Tanzania na Comoro zajadiliana kushirikiana katika ngazi ya miji

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
1,092
728
TANZANIA NA COMORO ZAJADILIANA KUSHIRIKIANA KATIKA NGAZI YA MIJI

Balozi wa Tanzania nchini Comoro Mhe. Saidi Yakubu amekaribishwa rasmi katika mji wa Bangoi Kuoni na kuzungumza na uongozi wa mji huo kuhusu ushirikiano na miji ya Tanzania.

Katika hafla hiyo ambapo wakazi wa mji huo walimvika rasmi ukaazi wa heshima Balozi Yakubu, viongozi wake walimueleza pia kuwa huo umekuwa ni utamaduni wao wa kushirikiana na Mabalozi wa Tanzania nchini Comoro na kumueleza historia ya mji huo na Tanzania hususan Zanzibar na Tanga.

Aidha, walimueleza kuwa viongozi wa Tanzania waliowahi kutembelea mji huo ni pamoja na Marehemu Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi, Rais wa Zanzibar Mstaafu Amani Abeid Karume, Kiongozi wa Upinzani wa Zanzibar, Marehemu Maalim Seif Sharif Hamad na pia kumtajia viongozi kadhaa wa Tanzania wenye asili ya mji huo.

Kwa upande wake, Balozi Yakubu alishukuru kwa kutuzwa Ukaazi wa Heshima na kuwaahidi kuendeleza utamaduni huo na kutekeleza masuala yote yalioahidiwa na Mabalozi waliomtangulia ikiwemo kuwasaidia kuwa na darasa mahsusi la Kiswahili kwa mji huo.

Balozi Yakubu pia alipata fursa ya kutembelea maeneo kadhaa ya vivutio vya mji huo ikiwemo Msikiti wa Maajabu na pia kuona miradi ya maendeleo inayofanywa kwa juhudi za wananchi na pia Serikali.
 

Attachments

  • IMG-20241006-WA0252.jpg
    IMG-20241006-WA0252.jpg
    142.3 KB · Views: 3
  • IMG-20241006-WA0253.jpg
    IMG-20241006-WA0253.jpg
    171.6 KB · Views: 3
  • IMG-20241006-WA0254.jpg
    IMG-20241006-WA0254.jpg
    193.5 KB · Views: 3
  • IMG-20241006-WA0251.jpg
    IMG-20241006-WA0251.jpg
    113.3 KB · Views: 3
  • IMG-20241006-WA0250.jpg
    IMG-20241006-WA0250.jpg
    181.1 KB · Views: 4
  • IMG-20241006-WA0255.jpg
    IMG-20241006-WA0255.jpg
    153.3 KB · Views: 4
  • IMG-20241006-WA0256.jpg
    IMG-20241006-WA0256.jpg
    98.6 KB · Views: 3
Hahahahaa yani wewe jamaa tangu nikujue humu wewe habari zako ni za balozi Yakub tuu hata akienda kula haluwa pale Anjouan unaleta uzi haya vipi hapo Moroni kwema?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom