliokuwa wameolewa na mwanaume fulani na kisha kufukuzwa/kutalikiwa na kutelekezwa bila aina yoyote ya matunzo wala msaada
  3. Wanawake waliozaa mtoto na mwanaume fulani na kisha kuolewa na mwanaume mwingine lakini yule mwanaume waliezaa nae hatoi matunzo kwa mtoto ambae kwa sasa bado ni mdogo na anaishi na wazazi wa mwanamke
  4. Wanawake waliozaa na wanaume na kubaki na watoto kwa kuwa wanaume waliozaa nao wako hoi kiuchumi
  5. Wanaume walioachwa/waliotalikiwa na wake zao ambao kwa sasa ni matajiri au wenye uwezo sana kuliko mwanaume waliemwacha
  6. Watoto chini ya miaka 18 ambao mama zao wamewaambia baba zao waliwatelekeza baada ya mama zao kupata mimba lakini mama zao hawako tayari kwenda kwa Makonda
  7. Wanaume/wanawake waliotelekezwa na baba/mama zao huko nyuma lakin sasa ni watu wazima zaidi ya miaka 18 na wanapaswa kujitegemea na huenda hata wameolewa/kuoa na kuzaa
  8. Wote hapo juu
 
Back
Top Bottom