Kwanza kabla ya yote, Uchawi sio tamaduni wala jadi ya muafrika, bali ni tabia ya washenzi, walafi, wenye roho mbaya, wabinafsi na washenzi ambao hawapendi maendeleo ya wenzao, na hii tabia(uchawi) si kwa waafrika tu bali ktk jamii zote dunian ipo.
Ungesema unataka kuunganisha na imani ya jadi na sio uchawi, kuna tofauti kati ya jadi na uchawi, jadi haihusiani na uchawi+ushirikina, uchawi unahusu kuharibu tu, jadi haihusu kuharibu.
Mlidanganywa na wazungu+dini kuwa jadi+mila za muafrika ni uchawi, wakat si kweli, bali jadi iko kinyume na tabia zote zinazokwenda kinyume na asili ya mtu.
Mchawi hajawai takiwa ktk mila+tamaduni za kiafrika ndiomaana wachawi tangu karne na karne walikuwa wakiwindwa kwa kuuwawa ama kutengwa na hizo hizo jamii za waafrika walioishi ktk mila+tamaduni+jadi.
Mjue kutofautisha mila za muafrika na huo ushirikina, we sema unataka kuwa mshirikina na hakunaga mshirikina au mchawi mzuri wote wabaya, utadangannywa unapojiunga lkn ukishaingia uko ndio hivyo tena.
Pili, uchawi hautafutwi adharani hivi, humu sidhan kama utapata ukitakacho, nenda vijijin huko ulizia wazee huko utapata connection, achana na hawa wachawi wa mjini ambao hata Panyaroad wanawasumbua, nenda vijijin huko nafaka zinaanikwa njian hakuna mdudu, mtu wala kiumbe wakubeba mali ya mtu[emoji16].