Ni umri gani unaofaa kuoa au kuolewa?

Ni umri gani unaofaa kuoa au kuolewa?

...sidhani kama kigezo cha kupishana umri ni sahihi, ingekuwa busara kutanguliza MAPENZI kwanza, badala ya UMRI. ...Mara nyingi, inferior na superior complex ndizo zinazoletesha majibizano ndani ya nyumba, jitahidini sana kuepuka kigezo cha umri. Mfano; hata mkioana umri sawa, huenda pia mtakuwa na kasoro za miezi, mfano bibie kazaliwa January nawe umezaliwa December, bado itakuwa tatizo?... la msingi ni Heshima, maelewano na kustahmiliana.

...hakuna ratio yeyote iliyo favourable ndugu yangu, wala vitabu vya dini havisemi hivyo. la msingi ni mwanaume muadilifu amuoe mwanamke muadilifu like wise!

...Japhet, ukipiga hesabu za haraka haraka, tuseme umebahatika kuoa mwaka huu 2009, na mwenyezi mungu amewajaalia uzazi mwaka 2010, ndio kusema wakati mwanao wa kwanza anaanza darasa la kwanza, wewe utakuwa na umri wa miaka 50yrs,(yr 2017)

....akimaliza STD 7 (yr 2023) wewe tayari utakuwa unakimbilia 56yrs na presha za kukimbizana na school fees za Form 1

.... kijana huyo akiwa na 18yrs (yr 2028) wakati huo anafukuzana na mafao ya kuingia Chuo kikuu wewe tayari utakuwa ushagonga 61yrs!

sasa jifikirie kama kijana huyo atakuwa na wadogo zake wawili wanaomfuatia, si ndio itakuwa kumtupia mzigo huyo kijana awasomeshe ndugu zake? Unless ukwapue fungu la EPA kama nalo litakuwepo (joke) ...otherwise ndio ule msemo wa "fainali uzeeni" unapokuja kuwa kweli.

Usikurupuke, endelea kuangalia taratibu, jaribu kupunguza vigezo vya 'mchumba' unayemtafuta, kwani hakuna binaadamu mkamilifu, ila nyie wawili (mke na mume) mkitaka, mwaweza kuifanya ndoa yenu iwe kamilifu.

Hapa ndio tunaona umuhimu wa umri katika hatua hii muhimu ya maisha.
 
Umri wa kuoa/kuolewa unategemea na mtu mwenyewe. kuna mtu anaweza kuamua kuoa akiwa na miaka 20 mwingine miaka 30 nk. Lakini swala la msingi ni kuhakikisha kuwa ataweza kukabiliana na maisha ya familia. kama mwanaume jitahidi kuhakikisha kuwa unaweza kujitunza yeye mwenyewe pamoja na familia yake.

Lakini kwa wanawake ambaye anahitaji kupata mtoto ndani ya ndoa, itabidi ajitahidi aolewe kabla ya miaka 30. kwa sababu ya mambo ya menstruation cycle na kwa wanawake walio wengi huwa inapotea kuanzia miaka 35.
 
acha kuwatisha kina dada wewe!
hakuna menopause inayoanzia miaka 35 in a normal woman ovarian cycle unless kuwe na other disease conditions ambazo zinaweza kuziharibu ovaries na kuzifanya zisitengeneze mayai.menopause at least should start at 45yrs.wengi tu inakuwa zaidi ya hapo.
 
Nimekuwa najiuliza kuwa ni umri gani mwanaume inamlazimu kuoa au mwanamke
inabidi kuolewa? Literally najua hamna miaka maalum; lakini kuna wakati watu wanaokuzunguka wanaanza kukunyooshea vidole kuwa mbona haowi au mbona haolewi? Na majina mengine mengine wataanza kukuita? Kama hujaoa au kuolewa
till 40's can it cause any kind of frustrations?
Inategemeana na wataka kuoa au kuolewa kwa sababu gani; peer pressure, relatives, parents au? au wataka kuzaa? au ume-fall in love. kwa hiyo kila sababu itakuwa na "appropriate" age.
 
Menopause usually occurs between the ages of 40 and 55. The occurrence of menopause is different for each woman. It can occur before 40 (it's defined as "easly menopause") and can be after 55.... sometimes even after 60..... In certain case it stops sudenly but in many cases menstrual activity tapers off until it completely stops. It may take up to 3 years for the menstrual cycle to completely stop. Menopause is a natural event. The age of when menopause occurs is affected by several factors: 1). Nutrition - Malnourished women begin menopause about 4 years earlier than well-nourished women. 2). Early onset of menstruation - Women who begin menstruation at an early age are more likely to begin menopause later.

sasa basi kinachotakiwa kuelewe hapa ni kuwa mara nyingi watoto wanaozaliwa baada ya mwanamke kufikisha miaka 35 wana nafasi kubwa sana ya kuwa abnormal (i.e kuwa na afya amboyo si nyema yani wadhaifu au hata kuwa na matatizo ya kiakili). So ni vizuri mwanamke akaolewa mapema na kupata watoto mapema/kabla ya kuwa na umri mkubwa sana.
 
Sifikiri kama kuna umri maalum wa kuoa au kuolewa labda nidokeze kuwa ni vyema mtu akaamua kuoa au kuolewa pindi atakapo kuwa juu wa umri wa miaka 18 na sio chini ya hapo.
 
Umri mzuri wa kuoa mi nafikiri ni kutegemeana na malengo yako mwenyewe. Kama ni kwa minajili ya kupata mtoto, basi ni vizuri kuoa mapema kadri iwezekanavyo ili uzae watoto wazuri wenye ngozi nyororo, usije kuchelewa ukazaa watoto wenye sura za kizee!!

Pili kwa sie tulieruhusiwa kuoa wake wengi, unaweza kuwa ushamaliza biashara ya kuzaa hivyo hata ukiwa na miaka 59 unaweza kuoa upate kitu kipya uendelee kuburudika na maisha.

Na pia kwa sisi wakongwe ambao wenzi wetu wametutoka au tumekorofisha beyond repair kama mzee Mandela, then hata ukiwa na miaka 80 unaweza kuoa.

Kwa hivyo suala la muda muafaka wa kuoa ni kutegemea na malengo na hali halisi uliyonayo katika kipindi husika!!
 
...😀 naaam naaaam!
 
Menopause usually occurs between the ages of 40 and 55. The occurrence of menopause is different for each woman. It can occur before 40 (it's defined as "easly menopause") and can be after 55.... sometimes even after 60..... In certain case it stops sudenly but in many cases menstrual activity tapers off until it completely stops. It may take up to 3 years for the menstrual cycle to completely stop. Menopause is a natural event. The age of when menopause occurs is affected by several factors: 1). Nutrition - Malnourished women begin menopause about 4 years earlier than well-nourished women. 2). Early onset of menstruation - Women who begin menstruation at an early age are more likely to begin menopause later.

sasa basi kinachotakiwa kuelewe hapa ni kuwa mara nyingi watoto wanaozaliwa baada ya mwanamke kufikisha miaka 35 wana nafasi kubwa sana ya kuwa abnormal (i.e kuwa na afya amboyo si nyema yani wadhaifu au hata kuwa na matatizo ya kiakili). So ni vizuri mwanamke akaolewa mapema na kupata watoto mapema/kabla ya kuwa na umri mkubwa sana.

uliandika menstrual cycle kwa wanawake wengi inaacha at 35?note hizo bolded letters.unasema wanawake wengi?kitaalam wanawake wengi inaanza baada ya 45 na kuendelea rarely before that kama hakuna matatizo mengine.mtoto anaweza kuzaliwa na kasoro katika umri wowote ule wa mama yake na mara nyingi wamama wanaozaa katika umri mdogo ndiyo wako katika risk kubwa.miaka 35 ni umri mzuri tu wa mama kuzaa na mtoto akakamilika vizuri tu kama mama ana afya nzuri.
 
Suala la kuoa linazingatia mambo manne KULA,KULALA,HUDUMA,KUZAA.
Unapoingia katika ndoa je mtaweza kula?Kipato chako chatosheleza familia?
Kulala,je malazi yapo yakukidhi familia?
Huduma je waweza kidhi huduma nyingine muhimu za kifamilia kama elimu,afya,etc?
Kuzaa je unaouwezo wa kuzaa?Nikimaanisha ushafikisha umri wa kuzaa(i.e 18yrs)
Hii yote ni iende sambamba kwa mke na mume
 
Je ni umri gani sahihi wa kuoa na je unatakiwa uwe umejipanga vipi au uwe na maisha gani ndio uoe?

Tujaribu kujadili ili jambo
 
Je ni umri gani sahihi wa kuoa na je unatakiwa uwe umejipanga vipi au uwe na maisha gani ndio uoe?

Tujaribu kujadili ili jambo
Umri sahihi unategemeana na jamii uliyopo,wengine huoa mapema kutokana na namna wanavyoishi,kwa mfano jamii ya wafugaji na wakulima huko vijijini huoa mapema kutokana na kuwa na kila kitu wanachoona kinawafaa katika maisha yao.
Kwa sisi watu wa mjini ni vigumu sana kuharakia kuoa kutokana na kutokukamilisha yale ambayo tumekuwa tumepanga kimaisha maana maisha ya mjini si ya kuharakia kuoa.
Kwa hiyo umri sahihi wa kuoa unategemea na namna hali ya sehemu uliyopo na maisha uishiyo na si suala la miaka kadhaa.
 
hakuna umri sahihi wa kuoa/kuolewa, oa/olewa ukijihc/ kuona mtu ulienae anakufaa maishani.
 
hakuna umri sahihi wa kuoa/kuolewa, oa/olewa ukijihc/ kuona mtu ulienae anakufaa maishani.
kuna post ya Kimbweka yuko 34 yrs lakini bado hajafikiria kuoa na imekuwa dhana ya wanaume wengi kuwa kuoa ni mpka uwe na kila kitu sasa je ni sahihi maana kuna rafiki yangu yuko 38 lakini anadai bado anajipanga na yuko safi ana gari mbili sasa sijui ni selfishness ya nafsi au ni nini?

Hapa naongelea sisi tulio mijini na wenye elimu na kazi au shughuli zinazoingiza kipato
 
me nilioa nikikwa na miaka 20 lakini sijaona challenges yyote
 
KUOA...SIO SUALA LA UMRI..ni suala la "UHITAJI WA MWENZA/MSAIDIZI WA MAISHA YAKO" .... KWA KUWA KILA MMOJA WETU ANAO WAKATI WAKE WA UHITAJI WA KUWA NA MWENZAKE WA MAISHA.....ILA KWA MTAZAMO WANGU...KAMA WATANZANIA TUNA LIFE SPAN YA 50YRS SO NI BUSARA UKIOA AT EARLY 30'S ILI UWEZE HATA KU-RAIS UR FAMILY ... ILI HATA MUNGU AKIKUPENDELEA KIDOGO UWEZE HATA KUONA WATOTO WA WATOTO WAKO...aka .. WAJUKUU
 
Back
Top Bottom