Ni vibaya binti kumnunulia baba yake boxer?

Ulikuwa unafanya kosa lipi? Hakuna kosa hapo

kwa mawazo ya wengi kosa nlilofanya ni kununua nguo za.ndani..ila zingine naweza..sasa kwangu niliona ni sawa tu
 
Sidhani kama nikweli

ukweli gani kaka..mimi mwenyewee nilinunua tena nikizihesabu zote zaweza fika 25 na si ajabu siku namnunulia mama nayeye ningemfungia za kwake kama si huyo mdada kunishtua ndo nkasema niulize humu mawazo ya wengi niyazingatie..nimejifunza kumbe kwa wengi ni kosa so sitarudia tena
 
Otakuwa ulianza ww kununuliwa pichu hapo umerdsha fadhila kwa dingi yako
 
Kibongobongo wengine wanaona mishe, nlivokua korea ni kama tradition mtoto wa kike na kiume wote wakipata mshahara wao wa kwanza wanawanunulia wazazi wao nguo za ndani...

huko inawezekana ila kwa hapa mawazo ya watu.wengi nimeona ni kosa..ingawaje kwangu mwanzoni niliona ni sawa kabisa
 
Otakuwa ulianza ww kununuliwa pichu hapo umerdsha fadhila kwa dingi yako

Wala..na hata hivyo sina mazoea ya kariibu zaid ya kumheshim kama babangu..nimegundua ni kosa ndugu so siwez kufanya vile tena..
 
Boxer ni kuvuka mipaka. Mama akijua atakutoa maini
 
alivonishauri huyo dada mtu mzima ambae naweza kumwita mamdogo ni kwamba sistahili kumnunulia baba zawad yeyote kwani mim ni mke wa mtu napaswa kumnunulia mama tu na.mume wangu..ila sijamaanisha boxer tu
ameline . Pamoja na ukubwa wa huyo aliyekuambia kuwa kwa vile umekuwa mke wa mtu ..basi hustahili kununua zawadi kwa wazazi!!!! sikubaliani kabisa. Endelea kuwatunza wazazi wako mana wakivaa mararuraru wakati uwezo kidogo unao ni aibu sana. Labda ntakushauri hizo boxer usinunue wewe tena.... mpe hela mama anunue yeye. Tatizo ni kuwa kama mama yako angekukataza toka mwanzo isingekuwa shida. Pole
 
Last edited by a moderator:
Boxer ni kuvuka mipaka. Mama akijua atakutoa maini

ungesoma mpaka mwisho ungenipata..mama nfi huwa nampa zawad.zote yeye ndo hutoa zake na za baba.humkabidhi mwenyewe..na hajawahi.kuniambia kama ni vibaya ama laa..but leo nimejifunza hapa kuwa ni vibaya so siwez rudia tena...
 
Nashukuru sana sana mwana ally kwa mawazo mazuri..ni kweli unavisema ningekatazwa muda mrefu nisingeweza kufanya hivyo ...ila kuanzia leo hii nimegundua ni kosa sitarudia tena...
 
Last edited by a moderator:

Kikwetu ni aibu hata kujua nguo gani ya ndani anavaa MZAZI wako. Wazazi kama wapenzi wengine hununuliana wenyewe nguo Za ndani. Mapenzi yako onyesha kwa nguo Za kawaida na zawadi zingine.
 
Kikwetu ni aibu hata kujua nguo gani ya ndani anavaa MZAZI wako. Wazazi kama wapenzi wengine hununuliana wenyewe nguo Za ndani. Mapenzi yako onyesha kwa nguo Za kawaida na zawadi zingine.

shukrani..nimekusoma ndugu nitazingatia
 
alivonishauri huyo dada mtu mzima ambae naweza kumwita mamdogo ni kwamba sistahili kumnunulia baba zawad yeyote kwani mim ni mke wa mtu napaswa kumnunulia mama tu na.mume wangu..ila sijamaanisha boxer tu
Huu ni ushauri wa kipuuzi. Kila mtu ana mila desturi na mazoea yake muulize sababu zake za msingi zinazofanya asimnunulie baba yake zawadi. Inawezekana wana ugomvi na anafanya hivyo kumkomoa baba yake
 
asante ndugu nimekuelewa nitalifanyia kazi..mdo maana nimetaka ushauri wa wengi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…