Ni umri gani unaofaa kuoa au kuolewa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni umri gani unaofaa kuoa au kuolewa?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Aluta, Feb 27, 2009.

 1. A

  Aluta Member

  #1
  Feb 27, 2009
  Joined: Aug 16, 2008
  Messages: 70
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Nimekuwa najiuliza kuwa ni umri gani mwanaume inamlazimu kuoa au mwanamke inabidi kuolewa? Literally najua hamna miaka maalum.

  Lakini kuna wakati watu wanaokuzunguka wanaanza kukunyooshea vidole kuwa mbona haowi au mbona haolewi? Na majina mengine mengine wataanza kukuita.

  Kama hujaoa au kuolewa tll 40's can it cause any kind of frustrations.
   
 2. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #2
  Feb 27, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,644
  Likes Received: 1,470
  Trophy Points: 280
  Kama ulivosema, hakuna umri maalum kama umeshakuwa mtu 'mzima' kwa mujibu wa sheria za nchi na jamii...so ukimpata umpendaye, twende kazi, lakini kama hujampata utamwoa nani? Muhimu be yourself and know what you are looking for in life
   
 3. Y

  Yassin JF-Expert Member

  #3
  Feb 27, 2009
  Joined: Jul 23, 2008
  Messages: 326
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mkuu nadhani hapo ni sawa lakini ukishafikia miaka kuanzia 30 angalia wangapi wanapata wanaowa??Na siwezi kumuowa mwanamke aliyekuwa over 30 sasa wa nini na atakusaidia nini??inabidi uowe ukiwa under 30 sio zaidi ya hapo maana kama zaidi ya hapo itakuwa vichekesho tu.....Utaambiwa bado upo upo!!
   
 4. Himawari

  Himawari JF-Expert Member

  #4
  Feb 27, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 2,183
  Likes Received: 665
  Trophy Points: 280
  Mapenzi hayachagui UMRI mkuu ingawa kuna umri ambao kisheria mwanamke anaweza kolewa au mwanaume anaweza kuoa.
   
 5. Y

  Yassin JF-Expert Member

  #5
  Feb 27, 2009
  Joined: Jul 23, 2008
  Messages: 326
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0

  Sawa sawa mkuu nimekupata hamna shaka wala nini......ila inategemea sana hapo mkuu maana inabidi kucheck huwezi kuwa na 30 ukaenda kumparamia mtu mwenye 60 inawezekana hapo??
   
 6. p

  p53 JF-Expert Member

  #6
  Feb 27, 2009
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 613
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  kuoa/kuolewa hakuna formula inategemeana na mtiririko wako wa maisha na malengo yako.lakini all in alll kina dada inapendeza wakiolewa below 30yrs.
   
 7. A

  Aluta Member

  #7
  Feb 27, 2009
  Joined: Aug 16, 2008
  Messages: 70
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Nimekuwa nikisikia watu mbalimbali wakisema mwanamke inabidi awe kaolewa before 25 yrs na wanaume wengi baadhi marafiki zangu nimewasikia wakisema '' Nataka kumuoa demu wangu...umri unaenda naelekea miaka 30 sasa''.Nimesikia hii sentensi mara nyingi sana!
   
 8. Binti Maringo

  Binti Maringo JF-Expert Member

  #8
  Feb 27, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 2,805
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Hakuna formula ya kuoa..besides age aint nothing but a number....hiyo miaka ni number tuu...what matter ni jinsi unavyoelewana na huyo mwenza wako lakini syo kwa sababu unaona kuwa unapiga milage basi ukimbilie kuoa matokeo yake a lot pf people wanaoa then after a year wanaaanza kufikiria kudivorce kwa sababu hakuna mutla feelings ni kwamba tuu mtu ameamua kuoa ili mradi...

  ushauri wangu ni kwamba usikimbilie kuoa au mwanamke usikimbilie kuolewa just because ukidhani umri wako unakimbia....utakuja kujuta down the road...think wise before making your decision..je is she the one?!...na ndoa ni mipango ya mungu!.
   
 9. N

  Ngereja JF-Expert Member

  #9
  Feb 27, 2009
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 796
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Pamoja na kwamba ukishakuwa mtu mzima, yaani umeshafikisha umri wa miaka 18 na kuendelea unakuwa na maamuzi yako na uaweza kuamua lini uoe au uolewe; inapendekezwa na ingefaa sana uoe au uolewe katika umri ufuatao:

  1. Kwa mwanamke inafaa uolewe ukiwa umefikisha umri wa miaka 23 hadi 30 na isizidi 35. Ikiwa umempata mchumba ukiwa na umri kati ya miaka 22-30 na huna kipingamizi cha kwa nini usiolewe, then ni bora zaidi. Hata hivyo, kama umefikisha miaka 30 au hata 35 ndo ukampata mchumba hakuna ubaya, japokuwa unatakiwa kupangilia vyema masuala ya uzazi. Hata hivyo, uamuzi wa mwisho wa kuolewa au usiolewe unao wewe mwenyewe.

  2. Kwa wanaume umri wa miaka 25 hadi 35 ni muafaka kuoa kama huna kipingamizi na majukumu mengine kama ya shule. Kwa mazingira ya Tanzania miaka 25 au hata 30 bado wanaume wengi wanakuwa wanasoma vyuo vikuu au vyuoni, na hasa kama mtu alichelewa au alikuwa anaahangaika na elimu kwa muda mrefu. Sasa hii haimaanishi kwamba kama umezidi 35 usioe, la hasa. Kuoa mapema katika umri wa miaka kati ya 25-30 ni bora zaidi.

  NB: Suala la kuoa kwa mwanaume linategea mambo mengi kabla mtu hajaamua kuoa, miongoni mwa hayo mambo ni je, uko tayari kuwa na familia, kuitunza na kuihudumia ipasavyo na kubeba majukumu ya ndoa? hapa, suala la uchumi ni muhimu sana kwa mwananume. Hapa ina maana ni lazima uwe tayari umejiweka katika nafasi ya kuwa na kipato kuhudumia familia. Uwe na kazi (Ya kuajiriwa au kujiajiri), biashara, kilimo, ufugaji, n.k.

  Sasa baadhi ya wanaume huchelewa kuoa kwa sababu ya kutokuwa na uhakika wa namna ya kuendesha maisha ya kila siku (Kipato). Na wengine huchelewa kuoa si kwa sababu hawana kipato, lakini sababu nyingine za kifamilia n.k.

  Suala la kuoa au kuolewa halitegemei sana umri, japo umri ni suala la kuzingatiwa. Kuna mambo mengi ya kuzingatia badala tu ya kuangalia umri maana kuoa na kuolewa ni kujenga familia na kutokufikiria kwamba unaolewa au kuoa ili baadaye muachane.

  Tuendelee na mjadala.....
   
 10. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #10
  Feb 27, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,867
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  Ukiona mda unakwenda na wewe ni dem na unataka kuolewa na hajaja mtu..je ntafanyaje?
   
 11. J

  Japhet Member

  #11
  Feb 28, 2009
  Joined: Jan 26, 2009
  Messages: 43
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Natoa shukrani zangu za dhati kwa mtoa mada hii na wachangiaji.

  Sasa na mimi nimepata ujasiri wa kutoa dukuduku langu. EE bw. wana JF mimi agea inakimbia kidogo...hivi sasa nakimbilia kwenye kiloba cha 42 cha chumvi (yaani miaka 42). Lakini kusema ukweli sijampata mchumba inagawaje nimeishajiweka sawa kuoa. Mnanishaurije ndugu zangu??? Nikurupuke nibebe wife yeyote juu kwa juu nioe kwa vile age inaenda fasta??? au niendelee kutafuta taratibu??? nomba msaada wenu tafadhali.
   
 12. Mhafidhina

  Mhafidhina JF-Expert Member

  #12
  Feb 28, 2009
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 548
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  mimi swali langu ni je, ni sahihi kuaoana mkiwa na umri unaofanana, kwa mfano mume kuwa na miaka 30 na mke kuwa na miaka 30?

  Au kuna ratio ya umri wa kuoana kati ya mwanaume na mwanamke? na je ipi ni ratio ilio favourable?
   
 13. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #13
  Feb 28, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  Mkuu maswala ya kutafuta taratibu utatafuta mpaka 60yrs........wewe tafuta yoyote mzuri zaa nae kwanza angalia kama anafaa kuwekwa ndani chukua jumla lkn kama ndio wale wale lea mtoto..

  ......siku hizi watu hawaoi wanaishi kinyumba tu....kuoa walioa wakina Nyerere etal.....na wanawake wa siku hizi wakishaolewa wanaota mapembe anajua kamaliza kazi.....wengi goal yao ni kuolewa wakishaolewa wanajisahau na kuwa na sauti.......
   
 14. A

  Aluta Member

  #14
  Feb 28, 2009
  Joined: Aug 16, 2008
  Messages: 70
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13

  Kwa maoni yangu mkiwa na umri sawa shwari tu, na kama mwanamke kakuzidi umri basi isiwe zaidi ya mitano although I don't expect that. Ila ratio nzuri nadhani mwanaume uwe at least miaka mitano zaidi ya mwanamke!
   
 15. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #15
  Feb 28, 2009
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0

  mie ckushauri kbsa ukurupuke, tena kama ni ndoa ya kikristu ndio kabisaaa zinabana sana!
   
 16. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #16
  Feb 28, 2009
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 235
  Trophy Points: 160
  Kuoa ama kuolewa ni suala ambalo nadhani huja bila hiari ya wawili.

  Binadamu hupenda, huamini anachopenda ndicho sahihi! Akipenda hata aambiwe nini huamini anaonewa donge na wenzake hawamtakii mema.

  Unapofikia wasaa wa kumvalisha au kuvalishwa pete (na) mwenzako si rahisi kueleza... Ni ngumu kiasi chake, inatokea tu (endapo ni mapenzi yalotoka moyoni).

  Kuna wanaofanya maandalizi makubwa sana wakati wa mapenzi na kuamua kuitana wachumba, hawa (hasa wanaume) hujikuta wanakuwa na girl friends wengi waliowahi kuwaita wachumba na pengine hata kuwavisha pete za uchumba.

  Pete za uchumba husababisha wanawake wengi kuongopa! Hu-act kuwa wema na hubadilika sana na hata kuonekana ndio wanaofaa kuwa wake.

  Tatizo la maisha ya namna hii ni hili: Mwanamke anakuwa kweli kapenda na kajua bwana huyu kweli ananipenda na mimi ndiye chaguo lake katika maisha! Kumbe sio, wanaume wengine wanajua udhaifu wa mwanamke na kuamua kuutumia kwa njia hii... Mbaya sana.

  Sishauri: Uvalishe mwanamke pete ya uchumba (umfunge) na umweke benchi la ufundi kwa zaidi ya mwaka huku ukiwa huna hata dalili za kumwoa!

  Sishauri: Umlazimishe mwanaume akuvalishe pete eti ndo uamini anakupenda kwani atafanya hivyo ili aweze kuendelea kukidhi haja zake kwako na kwa wenzako lukuki!

  Nashauri: Jiweke karibu na wanawake na wape heshima yao (endapo huna hata girl friend) huku ukijidhihirisha ulivyo (do not fake) ili unapowajua na kugundua mmoja wao anafaa kuwa mwenzi wako wa maisha basi umweleze ukweli (hakikisha unafahamu background yake na hakikisha kuwa ha-fake mwonekano wake). Uchumba ukidumu walau kwa miezi 9 hadi mwaka mmoja ni muda unaotosha kuwa umemtambua mwenzi wako na kujua udhaifu wake na ubora wake na namna unavyoweza kuvumiliana naye katika maisha.

  Nashauri: Jiepushe na ku-fake mwonekano wako wa kweli kwa wanaume, wakidanganyika na faking yako na wakaamua kukuoa maisha yatakuwa ya shida sana hata kama mtapata raha kwa miaka ya mwanzo wa maisha.

  Nashauri: Hakuna aliyezaliwa anajua kupenda, wote tumeyakuta na ukweli tutayaacha. Unaweza ukawa unam-feel mwenzako kwa kiwango kikubwa na hakuna njia nyingine ambayo unadhani inaweza kumfanya aelewe unamhitaji kama mwenza... Mweleze ukweli! Mpe heshima yake wakati wa kufanya hivyo, hii inaweza kufanywa na pande zote mbili, mwanamke kumweleza mwanaume (kitu ambacho wengi hukiogopa) na mwanaume kumweleza mwanamke (mfumo dume ulozoeleka). Kumbuka, kama umekwisha mfahamu kwa undani mwenzio ni rahisi kuweza kujua namna ya kumweleza ukweli halisia.

  Angalia: Kuna tofauti kubwa kati ya mapenzi ya hisia na mapenzi ya kuishi pamoja kama mme na mke. Kumpenda mtu kwa ajili ya sura kusikudanganye kuwa ndiye anafaa kuwa mke ama mme kwako. Kuna kitu ndani yake kitakachokuita, na ukiitwa tafadhali itika!

  Kwa leo naishia hapa... Sijasoma maoni ya wengine na nahisi nimekurupuka lakini huenda ikasaidia kidooooooogo!
   
 17. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #17
  Feb 28, 2009
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 235
  Trophy Points: 160
  Usisikilize maoni kama ya Nyamayao (japo yanaweza kuwa na ukweli flani).

  Ukweli ni kuwa hakuna kitu kizuri kama kuwa kwenye ndoa. Ndoa ni tamu sana... Siwezi hata kueleza.

  Tena, ndoa inakuwa tamu zaidi endapo inakuwa ni ya mme mmoja na mke mmoja!

  Hakuna kinachobana, ni wanandoa kutotekeleza wajibu wao katika ndoa.

  Fuatilia makala nitakayoandika hapa next week kuhusiana na ndoa na hakika naamini utaelewa kwanini nakwambia ndoa ni tamu.

  Ipo tiba kwa ndoa zinazolegalega, itakuwa kwenye makala hiyo, na wakati huo nitakuruhusu kuniuliza maswali tani yako.

  Sijaoa/sijaolewa wala sio/siolewi... Mimi robot tu!
   
 18. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #18
  Feb 28, 2009
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0

  Invcble hapo mie kwa upande wangu naona sio vzr kwa m2 kukurupuka coz kukurupukia m2 humjui vzr ni wa namna gani then akurupukie tu amuoe? kwa mawazo yangu ajitahidi kidogo akutane na wa kufahamiana kwa muda kidogo sio wa kukurupukia....au cjaelewa neno kukurupuka?na cjasema ndoa co tamu nipo kwenye ndoa pia na najua utamu/uchungu wake.
   
 19. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #19
  Feb 28, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160

  ...oa ukiwa katika umri utaoweza kumtunza mke, kulea na kuwasomesha wanao, ili hata utapofikia umri wa kustaafu, wanao wawe kwenye umri wa kuoa ili nawe upate muda wa kucheza na wajukuu zako...

  ...haipendezi ushakuwa kibabu, unahaha kuchangia pensheni ya kuwasomeshea wanao, ambao machoni mwa watu wanaonekana vijukuu vyako.
   
 20. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #20
  Feb 28, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...sidhani kama kigezo cha kupishana umri ni sahihi, ingekuwa busara kutanguliza MAPENZI kwanza, badala ya UMRI. ...Mara nyingi, inferior na superior complex ndizo zinazoletesha majibizano ndani ya nyumba, jitahidini sana kuepuka kigezo cha umri. Mfano; hata mkioana umri sawa, huenda pia mtakuwa na kasoro za miezi, mfano bibie kazaliwa January nawe umezaliwa December, bado itakuwa tatizo?... la msingi ni Heshima, maelewano na kustahmiliana.

  ...hakuna ratio yeyote iliyo favourable ndugu yangu, wala vitabu vya dini havisemi hivyo. la msingi ni mwanaume muadilifu amuoe mwanamke muadilifu like wise!

  ...Japhet, ukipiga hesabu za haraka haraka, tuseme umebahatika kuoa mwaka huu 2009, na mwenyezi mungu amewajaalia uzazi mwaka 2010, ndio kusema wakati mwanao wa kwanza anaanza darasa la kwanza, wewe utakuwa na umri wa miaka 50yrs,(yr 2017)

  ....akimaliza STD 7 (yr 2023) wewe tayari utakuwa unakimbilia 56yrs na presha za kukimbizana na school fees za Form 1

  .... kijana huyo akiwa na 18yrs (yr 2028) wakati huo anafukuzana na mafao ya kuingia Chuo kikuu wewe tayari utakuwa ushagonga 61yrs!

  sasa jifikirie kama kijana huyo atakuwa na wadogo zake wawili wanaomfuatia, si ndio itakuwa kumtupia mzigo huyo kijana awasomeshe ndugu zake? Unless ukwapue fungu la EPA kama nalo litakuwepo (joke) ...otherwise ndio ule msemo wa "fainali uzeeni" unapokuja kuwa kweli.

  Usikurupuke, endelea kuangalia taratibu, jaribu kupunguza vigezo vya 'mchumba' unayemtafuta, kwani hakuna binaadamu mkamilifu, ila nyie wawili (mke na mume) mkitaka, mwaweza kuifanya ndoa yenu iwe kamilifu.
   
Loading...