Hayati Maalim Seif alikataa kujiunga na CHADEMA na Kuamua kwenda ACT wazalendo kutokana na ubaguzi na chuki waliyonayo kwa Wazanzibari

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
16,066
10,570
Ndugu zangu Watanzania,

Hakuna mtanzania mwenye akili Timamu ambaye huwa anapenda ubaguzi au kubaguliwa au kumuunga mkono mtu anayeona amejaa mawazo ya kibaguzi na chuki katika kifua chake.kwa sababu anajuwa kuwa ipo siku na yeye atabaguliwa na kunyanyaswa tu. Wengi wa Wafuatiliaji wa masuala ya kisiasa na siasa walijuwa na kufikiri ya kuwa iwapo hayati Maalim Seif ataondoka chama cha wananchi CUF basi atajiunga CHADEMA.

na kweli wakati huo wa mgogoro wa Maalim Seif kama katibu mkuu wa CUF wakati huo pamoja na mwenyekiti wake profesa Ibrahim Haruna Lipumba ulipokuwa umepamba moto na kufikia kiwango cha juu kabisa cha uhasama, kati ya mafahari na majabali hao wawili na ambao walikuwa wametoka mbali sana kisiasa na kushibana kwelikweli kiurafiki na waliokuwa wasomi wasiotiliwa mashaka na mtu yeyote na wenye misimamo isiyo yumba wala kuteteleka na wenye kuaminiwa vilivyo na wafuasi wao waliokuwa wapo tayari kufa kwa ajili yao.

CHADEMA ilijitahidi sana na kwa nguvu zote na kwa mbinu zote kujipendekeza sana kwa hayati Maalim Seif ili akitoka tu cuf aweze kujiunga nao.hii ni kwa kuwa CHADEMA ilikuwa na haijawahi kuwa na nguvu wala kukubalika wala kuungwa mkono wala kupewa kura wala kuwa na wananchama wengi upande wa zanzibar.hii ni kutokana na asili yake ya kuwabagua na kuwachukia waziwazi wazanzibari na kuona kana kwamba ni vizingiti vyao katika kupata madaraka,ndio maana wazanzibari hawaipendi kabisa wala kutaka kuisikia wala kuiona wala kutaka kabisa kujihusisha nayo CHADEMA na harakati zake,kwa kuwa wanatambua kuwa ni chama kilichojaa ubaguzi na chuki kubwa kwao.

Hivyo CHADEMA wakawa wana mmezea mate sana hayati Maalim Seif ili ajiunge naye na watembelee nyota yake na kupata nguvu kwa upande wa Zanzibar kupitia mgongo wake na heshima kubwa aliyokuwa amejijengea kwenye mioyo ya wazanzibari mpaka kesho. Lakini kwa kuwa Maalim Seif alikuwa ni mtu mwenye akili nyingi,hekima,busara na maono ya mbali alikataa kabisa kujiunga wala kufikiria wala kuwa na wazo la kwenda kujiunga na CHADEMA na badala yake akaenda kujiunga na kuwa mwanachama wa ACT WAZALENDO, jambo ambalo liliwauma sana tena sana na kuwaumiza sana CHADEMA mpaka kesho walipoona uamuzi huo wa Maalim Seif anakwenda kwa hasimu wao Mheshimiwa Mwami Zitto Zuberi Kabwe ambaye walikuwa wanamchukia sana na kumuombea mabaya matupu.

Na kweli baada ya kujiunga na act wazalendo chama kikapata mapokezi mazuri kwa wazanzibari na kuungwa mkono wakati wa uchaguzi na hatimaye kuingia kwenye serikali ya umoja wa kitaifa ya Zanzibar chini ya Mheshimiwa Daktari Husseni Mwinyi. jambo ambalo likawa ni kama kuwapokonya Tonge mdomoni CHADEMA waliokuwa wanamtamani Maalim Seif awe mwanachama wao.

Kwa hiyo wenye akili walishaitambua kuwa CHADEMA ni chama chenye ubaguzi sana kwa misingi ya aina zote.kuanzia Udini ,ukabila,ukanda na jinsia. CHADEMA ni chama ambacho kinawaweka watu katika madaraja kutokana misingi ya ubaguzi iliyoota mizizi ndani ya chama hicho kinachoendelea kupoteza ushawishi kwa watanzania kila uchwao. Ni matarajio yangu kuwa chama hiki kitaendelea kupukutika katika mioyo ya watanzania kila siku na hatimaye kubakia kama ilivyo Nccr mageuzi leo ambayo iliwiki sana na kutamba sana enzi na wakati wake.

Dhambi ya ubaguzi ni mbaya sana ndugu zangu na nawaambieni ya kuwa dhambi hii itaitafuna sana CHADEMA hii ambayo imeamua kujiweka wazi kwa mbegu hii iliyokuwa inafichwa fichwa kwa miaka mingi.

Ni CCM Pekee iwezayo kuliongoza Taifa letu na kulifanya likaendelea kuwa na umoja, mshikamano na utulivu.ni CCM Pekee iwezayo kuongoza na kuwafanya watanzania kushirikiana kwa pamoja na kuishi kwa pamoja bila kubaguana kwa misingi ya aina yoyote ile.hao wengine kama CHADEMA tukirogwa tukawapa nchi watalipasua na kuligawa Taifa letu vipande vipande. Na tutaanza kuishi kwa kuangaliana sura zetu ,pua zetu,dini zetu,makabila yetu ,mikoa yetu na rangi zetu.watatugawa na kutufanya tuanze kuchinjana na kupigana sisi kwa sisi. CHADEMA ni chama cha hovyo sana tena sana na hatuna budi kukipinga na kukikataa kwa nguvu zetu zote. Tusikubali kamwe na katu kitugawe watanzania kwa uchu na uroho wake wa madaraka.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa. Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
 
Mwashambwa ntakuuunga Mkono kwenye vyoooote lkn suala la kutetea Wazanzibar kaa kimia. Ama umejitoa ufahamu ama hujawahi kukaa Zanzibar.

Narudia, kaaa kimia wale majirani sio riziki hata kwa kuomba chumvi baba tena uende wewe Mnyakyusa wa Kyela mweusi tiiii kama mkaa wa IPOLE!

Baba waskie tuu hao viumbe, usione wanajichekesha wakiwa hapa Bara, ndugu yangu waweza nyimwa huduma pahala na pesa unayo mkononi kisa una choggo.

Narudia, Mwashambwa kaaa kimia waache akina LISSU Wateme nyongo.
 
Ubaguzi kwenye chama cha siasa umeanza kwa ccm kuwabagua wazanzibar kwa kuwaita hizbu na masultan.
Ndani ya CCM hakuna ubaguzi wa aina yoyote ile na kwa misingi ya aina yoyote ile ,zaidi ya kuangalia sifa za mtu kiuongozi pamoja na uwezo wake wa kumudu na kutekeleza majukumu yake ya nafasi husika.
 
unayo hutuba ya Mh Lukuvi kanisani?
Huyu wakuja hayajui hayo.

abdulrahman Kinana aliwahi kuandika waraka mrefu sana kwenye jarida la "the Hill" kuelezea kuwa Maalim Seif akishinda Zanzibar itageuka kuwa Paradiso ya Magaidi.

Leo Lucas Mwashambwa analeta hoja kama vile CCM iliwahi kuwa rafiki wa Maalim.

Huko ACT alikokwenda Maalim Seif baada ya CCM kumtumia Lipumba kuivuruga CUF, CCM iliacha kumwibia kura?
 
Jibu hoja za Tundu Lisu kikatiba na kisheria!!

Samiah ni mzenji sio mtanganyika lakini anauza vya Tanganyika,wewe una haki ya kuuza vya Zanzibar Kwa wazungu!!?katiba yao inasema kabisa Samiah ni mzanzibari na anauza vya Tanganyika hauzi vya Zanzibar!!

Unaelewa!!?

Mi nadhani Bungee litunge Sheria ya kunyonga na kuwaua chawa!wanaliharibu Taifa sana!!
 
Huyu wakuja hayajui hayo.

abdulrahman Kinana kuandika waraka mrefu sana kwenye jarida la "the Hill" kuelezea kuwa Maalim Seif akishinda Zanzibar itageuka kuwa Paradiso ya Magaidi.

Leo Lucas Mwashambwa analeta hoja kama vile CCM iliwahi kuwa rafiki wa Maalim.

Huko ACT alikokwenda Maalim Seif baada ya CCM kumtumia Lipumba kuivuruga CUF, CCM iliacha kumwibia kura?
Mimi siyo wakuja .ndani ya CCM hatuna wakuja. Ndio maana nikasema CHADEMA ninyi ni wabaguzi sana.hiyo dhambi ya ubaguzi itawatafuna sana na kuwapukutisheni kwenye mioyo ya watanzania.
 
Back
Top Bottom