Ni wakati gani wachawi huroga?

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
376,176
Reaction score
871,520
Ukiuliza hili swali wengi watakuambia usiku...lakini kiuhalisia ni kwamba wachawi huroga muda wowote katika mazingira yoyote na popote.Wale wa usiku ni wanga na washirikina tuu.

Mwanga kazi yake kubwa ni kufurahisha nafsi kwa kukuchezea na kukuchosha lakini hana madhara kivile.

Mshirikina ni mpiga dili na mfanyabiashara ni mtu wa kati huyu ndio mhusika mkuu wa kupeleka kwa wachawi zana za kufanyia madawa kama nywele damu, nguo, nyayo, kucha, viungo vya binadamu kulingana na mahitaji nk nk..

Mshirikina hana muda bali huangalia ni saa ngapi na sehemu gani sahihi ya kufanya yake ili apate alichokusudia (kumbuka mshirikina pia anaweza kuwa mwanga au mchawi )

Sasa basi mchawi yeye ndo yule anayejiita au kujifanya mganga wa kienyeji huyu anacheza na fani zote tatu uchawi ushirikina na ulozi.

Ni mchawi huyu huyu anayeweza kukuroga kwa kutumia ushirikina wake kisha akakutibu kwa kutumia uganga wake ni michezo tu ya kucheza na zana.

Mchawi na mshirikina huweza kufanya mambo yao popote na vile jinsi wapendavyo wao japo kupitia ushirikina hupata vitendea kazi na kupitia uchawi huweza kutoa tiba.

Mpiga zongo ni mchawi si mshirikina japo anatumia ushirikina kukupiga hilo zongo.

Ukikuta umewekewa madawa sehemu jua ni mchawi katumia ushirikina kufanya yake



Lakini usihadaike wala kubabaika siku hizi uchawi wa kweli unapotea kilichobaki ni stori na mazingaombwe.

Kitakachokuumiza ni imani yako na woga wako.Simama na Mungu wako utafunuliwa mengi.
 
Bro si ni bado kama saa moja na nusu ndo waanze mambo yao? Kwenye training akipatakana mchawi mmoja ambaye yuko single please let me know! Sijawahi kubahatisha kada hii!
 
Mkuu, kwa kuwa wachawi wana tabia ya kujaribu watu haswa wageni, umeshawahi kukumbana na hizo test?
 
Mkuu naomba kuuliza katika siku za juma ni siku ipi huwa nzuri sana kwa wachawi, mashetan kufanya kaz zao?
 
Tueleweshe zaidi mkuu...baada ya kutoka chooni ilikuaje??
 
Mkuu naomba kuuliza katika siku za juma ni siku ipi huwa nzuri sana kwa wachawi, mashetan kufanya kaz zao?
Nijuavyo hakuna siku wala saa maalum japo siku za jumanne na Ijumaa hupendwa zaidi..hebu ngoja jichawi aseme neno
 
Hii mada naisoma wakati nna mshangao hasa...nimeamka muda huu mahali nimekuta nilipoweka kichwa usiku(nilipogeukia) sipo nilipoamkia asubuhi hii,hali hii haijawahi kunitokea hata siku moja na sina kawaida ya kuhama nikilala...Ngoja nizidishe maombi asee!
 
Mshana Jr na jichawi....kuna kitu kimetoke Busega...kuna mtu alifariki 2014 sasa ameonekana juzi...na hawez kuonge ni kama vile mtoto mdogo anavyoanza kuzungumzaaa....taratibu zinafuata za kwenda kufukua kaburi.....je nini huwa wanaweka.....jaman uchawi upo na tena una nguvu..
 
Mkuu mbona stori imeishia njiani.. What next. Very interesting story
 
Kama alichukuliwa msukule huko kaburini mtakuta gogo...huyo alichukuliwa kimazingara na facts nyingi ambazo zimesababisha aonekane tena
 
Kama alichukuliwa msukule huko kaburini mtakuta gogo...huyo alichukuliwa kimazingara na facts nyingi ambazo zimesababisha aonekane tena
Huwa nasikia......kuna mengine kule huwa na viburi huwapiga hata kuwafanyia fujo ...na kupelekea kuwarudisha au pia ndugu kucheza na kamati za ufundi...

Kumbe unaeza kutengenezewa ajali...halafu wakakuchukua msukule....na kwa nini?
 
Hiyo sentesi ya mwisho nimeikubali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…