ameline
JF-Expert Member
- Jan 8, 2013
- 2,292
- 1,152
Wana MMU naombeni msaada wa ushauri..
Kabla sijaoewa nilikua na tabia ya kuwanunulia wazazi wangu zawad mbalimbali..mfano nikimnunulia mama vitenge au makatalogi yaliyotoka baba nae humnunulia mashati, suruali, viatu, mikanda n.k nikinunua underware za mama na nguo nyingine za ndani bas na baba namnunulia vilevile boxerz, pants,vest n.k na huzipeleka kwa pamoja..walikua wameshazoea na kuzifurahia zawad..na nilifanya hivi kwa muda mrefu tu na nlikua sina ubaguz wa mzaz yeyote.wote wanapata.
baada ya kuchumbiwa pia sikuacha hata mchumba wangu aliona wakat nanunua zawad.hizo na wakat mwingine tunachagua wote nae akimnunulia.mama yake.
Baada ya.kuolewa sasa..siku moja nikanunua kama kawaida makadet na mashati pamoja na nguo za mama na wakwe zangu kama zawadi nikamwita mdogo wangu aje dukani kuchukua za wazaz wangu awapelekee.sasa rafiki yangu nliekua nae akanambia unafanya nini? unamnunulia babako nguo mpaka leo? wewe mke wa mtu acha mke wake (mama yangu) amnunulie! hutakiwi kumnunulia tena! mnunulie mama tu! mh na.maneno mengi tu aliongea yaliyonikatisha tamaa mpaka ikabidi nisitishe zawad hizo mpaka leo sijawahi tena kuwanunulia sio baba wala mama kwani naogopa kumpa mama bila baba kwani nilishazoea kuwapa wote.
Nauliza jamani;: kuna ubaya wowote kwa binti alieolewa kumnunulia baba yake zawadi kama nguo na nguo za ndani n.k?
sina amani najisikia vibaya kwani wazaz wangu wataona nimewatelekeza tangu niolewe hakuna zawadi tena..naombeni mnisaidie wale wenye uzoefu na haya mambo jamani.