“Ni upuuzi tu!” Wanamtandao wa Afrika wakasirika baada ya Taasisi ya Marekani kuja kupaka matope tena

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,036
Wiki iliyopita, Wizara ya Mambo ya Nje ya China ilitangaza kuiwekea vikwazo Taasisi ya Hudson ya Marekani inayounga mkono vitendo vya kuitenganisha Taiwan na China. Kwa muda mrefu, taasisi hiyo ya washauri bingwa ya Marekani imekuwa ikiishambulia China, na watafiti wake wametoa tafiti na ripoti nyingine zinazoikashifu China, na kutetea kwamba Marekani inapaswa kuikandamiza China katika nyanja zote.

1681193716380.png


Katika uhusiano kati ya China na Afrika, msimamo wa taasisi ya Hudson pia ni mbaya sana. Kwa mfano, mwezi Februari mwaka huu, taasisi hiyo ilichapisha makala yenye kichwa cha "Urithi wa 'Kuchukiza' wa Misaada ya Maendeleo ya China kwa Afrika", ikirudia tena uwongo kwamba mikopo ya China imezipelekea nchi za Afrika kuingia kwenye "mtego wa madeni". Hivi majuzi tu, mtafiti mwandamizi wa masuala ya Afrika katika Taasisi ya Hudson Joshua Meservey, alidai kwenye mtandao wake wa Twitter kuwa ""Bandari ya Lamu Kenya, iliyojengwa na kampuni ya China, inabeba shehena ndogo kuliko ilivyotarajiwa. Reli ya SGR, mradi mwingine mkubwa na wa gharama kubwa wa miundombinu pia inaendeshwa chini ya uwezo wake. Mapato ya awali kupitia uwekezaji wa miundombinu hiyo si mazuri." Mara tu baada ya tweet hii kutolewa, ilikosolewa vikali na wanamtandao wengi wa Afrika.

1681193737737.png

1681193744320.png


1681193751301.png



"Ni upuuzi tu. Mbona huwezi kuwa na mtamazo sahihi na kuacha kueneza propaganda za uongo kuhusu China?"

"China imesaidia Kenya kujenga bandari, reli, viwanja vya michezo na barabara kuu... Lakini vipi kuhusu Marekani? Ni kuchapisha pesa na kusafirisha nje mfumuko wa bei au kutoa vikwazo vya kiuchumi barani Afrika?"

"Ni mmarekani mwengine mwenye uchungu kuona nchi ya Afrika inakua kwa msaada wa nchi yenye nguvu ya Mashariki."

"China ni johari...jambo pekee ambalo Marekani inaweza kufanya kusaidia nchi za Afrika ni kuwafunza waasi wenye silaha ili wapigane na serikali zao, na kuinyonya Afrika kupitia dola ya kimarekani. Wakati umefika kwa Afrika kubadilisha njia."

......

1681193760364.png


Ili kuitetea Marekani, Joshua Meservey awali alibishana na wanamtandao hao kwenye sehemu ya maoni. Alisema, "Ni kweli Marekani imewekeza kidogo katika miundombinu barani Afrika, lakini imefanya vizuri katika afya ya umma. Makumi ya mamilioni ya Waafrika wako hai leo, kwa sababu ya mipango ya afya ya umma ya Marekani." Lakini watu hawawezi kusahau kuwa wakati Afrika ilikuwa katika kipindi kigumu cha kupambana na janga la COVID-19, Marekani ilihodhi chanjo nyingi hadi zikaisha muda wake, ndio ikasisitiza kuzipatia nchi za Afrika. Joshua alitoweka katika sehemu ya maoni baada ya kugundua kuwa matamshi yake yaliibua kejeli na kukosolewa zaidi na wanamtandao.

1681193775984.png


Hali halisi ni kuwa Bandari ya Lamu au Reli ya SGR zilizotajwa na Joshua, yote ni mafanikio muhimu ya ujenzi wa pamoja wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja" kati ya China na Kenya, na pia ni miradi mikuu ya Ruwaza ya Kenya 2030. Kwa mujibu wa ripoti mpya iliyotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu ya Kenya, mwaka jana mapato ya mwaka ya Reli ya SGR yalizidi shilingi za Kenya bilioni 15, ambapo kiasi cha abiria na mizigo kiliongezeka hadi watu milioni 2.4 na tani milioni 6 mtawalia. Wakati huo huo, miji ambayo reli ya SGR inapita pia imepata maendeleo, haswa katika sekta ya hoteli, hayo yote ni matunda ya mradi huo. Kama njia mpya ya nchi kavu za Afrika Mashariki kusafirisha bidhaa zao nje, mradi wa Bandari ya Lamu pia umesifiwa sana na serikali ya Kenya. Mradi huo sio tu umesukuma maendeleo ya eneo la Lamu na hata Kenya nzima, bali pia umekuwa miundombinu muhimu ya kukuza mafungamano ya kiuchumi barani Afrika. Na kwa kuwa wengi wa wajenzi wa bandari hiyo walikuwa wazawa, mradi huo pia umefunza watu wengi wenye ujuzi wa kifundi.

1681193785465.png


Kwa macho ya baadhi ya wanasiasa na wasomi wa Marekani, nchi na watu wa Afrika hawana maamuzi yao wenyewe. Lakini chini ya tweet hii inayotolewa na taasisi ya kitaaluma kama chombo cha kuchezea maoni ya umma kwa ajili ya maslahi ya serikali ya Marekani, wanamtandao wa Afrika walitoa mafunzo kwa makini—— Nani anazisaidia nchi za Afrika kutafuta maendeleo, na ni nani anafanya kila awezalo kuihusisha Afrika katika vita ya siasa za kijiografia, watu wa Afrika wenye busara wametambua vya kutosha. Kama alivyosema mwanamtandao huyu anayejiita Yahoh, "Hebu nione miundombinu iliyojengwa na Marekani iko wapi! Lo, nilisahau, hutafanya chochote cha maana isipokuwa kukuza maadili yako yaliyovunjika kwetu Afrika!"
 

Attachments

  • 1681193669066.png
    1681193669066.png
    49.8 KB · Views: 2
Back
Top Bottom