Ni vyuo gani vya Serikali vinatoa diploma ya ualimu wa shule ya msingi?

Ingekuwa amri yangu ningekushauri hiyo ada ungaeanza uwekezajihata kwenye kilomo mapema kidogo kidogo naona tumetupa pesa nyingi kusoma wakati ajira sumbufu na mshahara kijiko
 
Ingekuwa amri yangu ningekushauri hiyo ada ungaeanza uwekezajihata kwenye kilomo mapema kidogo kidogo naona tumetupa pesa nyingi kusoma wakati ajira sumbufu na mshahara kijiko
Hao wanao force kusoma wanatokea huko huko mtaani mambo sio rahisi Kama usemavyo at kilimo


Anyway mleta mada fuatilia hivi

Dakawa ttc

Butimba ttc

Morogoro ttc

Bustani ttc

Nyingine Google usiwe mzembe utafeli Tena ooh
 
Habari , Ninaombeni Msaada wa Vyuo vya Serikali vinavyotoa Diploma YA Ualimu wa Shule YA Msingi
Vyuo viko Vingi sana Mkuu ingia kwenye Tovuti ya Wizara ya Elimu utakuta Orodha yake kuanzia Vikindu TC, Korogwe, Butimba, Tabora, Morogoro nk nk viko vya kutosha. Achana na stori za Vijiweni kwamba walimu wanatosha. Mpeleke Kijana wako asomee masomo adimu kama Sayansi, Kiingereza na Hesabu Ajira bado zipo. Walimu waliopo wanastaafu, kupangiwa majukumu mengine, Shule mpya zinajengwa, Idadi ya watu inaongezeka maaana Wanafyatua tuuu wakijua elimu ni bure. Kwahiyo walimu bado wanahitajika sana tu usikatishwe tamaa.
Kuomba udahiri ni Tshs. 5,000/=tu kikubwa uwe na namba yake ya mtihani kidato cha nne na sita.
Kazi njema
 
Ila kwa ushauri wangu acha kupoteza muda sooon serikali inaanza kuajiri only degree qualified teacher ,ajira zenyewe unaziona
 
Ila kwa ushauri wangu acha kupoteza muda sooon serikali inaanza kuajiri only degree qualified teacher ,ajira zenyewe unaziona
Mkuu....
Kwani akiwa amesoma Diploma atazuliwa kuipata Degree?
Kwa Uchumi upi serikali iajiri mwalimu wa Degree kufundisha Msingi wakati wale waliojiendeleza na kuipata hiyo Degree wanaondolewa. walimu wa Degree Wage Bill yao ni kubwa kulinganisha na Cheti au Diploma.
Je, huko Vyuoni wameandaliwa kufundisha msingi au sekondari?
Unachosema siyo jambo la kufumba na kufumbua Mkuu linahitaji muda na mipango pia.
 
Back
Top Bottom