Ni wapi wanakopokea rushwa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni wapi wanakopokea rushwa?

Discussion in 'Jamii Intelligence' started by Wamnetu, May 21, 2012.

 1. W

  Wamnetu Member

  #1
  May 21, 2012
  Joined: Apr 29, 2012
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimebahatika kuingia katika ofisi mbalimbali za serikali na hata baadhi ya mahakama zetu jijini Dar es salaam na nilishangaa kuona matangazo mbalimbali katika kuta za ndani za baadhi ya ofisi hizo yakisema kwa maandishi makubwa "HATUPOKEI RUSHWA".

  Jambo la kushangaza ni kuwa hata wakuu wa ofisi hizo wameafiki kuwepo kwa matangazo hayo. Jambo lingine la kushangaza ni kuwa baadhi ya ofisi hizo ndizo zimekuwa zinalalamikiwa sana na wananchi kuhusu ulaji/upokeaji rushwa.

  Swali langu ni kuwa je kuna yeyote anayefahamu ofisi ambayo inatangaza kuwa wanapokea rushwa? Ningependa kuitembelea kama ipo!
   
 2. m

  mabhuimerafulu Member

  #2
  Jun 7, 2012
  Joined: May 29, 2012
  Messages: 89
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Ndiyo naifahamu. Inaitwa Tanzania
   
 3. Viol

  Viol JF-Expert Member

  #3
  Jun 7, 2012
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 18,982
  Likes Received: 1,088
  Trophy Points: 280
  mkuu we unadhani rushwa inatolewa vipi,bandiko ukutani ni kuzugia tu,but unapoanza kuongea nao kama una tatizo utajua tu wanavyoomba rushwa
   
 4. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #4
  Jun 7, 2012
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  waulize waendesha mashtaka na makarani wa mahakama watakueleza ziliko ofisi za kupokelea rushwa.
   
 5. kadoda11

  kadoda11 JF-Expert Member

  #5
  Jun 7, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 16,337
  Likes Received: 8,453
  Trophy Points: 280
  jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani
   
 6. Capt Tamar

  Capt Tamar JF-Expert Member

  #6
  Jun 7, 2012
  Joined: Dec 15, 2011
  Messages: 6,663
  Likes Received: 3,317
  Trophy Points: 280
  Pale kwenye hicho kibandiko ndipo unapotakiwa kusalimisha rushwa yako,baada ya kumalizana na wakuu walio ndani,ama unaandika namba ya simu unaichomeka pale,maisha yanaendelea, we ofisini kwenu hakuna sanduku la maoni?mimi nilitakiwa kuchomeka rushwa ya 250,000/= kwenye sanduku hilo,ikiwa ndani ya bahasha,nikajua kumbe sanduku hili lina umuhimu mkubwa kiasi hiki,hii ndio Bongo.
   
 7. L

  Losemo Senior Member

  #7
  Jun 8, 2012
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 183
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  It is the other way round. Kule wanakoandika hatupokei ina maana wanapokea zaidi. Pale pasipoandikwa wanapokea kdg kutokana na umuhimu wa huduma yao. TAKUKURU yenyewe iko kama daktari anayemtibu mgonjwa wa kansa na kumshauri aache sigara wakati yeye ana sigara mdomoni. RUSHWA NI UGONJWA WA HATARI MUNGU APISHE MBALI
   
 8. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #8
  Jun 8, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Tanzania kama hatujaweka sheria ya kuwatandika watu risasi hadharani kwa kutoa au kupokea rushwa basi haitaisha.

  Wapokea na watoa rushwa wa kwanza ni watunga sheria, nao ni wabunge wa bunge la JMT. Kwanini hawatungi sheria kali za kupambana na rushwa?
   
 9. M

  Malila JF-Expert Member

  #9
  Jun 8, 2012
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  tayari wamekula rushwa ili wasitunge sheria hiyo, ushahidi ni huu, siku walipoiita rushwa kwa jina la takrima.
   
 10. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #10
  Jun 8, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Hapana, takrima ilishawekwa kwenye kundi la rushwa.

  Sheria zipo lakini adhabu ni ndogo sana. Zirudishwe zikafanyiwe marekebisho adhabu ya rushwa hata kama umeomba soda tu, iwe ni kifo.
   
 11. mangosutu

  mangosutu JF-Expert Member

  #11
  Jun 26, 2012
  Joined: Jun 24, 2012
  Messages: 567
  Likes Received: 657
  Trophy Points: 180
  tz n zaidi ya uijuavyo
   
 12. LexAid

  LexAid JF-Expert Member

  #12
  Jul 13, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 1,950
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Hayo ni matangazo ya kuvutia biashara...Kha! mbona kichwa kigumu wewe? Huelewi?
   
 13. U

  Ubungo JF-Expert Member

  #13
  Jul 14, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 1,239
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Najua polisi wameacha kupokea rushwa. Kama kuna wengine mnijuze.
   
Loading...