Ni ushamba Tanzania kushindwa kufunga taa za mitaa!

alexelias

JF-Expert Member
Joined
Sep 1, 2017
Posts
2,032
Reaction score
3,198
Hivi hata ktk hili hadi mh Rais alitolee kauli?!

Nchi yetu inazo nyenzo zote za kuweza kufunga taa za usiku mijini hadi vijijini. Nguzo tunazalisha wenyewe hapa kwetu, kwanini wataalamu wetu msilisimamie hilo?

Nchi ndogo kama Rwanda 99% ya miji na vijijini vyao wakati wa usiku hupendezeshwa sana na taa za mtaani.Kwa nini sisi tumeshindwa!

Kwa mfano, miradi yote ya barabara mkandarasi angewekewa kipengere cha kuweka na taa kila kijiji na miji na gharama zikajumlishwa katika malipo ya mradi husika.

Jamani jambo dogo kama hilo si lazima libuniwe na Rais Magufuli. Mengine ninyi wasaidizi wake jiongezeni!

Hatujachelewa sana-anzeni sasa.
 
Unaongelea taa za barabarani ili hali
Umeme wa nyumba shida
 
Taa za barabarani hazihitaji eneo liwe na Umeme au lah mana Technology ya PV yani Panel za solar ndio ina take over now, Mi nafikiri Hili swala ulilotoa mtoa mada Viongozi waliangalia tu, Zamani nguzo za Tanesco zilikuwa na Taa ila kwa sass hakuna tena
 
hawa harmashauri wamezoea kukusanya kodi ila kutumia kodi ni tatizo zamani si kulikuwa na taa za barabarani mitaa hata mapipa ya taka waligawa bure
 
Kwa umeme gani ? Usidhani hmna waliolifikilia hilo, litawezkna kama likifanywa na prince au baba yake,hao wanaweza zima umeme hta wa mochwari ilimrd taa ziwake mitaani
 
Tatizo utunzaji hatuwezi. Barabara zote kubwa zinapojengwa hufungwa taa.
 
Hiyo miradi imeanzishwa katika miji mbalimbali.

Wanatumia solar power hawahitaji tena umeme wa tanesco.
 
Kwa nini taa za barabarani na mitaani ni muhimu kwetu
Kwanza kwa usalama wa raia na pia kwa waendesha vyombo vya moto.
Pia ni mwanga wa artificial ukiongeza mda zaidi kuwa kama jua ili watu wafanye shughuli zao kama biashara.

Serikali ingewapa makampuni kuifanya hii kazi ya kusimamia na kutengeneza au kukarabati pindi zinapoharibika.
Au waweke umeme wa solar au gas lightning maana umeme umekuwa shida kwetu ingawa solar ni rahisi pia
 
Kweli kabisa!
 
Hivi hata ktk hili hadi mh Rais alitolee kauli?!

Nchi yetu inazo nyenzo zote za kuweza kufunga taa za usiku mijini hadi vijijini. Nguzo tunazalisha wenyewe hapa kwetu, kwanini wataalamu wetu msilisimamie hilo?

Nchi ndogo kama Rwanda 99% ya miji na vijijini vyao wakati wa usiku hupendezeshwa sana na taa za mtaani.Kwa nini sisi tumeshindwa!

Kwa mfano, miradi yote ya barabara mkandarasi angewekewa kipengere cha kuweka na taa kila kijiji na miji na gharama zikajumlishwa katika malipo ya mradi husika.

Jamani jambo dogo kama hilo si lazima libuniwe na Rais Magufuli. Mengine ninyi wasaidizi wake jiongezeni!

Hatujachelewa sana-anzeni sasa.
Anza kuweka mishumaa kwenye barabara za mtaani/ubalozi wako.
 
Back
Top Bottom