Ni Uvivu au kutokuwa na weledi kwa watumishi wa umma. Utendaji kazi wao ni zaidi ya ufanisi dhoofu

Paploman

JF-Expert Member
Apr 13, 2019
1,720
3,237
Kufatilia huduma katika mashirika ya Umma kunakera sana.

Kuna ujinga na kujisahau sana kwa watumishi sijui shida ni nini? Kwa mfano

Taasisi nyingi zina namba za simu za huduma kwa wateja ila ukipiga hazipokelewi ama hazipatikani kabisa, tatizo ambalo ungetakiwa ulisolve ukiwa kigoma tena kwa saa kadhaa linakulazimu uje Dar ambako unakutana na mlolongo wa watumishi wavivu wanakuweka siku kadhaa bila kujali hali yako ya kiuchumi na gharama unazoingia kwa jambo ambalo linaweza kumalizika kwa haraka.

Huko Hospitalini ni majanga Sina hata haja ya kueleza.

Kuna ishu ya Hawa TANESCO ndio wamefanya niandike, Kuna kibanda changu nimemjengea Bibi yangu kijijini sasa nimefanya process zote za kuvuta umeme, kufika hatua ya kupata control number Ili nilipe waniingizie umeme imekuwa shida.

Mwezi wa pili sasa unaelekea wa tatu control number hakuna yaani unafatilia mpaka unachoka, ukipiga simu personal hawapokei wanaona kama kero,. Ukiwafuata ofisini wanakuambia kesho, kesho imekuwa kesho....

Control number ya kusubiria kwa zaidi ya miezi miwili? Halafu bado tunataka tuendelee kama taifa

Halafu, nyie watumishi kama hamzipendi kazi zenu acheni muendelee na majukumu mengine maana mnafanya ufanisi wa serikali unakuwa mdogo

Hawa watu hawafai kabisa kuongezewa mshahara maana ni wavivu sana.
 
Taasisi nyingi zina namba za simu za huduma kwa wateja ila ukipiga hazipokelewi ama hazipatikani kabisa, tatizo ambalo ungetakiwa ulisolve ukiwa kigoma tena kwa saa kadhaa linakulazimu uje Dar ambako unakutana na mlolongo wa watumishi wavivu wanakuweka siku kadhaa bila kujali hali yako ya kiuchumi na gharama unazoingia kwa jambo ambalo linaweza kumalizika kwa haraka.
Hata ukiwatumia 'email' hawajibu kabisa, nadhani hizo email zipo kama geresha tu.
 
Hata ukiwatumia 'email' hawajibu kabisa, nadhani hizo email zipo kama geresha tu.
Kuna hawa MCT -baraza la usajili wa madaktari, utapaata control number ,utalipiwa leseni ila haiwi printed mpaka uende manually,yaani mtu atoke kigoma mpaka Dodoma kufuata leseni
Nacho nzima ofisi ipo Dodoma,nchi hii ni ya hovyo sana
 
Back
Top Bottom