Nimekuwa najiuliza kuwa ni umri gani mwanaume inamlazimu kuoa au mwanamke
inabidi kuolewa? Literally najua hamna miaka maalum; lakini kuna wakati watu wanaokuzunguka wanaanza kukunyooshea vidole kuwa mbona haowi au mbona haolewi? Na majina mengine mengine wataanza kukuita? Kama hujaoa au kuolewa
till 40's can it cause any kind of frustrations?
Kuoa ama kuolewa ni suala ambalo nadhani huja bila hiari ya wawili.
Binadamu hupenda, huamini anachopenda ndicho sahihi! Akipenda hata aambiwe nini huamini anaonewa donge na wenzake hawamtakii mema.
Unapofikia wasaa wa kumvalisha au kuvalishwa pete (na) mwenzako si rahisi kueleza... Ni ngumu kiasi chake, inatokea tu (endapo ni mapenzi yalotoka moyoni).
Kuna wanaofanya maandalizi makubwa sana wakati wa mapenzi na kuamua kuitana wachumba, hawa (hasa wanaume) hujikuta wanakuwa na girl friends wengi waliowahi kuwaita wachumba na pengine hata kuwavisha pete za uchumba.
Pete za uchumba husababisha wanawake wengi kuongopa! Hu-act kuwa wema na hubadilika sana na hata kuonekana ndio wanaofaa kuwa wake.
Tatizo la maisha ya namna hii ni hili: Mwanamke anakuwa kweli kapenda na kajua bwana huyu kweli ananipenda na mimi ndiye chaguo lake katika maisha! Kumbe sio, wanaume wengine wanajua udhaifu wa mwanamke na kuamua kuutumia kwa njia hii... Mbaya sana.
Sishauri: Uvalishe mwanamke pete ya uchumba (umfunge) na umweke benchi la ufundi kwa zaidi ya mwaka huku ukiwa huna hata dalili za kumwoa!
Sishauri: Umlazimishe mwanaume akuvalishe pete eti ndo uamini anakupenda kwani atafanya hivyo ili aweze kuendelea kukidhi haja zake kwako na kwa wenzako lukuki!
Nashauri: Jiweke karibu na wanawake na wape heshima yao (endapo huna hata girl friend) huku ukijidhihirisha ulivyo (do not fake) ili unapowajua na kugundua mmoja wao anafaa kuwa mwenzi wako wa maisha basi umweleze ukweli (hakikisha unafahamu background yake na hakikisha kuwa ha-fake mwonekano wake). Uchumba ukidumu walau kwa miezi 9 hadi mwaka mmoja ni muda unaotosha kuwa umemtambua mwenzi wako na kujua udhaifu wake na ubora wake na namna unavyoweza kuvumiliana naye katika maisha.
Nashauri: Jiepushe na ku-fake mwonekano wako wa kweli kwa wanaume, wakidanganyika na faking yako na wakaamua kukuoa maisha yatakuwa ya shida sana hata kama mtapata raha kwa miaka ya mwanzo wa maisha.
Nashauri: Hakuna aliyezaliwa anajua kupenda, wote tumeyakuta na ukweli tutayaacha. Unaweza ukawa unam-feel mwenzako kwa kiwango kikubwa na hakuna njia nyingine ambayo unadhani inaweza kumfanya aelewe unamhitaji kama mwenza... Mweleze ukweli! Mpe heshima yake wakati wa kufanya hivyo, hii inaweza kufanywa na pande zote mbili, mwanamke kumweleza mwanaume (kitu ambacho wengi hukiogopa) na mwanaume kumweleza mwanamke (mfumo dume ulozoeleka). Kumbuka, kama umekwisha mfahamu kwa undani mwenzio ni rahisi kuweza kujua namna ya kumweleza ukweli halisia.
Angalia: Kuna tofauti kubwa kati ya mapenzi ya hisia na mapenzi ya kuishi pamoja kama mme na mke. Kumpenda mtu kwa ajili ya sura kusikudanganye kuwa ndiye anafaa kuwa mke ama mme kwako. Kuna kitu ndani yake kitakachokuita, na ukiitwa tafadhali itika!
Kwa leo naishia hapa... Sijasoma maoni ya wengine na nahisi nimekurupuka lakini huenda ikasaidia kidooooooogo!