Ni Watanzania wangapi wanamudu kusafiri na ndege kwa pesa kutoka mifukoni mwao?

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Nov 28, 2013
10,129
35,146
Tumekuwa tukisikia wanasiasa fulani wakijisifu kuleta maendeleo kwa kununua ndege na wengine wakikosoa vikali uamuzi huo.

Ukweli unaokubalika kwa makundi yote mawili kuhusu usafiri wa ndege ni kuwa; usafiri wa ndege ni jambo la gharama kubwa na huenda ni mahususi kwa baadhi ya watu tu.

Nimekaa na kujiuliza haya maswali

1. Usafiri wa ndege hapa Tanzania umelenga kundi gani haswaa la kijamii?

2. Ni Watanzania wangapi wanaweza kumudu kulipia gharama za kusafiri kwa ndege kwa pesa zao kutoka mifukoni mwao?
 
Sisi Watanzania tunapanda ndege, Rais Magufuli ameshusha sana bei ndege zake
 
Watumiaji wa ndege Tz ni chini ya 1% ya Watanzania.
Huo mtaji midege ungewekezwa katika kilimo leo hii JPM ile agenda ya viwanda 2015 ingekuwa katika pick na std gauge ingesubiriwa kwa hamu na Watanzania kuokoa jam tatizo usafiri bidhaa kilimo toka viwandani na mashambani.
..."mimi sipangiwi..... nipeni wabunge na madiwani ccm nina uwezo kuwadhibiti.."
 
Nilianza kupanda ndege baada ya FastJet kuleta neema, nalaani kwa nguvu zote serikali kwa figisu walizolitendea shirika lile.

Na kwa hasira zote, tuungane kumtia adabu huyu uchwara hapo tarehe 28.
 
Tumekuwa tukisikia wanasiasa fulani wakijisifu kuleta maendeleo kwa kununua ndege na wengine wakikosoa vikali uamuzi huo.

Ukweli unaokubalika kwa makundi yote mawili kuhusu usafiri wa ndege ni kuwa; usafiri wa ndege ni jambo la gharama kubwa na huenda ni mahususi kwa baadhi ya watu tu.

Nimekaa na kujiuliza haya maswali
UKISIKIA UBWEGE NDO HUU, sio lazima kila mtanzania apande ndege wanaoweza watapanda, kama wewe huwezi basi viongozi wako wa chadema na act wanapnda na ushahidi upo.
 
Tumekuwa tukisikia wanasiasa fulani wakijisifu kuleta maendeleo kwa kununua ndege na wengine wakikosoa vikali uamuzi huo.

Ukweli unaokubalika kwa makundi yote mawili kuhusu usafiri wa ndege ni kuwa; usafiri wa ndege ni jambo la gharama kubwa na huenda ni mahususi kwa baadhi ya watu tu.

Nimekaa na kujiuliza haya maswali

1. Usafiri wa ndege hapa Tanzania umelenga kundi gani haswaa la kijamii?

2. Ni Watanzania wangapi wanaweza kumudu kulipia gharama za kusafiri kwa ndege kwa pesa zao kutoka mifukoni mwao?
Hujui kuwa kuna vitu mtu unafanya kama kitegauchumi? Hii ni pamoja na ndege
 
Watumiaji wa ndege Tz ni chini ya 1% ya Watanzania.
Huo mtaji midege ungewekezwa katika kilimo leo hii JPM ile agenda ya viwanda 2015 ingekuwa katika pick na std gauge ingesubiriwa kwa hamu na Watanzania kuokoa jam tatizo usafiri bidhaa kilimo toka viwandani na mashambani.
..."mimi sipangiwi..... nipeni wabunge na madiwani ccm nina uwezo kuwadhibiti.."
Ndege zinajaa kila siku, watanzania wengi wa vipato tofauti tofauti tunapanda. Umebaki wewe tu kamanda.
 
Back
Top Bottom