Mzee Mwinyi akiwa na Diploma ya Ualimu Ndiye aliyeleta Mageuzi ya Kiuchumi na Kisiasa, Kumbe PhD siyo Muarobaini!

secular education ni overrated sana. Kiufupi hata uwe na PHD haikufanyi wewe uwe ndio unajua kila kitu.

Moja ya sifa kubwa za uongozi ni Hekima, Busara, kusikiliza ushauri wa wengine kitu ambacho mzee Mwinyi alikua nacho na hao viongozi wengine wenye elimu kubwa walikosa.
 
Ndio uongozi ni karama, ila ukiongeza na elimu nzuri utajiamini zaidi. Angalia Msukuma bungeni anavyochangia hoja ila hajiamini kwa sababu ya elimu. Kiongozi unatakiwa ukisimama mahali popote ujiamini, mf. GDP utaijuaje kwa undani kama hujapiga kitabu? Utawahutubiaje wanafunzi wa chuo kikuu na elimu yako ndogo?
 
Wasomi level ya PhD huwa wagumu sana kushaurika wengi hujiona Wanajua Kila kitu
Na hili ndo tatizo kubwa sana, ukimshauri tu kama wewe sio msomi kama yeye basi ili kukudhoofisha ataanza viingereza hapo ili akutengenezee hofu.
Mifano ya kitabuni ya kilatini na kifaransa mpaka wachina watatajwa ili tu uache kumshauri uone yeye yko sahihi.
 
Mkuu tunapaswa kutofautisha vitu viwili, elimu na akili. Elimu ni utaratibu wakuambukizwa akili na maarifa ya watu waliyoyatoa kichwani mwao wakauaweka kwenye makaratasi ambayo sisi tunapaswa kuyasoma na kuyakariri kama yalivyo au kuyasoma na kuyaelewa na kutumia akili yako namna yakuyatumia kwa manufaa yako au ya wengine.

Akili ni kile binadamu anachozaliwa nacho yaani kipo kichwani mwake ambacho anaweza kujiongoza kuishi na kukabili mazingira aliyonayo. Yaani akili ni kile mtu anachoweza kufanya mwenyewe bila support ya mtu yeyote na hili utalijua endapo utawapa watu tofauti wafanye jambo moja bila kufundishwa na hapo utaona kila moja anafanya kwa namna yake.
 
Wasifu wa hayati Mwinyi unasema Elimu yake ni Diploma ya Ualimu aliyoipata nchini Uingereza

Natafakari namna Diploma ya Ualimu ilivyotuletea mabadiliko makubwa tena chanya ya Kiuchumi na kisiasa

Walimu shikamoo

RIP Mwalimu Mwinyi
Tuwekee clips za mwalimu Nyerere akikemea Ikulu kufanywa pango la walanguzi!!

Tuache kujipendekeza kwa wafuasi wa waarabu
 
Apumzike kwa amani mzee wa watu asiye na tuhuma zozote za ufisadi wala umungu mtu, mzee wa ruksa na mzee wa Siasa safi, wazee wengi ambao leo hii ni matajiri wakubwa walianza kufanikiwa kipindi chake, baada ya yeye kuichukua nchi ikiwa kwenye lindi la umasikini na kuanza kuiinua kiuchumi, hata mwanaye Hussein anafaa kuiongoza hii nchi maana naye aonekana ana kaliba kama ya baba yake, bora hii nchi aendeshe yeye kuliko kina Kikwete, Makamba na magenge yao ya wahuni
 
Back
Top Bottom