kama umempenda huwezi kuanglia umri
wapo wengi sana, bali nyie ndio mnakosea kuchagua, mnawataka wa matawi ya juu, mkutane cjui Carnivore, umkute nae ana kila kitu kama wewe, awe mtoto wa mjini mwenye kujua mambo ya kimjini,hao lazima wawe kimaslahi na sio kimapenzi... mabinti descent wamejaa kibao ni uchaguzi wenu mbovu.
Mimi mwenyewe nataka kuwasaplaiz watu,nikiamua kuoa nataka kuoa demu mmoja wakawaida sana mshamba mshamba...natafuta sana mwalimu nasikia walimu ndio wake haswa, sema bana walimu hawaonekani mtaani sijui wanajifungiaga wapi au wanaoana wenyewe kwa wenyewe...ila wanafaa sana nikikumbuka walimu wangu wa primary na vikapu vyao vya bagia hawana makuu.