Mbase1970
JF-Expert Member
- Jun 11, 2015
- 6,054
- 4,601
Nimeanza kumfuatilia Maalim Seif na siasa zake zaidi bada ya kuwa kizuizini na kuachiliwa huru. Japo sizijuizaidi sababu zilipelekea Maalim kizuizini lakini kwa muono wangu Maalim Seif anatakiwa kupongezwa kwa mambo mengi aliyolifanyia Taifa hili la Tanzania pamoja na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar tangu alipokuwa Waziri Kiongozi na kama katibu mkuu wa CUF.
Maalim Seif kakumbana na dhoruba nyingi tangu akiwa mwanachama wa CCM hata pale alipovuliwa uanachama wa CCM na kujiunga na Upinzani. Kuna habari pia kuwa ameshadhurumiwa kura kuwa Rais wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar mara nne na hii ya mwaka huu ni ya tano. Kama kuna ukweli ama hakuna mimi si mtu wa kuhakiki hizo taarifa lakini kuna usemi usemao lisemwalo lipo kwa mantiki hii naweza kukubaliana na hoja hizo za kudhulumiwa.
Lengo langu la kuandika hii mada siyo kumdharau Maalim Seif la hasha, ila ni kumshauri tu kama kweli ana nia na maisha ya wananchi wa Zanzibar na ili kuuhakikishia ulimwengu na sisi tunaompenda na kumfuatilia miaka mingi kuwa hana uroho wa madaraka kama hao wanaomfanya asiweze kuwa rais basi angejitahidi kukaa pembeni na kuwa mshauri na kututafutia kijana muafaka kushika mikoba. Nchi za wenzetu zilizoendelea ukishindwa uchaguzi hata kama umeibiwa kura awamu inayofuata unakaa pembeni kupisha wenzako, lakini hapa kwetu hilo haliwezekani.
Unamkumbuka Al Gore? Mwaka 2000 aliibiwa kura na George Bush lakini mwaka 2004 hakuweka hata jina lake maana alijua kuwa kuna wengine wenye uwezo kama yeye ama hata kumzidi yeye. Unakumbuka mwaka 2008 John Kerry hakuthubutu hata kuweka jina lake maana aliona bahati haikuwa yake mwaka 2004 na akawachia kina Obama, Unamkumbuka John Mcain 2012 yeye pia hakuthubutu kuweka jina lake pia. Siasa zetu hapa africa tunaendelea kuwalalamikia kina Mugabe ati wanang'ang'ania kukaa madarakani lakini tunasahau pia hata kukaa sana madarakani kama mwenyekiti ama katibu mkuu bila kujali kuweka sura na akili mpya katika safu za uongozi hakutofautiani na kina Mugabe.
Miaka zaidi ya 20 imepita tangu Maalim na mwenziwe Lipumba wawe viongozi hatujaona mabadiliko yoyote ya uongozi, Mwalimu Nyerere alisema hata kama unapendwa saana ni bora ukaondoka wakati bado unapendwa kuliko kulazimishwa kuondoka (yeye aliita kung'tuka). Na mimi nasema ni bora kumtayarisha kijana kwa muda huu wa miaka mitano ili ikifika 2020 awe ameshakubalika inabidi pia kuwa naye bega kwa bega katika kumnadi Nchi nzima siyo zanzibar peke yake mpaka bara. Kwa kufanya hivyo Maalim utakuwa umeacha Legacy kubwa sana na utakumbukwa vizuri zaidi maana sasa utakumbukwa kama Kiongozi uliyeshindwa urais kwa vipindi vitano mfululizo kwa maadui zako na kiongozi uliyedhulumiwa urais kwa vipindi vitano mfululizo kwa wafuasi wako.
Wakati umefika wa kutowaona watu wachache tu ndiyo wenye uwezo wa kutuongoza, na pia kuiga mazuri kutoka kwa wenzetu waliobobea katika democracy kwani kuiga jambo nzuri siyo aibu. ED Milband aliposhindwa tu uchaguzi wa mwaka jana kule UK wiki hiyo hiyo alijiuzuru kama kiongozi wa Labour Party maana alijua chama chake kilishindwa uchaguzi mkuu sababu yeye kama kiongozi alishindwa kazi hivyo ilikua wakati muafaka wa kuwapisha wenzake.
Haya ni maoni yangu sina ubaya na Maalim Seif na ninamuheshim saana Maalim, Ninakumbuka miaka ya mwanzo wakati vyama vingi vinaanzishwa sisi wengine tulikua mstari wa mbele na ndiyo tulikua kwanza tumemaliza shule ama vyuo, wakati huo migomo mingi vyuo vikuu na tulikuwa na viongozi wazuri kama rais wa serikali ya wanafunzi wa pale Mlimani Mheshimiwa James Mbatia(MB) na mangi mwenziwe wa pale Muhimbili jina nimelisahau. Nilihudhulia mkutano pale Diamond Jubelee wakati kina mapalala, Chief Fundikira, Mabere Marando, Masumbuko Lamwai na wengine wengi walipoanzisha NCCR. Moja ya agenda muhimu ilikua kuhusu Maalim Seif na kumwombea ili achiwe huru kuungana nasi katika kuijenga Tanzania mpya ya demokrasia ya vyama vingi kabla ya viongozi wetu kutusaliti na kunza kumeguka badala ya kuomba Katiba mpya kama ilivyokusudiwa ktk mikutano yetu na wengie kutaka kuikimbilia IKulu na kuigeuza NCCR kuwa NCCR Mageuzi chama cha siasa badala ya Movement ya kudai katiba mpya. Na hii ilitufanya baadhi yetu kujiweka pembeni maana tulijua movement yetu iliingiliwa na mamluki wa CCM na tulijua kuwa kuingia Ikulu ingekuwa ndoto ya mchana. Hivyo Maalim Seif kwangu mimi unabaki ni Role Model wangu.
Hivyo basi ni vizuri tuwe na hulka ya kuachiana na kuacha uzandiki na majungu kwa vijana wapya ambao hawana damu ya UCCM kama ilivyo kwenu ninyi kina Maalim Seif jiepusheni na mamluki wa CCM ama sivyo upinzani utazidi kuwa kivuli cha CCM wengi mtanibeza na kuniita Lumumba maana siku hizi ukiusema upinzani japo kwa mazuri unaambulia matusi.
Asanteni kama mmesoma hoja yangu ipo wazi kwa majadiliano.