Ni vita Arusha

PISTO LERO

JF-Expert Member
Mar 8, 2011
2,819
1,454
Juzi niliweka bandiko hapa juu ya mapigano kati ya wamasai na waarusha ugomvi ambao mpaka sasa unaendelea POLISI NA FFU wameshindwa kuwaamulia na sasa JWTZ wameingilia kati na mafanikio yanaonekana kwa mbali kwani silaha zinazotunika ni zajadi yaani MASIME,MIKUKI NA MISHALE ugomvi ni kugombea maeneo ya malisho ambapo ndani ya eneo hIlo kuna shule ya sekondari ya OLDONYOSAMBO wanafunzi wameshindwa kutoka eneo la shule kutokana na mapigano hayo nyumba na mali kadhaa zimeteketezwa kwa moto,watoto wamepotea pamoja na mifugo.NASIKITIKA SAMA MOODS WAKAITOA BILA SABABU NILIGHAFILIKA SANA.
 
We mbona habari zako kila siku za machafuko tu. tafuta habari angalau moja ya kawaida ulete.
 
Hakuna waarusha,wote ni maasai.wewe ndo unachemka.iyo ni vita ya mtu na mtu

nduguyangu kunatofauti katiya wamasai na waarusha hizi ni kabila mbili tofauti na kama wewe ni mgeni hapa arusha itakuchukua muda kutambua tofauti hiyo.wanafanana karibu kila kitu mpaka mila.
 
Juzi niliweka bandiko hapa juu ya mapigano kati ya wamasai na waarusha ugomvi ambao mpaka sasa unaendelea POLISI NA FFU wameshindwa kuwaamulia na sasa JWTZ wameingilia kati na mafanikio yanaonekana kwa mbali kwani silaha zinazotunika ni zajadi yaani MASIME,MIKUKI NA MISHALE ugomvi ni kugombea maeneo ya malisho ambapo ndani ya eneo hIlo kuna shule ya sekondari ya OLDONYOSAMBO wanafunzi wameshindwa kutoka eneo la shule kutokana na mapigano hayo nyumba na mali kadhaa zimeteketezwa kwa moto,watoto wamepotea pamoja na mifugo.NASIKITIKA SAMA MOODS WAKAITOA BILA SABABU NILIGHAFILIKA SANA.

Mkuu ni kweli nimehakikisha mwenyewe, maana nilienda mpaka eneo la tukio, majeruhi wengine wameletwa hospitalini Seliani
 
Inaonekana as if you're blowing it out of proportions.Hayo ya kugombea maeneo ya malisho ni kawaida sana maeneo hayo,sasa unaposema "Ni vita Arusha",ndo hapo unayakuza zaidi.Anyways,tunatoa pole kwa waliopoteza maisha pamoja na mali zao kwenye mgogoro huo.
 
Mkuu ni kweli nimehakikisha mwenyewe, maana nilienda mpaka eneo la tukio, majeruhi wengine wameletwa hospitalini Seliani

dunia ya sasa haiitaji maneno tu; wanasema "a picture is worthy a thousand words". Kama ulienda na kuona mwenyewe ungejaribu kupiga picha au kuweka ushahidi fulani. Bila picha watu wanaona siyo jambo zito kihivyo? Si umeona mambo ya kule Iringa? Bila picha Watanzania wangelishwa kila aina ya bs.. but the picture stands as a silent witness.
 
POLISI WA TANZANIA,uwezo wao ni mdogo katika kuthibit matukio kama hayo ila wanasubir waje mjin kwenye mikutano ya siasa
 
dunia ya sasa haiitaji maneno tu; wanasema "a picture is worthy a thousand words". Kama ulienda na kuona mwenyewe ungejaribu kupiga picha au kuweka ushahidi fulani. Bila picha watu wanaona siyo jambo zito kihivyo? Si umeona mambo ya kule Iringa? Bila picha Watanzania wangelishwa kila aina ya bs.. but the picture stands as a silent witness.

Uko sahihi Kaka, tatizo nilienda jana majira ya jioni, wakati mapigano yameshapungua kutokana na nguvu ya polisi. pia kwa kuwa nilienda kikazi, na kutokana na nature ya kazi yangu sikuweza kuchukua picha, ukizingatia hali ilinilazimisha. In fact nilienda kwa ajili ya evacuation strategies. Ndiyo maana sikuanzisha thread kutokana na kutokuwa na picha!
Ni kweli kuna mapigano, hata hivyo kwa leo hayakuwa na nguvu kama siku tatu zilizopita.
 
Arusha is safe wakuu....Leo tulikuwa na mbunge wetu viwanja vya kilombero....
 
Katika mambo ambayo yanaipasua serikali kichwa ni suala la wafugaji na mifugo yao.
tusije shangaa nchi nzima ikigeuka jangwa.
poleni wote mliokumbwa na masahibu haya.
 
Mimi ni mzaliwa wa mkoa wa Arusha. Ningependa kukuthibitishia kwamba kuna tofauti kati ya Waarusha na Wamaasai.
Tofauti yao ni kuwa wamasai ni wafugaji na waarusha ni wakulima lakini ni kabila moja. Soma historia ya wamasai utajua kuwa ni kabila moja lenye mila na dasturi moja.
 
Katika mambo ambayo yanaipasua serikali kichwa ni suala la wafugaji na mifugo yao.
tusije shangaa nchi nzima ikigeuka jangwa.
poleni wote mliokumbwa na masahibu haya.
cha kusikitisha hawa wanaopigana ni ngugu kabisa kwani wanaoana hivyo hapo wanaopigana ni mashemeji, wakwe, wajomba, kaka, baba, nk. Jana walimkataa mbunge wa Longido asiwepo katika kikao kati yao na uongozi wa mkoa. Ilibidi akae ndani ya gari. Eneo hilo linawagusa wabunge watatu; wa Monduli, wa Longido na wa Arumeru Magharibi. Hao wawili hawakuwepo eneo la tukio jana. Na sidhani kama wangetokea wangekubaliwa.
 
Wamtumie Lema hawapatanishe si nasikia anakubalika Arusha nzima.
 
ndio anakubalika na hilo linawezekana pia......ila kama wewe si mchochezi.....kuna mtu amewataja wabunge wanaohusika na eneo hilo....wewe Lema kakutoka wapi.....?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom