Ni ushuhuda ambao umeniumiza kuusikia..... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni ushuhuda ambao umeniumiza kuusikia.....

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by FirstLady1, Jun 18, 2011.

 1. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #1
  Jun 18, 2011
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Nilikuwa naangalia kipindi cha Mimi na Tanzania kinachoongozwa na Hoyce temu..
  Chanel Ten
  Ni kuhusu mtoto Shigella William yatima anayeishi Mwanza 14 years old na anayeishi na Virus vya ukimwi..
  Na kionekana zaidi ni muumini wa dini ,aliekuwa na imani thabiti juu ya Kikombe cha babu..
  kwa imani yake Alienda kunywa Kikombe cha babu Loliondo na aliporudi baada ya siku 21 aliamua kwenda kupima na kujua kama amepona..
  Hoyce alimpeleka Clinic kupima na vipimo vyake kuonyeshwa kila hatua lakini majibu yalionyesha bado ameathirika..
  Lakini alipopokea majibu hayo alinyong'onyea kidogo na bado aliendelea kumshukuru mungu kwa kila kitu na kisha kusali..
  ooh my god ameniliza na ushuhuda huu umeniumiza moyoni na kubaki natafakari kwa huzuni sana ..
  Nimeamini kweli Loliondo ni imani ya mtu ..
  Nijulisheni wenzangu inakuwaje wengine wanatoa ushuhuda wamepona na wengine hawaponi...
  Iweje mtoto mdogo kama Shigella anayeonekana ni mwingi wa imani hakupata uponyaji huu???na ugonjwa wake inavyoonekana alipata maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto
  Nafedheheka sana wadau.... weekend yangu imekuwa ya mawazo...Muwe na weekend njema yangu si njema tena
   
 2. Mamzalendo

  Mamzalendo JF-Expert Member

  #2
  Jun 18, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 1,664
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Ndugu yangu Mungu hachelewi wala hawahi hufanya jambo lake kwa wakati anapoona sawa,asikate tamaa siku yake inakuja tu,
   
 3. Egyps-women

  Egyps-women JF-Expert Member

  #3
  Jun 18, 2011
  Joined: Feb 5, 2010
  Messages: 499
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  mambo ya imani haya mungu amponye mtoto huyu
   
 4. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #4
  Jun 18, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Huo nao ni ushuhuda,kwamba kumtegemea Mungu si pale tunapopokea miujiza tu,hata pale tunapotegemea miujiza na hatuipokei bado Mungu atabaki kuwa Mungu na Baba yetu anayetupenda na kutupigania na ambaye anajua kuzaliwa,kuishi na kuondoka kwetu Mungu amzidishie nguvu Shigella,azidi kumshuhudia Mungu kwa mema mengi na maisha yake,jambo loliondo lisimfanye asahau baraka nyingi.

  Usisononeke FL1,sote tuko safarini na tunapitia mitihani tofauti. Mungu atupe nguvu na ujasiri.
   
 5. C

  ChiefmTz JF-Expert Member

  #5
  Jun 18, 2011
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 2,513
  Likes Received: 286
  Trophy Points: 180
  Namwombea awe na subira. Mwenyemungu hupenda wenye subira na watenda mema. FL kuwa jasiri mungu atampa heri yake mapema tu. Just a matter of time
   
 6. Nanren

  Nanren JF-Expert Member

  #6
  Jun 18, 2011
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 1,739
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Michelle,
  Umeshusha nasaha kama mama yangu mzazi...
  Thanks.
   
 7. Blaki Womani

  Blaki Womani JF-Expert Member

  #7
  Jun 18, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 8,459
  Likes Received: 3,713
  Trophy Points: 280
  watoto wa ain ahiyo wapo wengi kinachotakiwa kuwap upendo wa dhati kutoka jamii inayowazunguka nao watajiona sawa mbele ya watoto wengine............... kuzidi kuwaombea Mungu awape nguvu.............. kuhusu dawa tumesikia ni kwa imani zaidi basi imani aliyonayo ya uponyaji ipo siku itatimia.... tuwaombee watoto wa aina hii kila mara
   
 8. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #8
  Jun 18, 2011
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Sijakiona kipindi hicho FL ila una moyo wa huruma.
  Mtoto wa aina huyo tunajua huwezi kuonana naye uso kwa uso, lakini kwa mazingira yaliyopo piga magoti mwombee na Mwenyezi Mungu naye anasikia, hakosi kusikia.
  Nami kabla ya kulala nitaomba ili Mungu ayapunguze mateso ya kijana huyo.
   
 9. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #9
  Jun 18, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,402
  Likes Received: 736
  Trophy Points: 280
  Mungu anatenda kwa namna ambayo binadamu hatuelewi...anatenda kwa muda wake...imani yake inatakiwa kuwa juu ya Mungu na sio kikombe cha babu.
   
 10. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #10
  Jun 19, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 254
  Trophy Points: 160
  Binafsi sijabahatika kuona kipindi hicho lakini roho yangu huniuma sana naposikia mtoto kapata maambukizi kutoka kwa Mama nasikia uchungu kuliko.

  Nimejifunza sana leo kanisani kuwa tusiwe tunaishi kwa kuwaza kesho au baada ya muda fulani what will happen to our life.

  Let me say this as an example: Mimi naishi na wazazi wangu Mpitimbi but wakati niko na rafiki zangu weekend nikachelewa kurudi home na Baba na Mama ni wakali ile mbaya sasa wakati narudi naanza kupanga uongo wakusema may be nilikosa usafiri mama atauliza kwanini hukupiga simu nitamwambia simu ilikwisha charge ataniuliza yaani wewe hujui simu yangu kwa kichwa hata upige kwa call box?? Nitatunga tena uongo mwingine hiyo ni moja then anather day nitafanya kitu kama hicho huku nikiogopa sana nakuanza kupanga majibu meeengi na nikirudi home si mama wala baba atakayeniuliza ulikuwa wapi umechelewa wapi yale majibu yanguuu yoote yameyeyukia hapo na nimepoteza wakati wangu kwa kufikira mambo ya what will happen.

  Usiku mwema wapendwa I just feeling so bad nikisikia mtoto anapata shida
   
 11. A

  Ave Ave Maria JF-Expert Member

  #11
  Jun 19, 2011
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 10,757
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 0
  Japo sikukiona hicho kipindi lakini imenigusa sana. Tusielekezee sana imani kwa babu bali tumwachie mwenyezi Mungu ye atajibu kwa wakati wake, mapenzi yake yatimizwe. Amina
   
 12. KakaJambazi

  KakaJambazi JF-Expert Member

  #12
  Jun 19, 2011
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 15,012
  Likes Received: 3,197
  Trophy Points: 280
  yaani kwa jinsi ulivyosimulia, nimehisi kuumia kama vile nimeona live.
   
 13. babayah67

  babayah67 JF-Expert Member

  #13
  Jun 19, 2011
  Joined: Mar 28, 2008
  Messages: 493
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Pole kaka kwa mfadhaiko huo ulioupata kutokana na kikombe cha babu. Jibu la kwanini watu wengi hutoa ushuhuda wa kupona wakati hali halisi ni kama hiyo kesi ya mtoto Shigella linapatikana katika kisa kimoja cha Abunuwasi. Kisa hicho kinaanza kama ifuatavyo:

  Hapo zamani za Kale alikuwepo mfalme mmoja aliyekuwa na watoto wawili,wa kwanza (mkubwa kuzaliwa) akiitwa Abunuwasi na wapili akiitwa Harounrashid (mdogo). Basi siku moja moja baba yao akamwita Abunuwasi akamwambia siku nikifa, unuse pua zangu ukisikia harufu mbaya basi ujue ufalme haukufai na usirithi ufalme wangu. Basi ikatokea siku yasiku Baba huyo akafariki, na Abunuwasi akafanya kama alivyoambiwa, na aliponusa pua kweli akanusu harufu mbaya, na akasema sitaki kuwa mfalme kwa sababu mungu kaniambia nisiwe mfalme. Wananchi wake wakasema basi mdogo wako atakuwa mfalme, lakini hebu tuambie huyo mungu wako uliongea naye kweli??? Akawaambia ni kweli na mkitaka kumwona nitaongea naye atakuja nanyi mtamwona isipokuwa kwa mtoto wa haramu hataweza kumwona!!!! Basi Abunuwasi akatengeneza kijichumba, akaweka kiti, na kulikalisha sanamu kubwa. Sanamu hilo akalishikisha bakora mkono wa kushoto na kulia akilishikisha Tasbihi/Rozari kuubwa saana. Basi akamwambia mfalme (mdogo wake) awaite watu woote waje kumwona mungu. Lakini akasisitiza kuwa MTOTO WA HARAMU HATAWEZA KUMWONA!!!!!! Basi watu wakaitwa wakaja kwa wingi saana, na Mfalme akawa mtu wa kwanza kwenda kumwona mungu. Lakini alipoingia ndani, aliona li sanamu lililovalishwa Tasbihi/Rozari na lisilosema chochote. Mfalme akasema mbona huyu sio mungu, lakini akakumbuka kuwa akisema kuwa hakumwona mungu yeye atajulikana kuwa ni mwana wa haramu, basi alipotoka nje akasema ni kweli nimemwona Mungu. Basi hali ikawa hivyo kwa waziri mkuu, na wote waliofuatia, japo hawakumwona mungu lakini hakuna aliyethubutu kusema kuwa lile ni sanamu na sio mungu kweli kwa hofu ya kuambiwa yeye ni mtoto wa haramu.
  Kama ilivyo katika kisa hiki, basi hali hiyo ndio iliyopo kwenye Tiba ya Babu wa Loliondo. Toka aanze kutoa kikombe, viongozi wengi wakubwa wameenda huko na kila mmoja akirudi unasikia kuwa amepona, hakuna anayesema kuwa hajapona kwa hofu ileile ya kuonekana kuwa ni mtoto wa haramu (yaani hana imani) kama ambavyo tiba ya babu imeegemeza uponyaji wake na imani. Hali halisi ni kama iliyoonekana kwa huyo mtoto, na imetokea kwa wengi saana wengine weshapoteza maisha!!!
   
 14. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #14
  Jun 19, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Pole sana FL1,

  Suala la babu ni zito sana. Ila namshukuru Babayah67 ameandika mambo mazito!!

  DC
   
 15. l

  lucy mboya Member

  #15
  Jun 19, 2011
  Joined: Jun 18, 2011
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  biblia inasema kila chozi litapimwa, hata chozi la mtoto huyu na wote wanaolia kuomba kwa ajili yake Mungu wetu ni mwaminifu na lililo kusudi lake ndilo litasimama.
   
 16. Dreamliner

  Dreamliner JF-Expert Member

  #16
  Jun 19, 2011
  Joined: Jan 17, 2010
  Messages: 2,034
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Pole FL1.... Yote MAISHA.
   
 17. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #17
  Jun 19, 2011
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Nilibahatika kuangalia kipindi.
  hakika inasiklitisha, ila kijana anaimani kuu ya kushinda milima, Mungu atamponya. Nilipoenda kwa Babu Loliondo neno moja lilinipa nguvu na ndio imani ya kweli. Babu anasema hata kama ukipima na kuonekana bado una VVU baada ya kunywa dawa amini utakuwa umepona. Virusi vinakluwa bado mwwilini ila havina nguvu tenda ya kukumaliza..vinakwisha taratibu, havizaliani tena....Kijana atapona kwa imani.
   
 18. std7

  std7 JF-Expert Member

  #18
  Jun 19, 2011
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 331
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 45
  Mungu ni zaidi ya kikombe cha babu aendelee kumwamini na kumtumainia. kwa kuwa hakuna neno lisilowezekana kwa Mungu. Luka.1:37;
   
 19. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #19
  Jun 19, 2011
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Natizama Marejeo ya habari ya Shiggela Channel 10
   
 20. ALLEX

  ALLEX JF-Expert Member

  #20
  Jun 20, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 2,046
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145
  shigella umepona kuwa na subira na usiwe na imani za thomasi mpaka ushike ndiyo uamini wewe nenda peke yako wala usisindikizwe na mtu wengine wana mapepo yao ......usiogope wewe tulia nenda tena
   
Loading...