...
As President of Tanzania it is my duty to safeguard the integrity of the United Republic. But if the mass of the people of Zanzibar should, without external manipulation, and for some reason of their own, decide that the Union was prejudicial to their existence, I could not advocate bombing them into submission. To do so would not be to defend the Union. The Union would have ceased to exist when the consent of its constituent members was withdrawn. I would certainly be one of those working hard to prevent secession, or to reduce its disintegrating effects. But I could not support a war on the people whom I have sworn to serve - especially not if the secession is preceded by a rejection of Zanzibaris by Tanganyikans.
Mkuu lakini unajua kwamba hakuna mtu wala kiongozi yeyote wa Zanzibar aliyetaka au anayetaka kuuvunja Muungano?Natamani mtu mmoja angekuwa na fikra kama hizo.
M
Mimi nawaomba sana viongozi wa Zanzibar kama kweli wanasimamia mawazo ya wananchi wake waombe kuuvunja Muiungano kisha yatakayofuatia baada ya hapo wagawane madaraka wanavyopenda. .
Kila kitu kina mwanzo wake, wakiondoka ndani ya Muungano wataunda seikali yao mpya wanavyopenda wao ili mradi wananchi wake wanaridhika. Lakini najua wazi yatafuata ya Comoro kwani hawa watu maswahiba wangu sana tu, ni wabishi sijapata kuona watatiana vidole vya macho wala haitachukua miaka mingi. Kisha Bara itapigiwa SOS..Hii inaitwa hekima; kwa sababu wakishatoka kwenye muungano wataanza kudai nini? watakuwa wamepata wanachotaka au watarudi kwenye status quo ya 1963 baada ya Mwingireza kuondoka, serikali kuwa chini ya kina Shamte (na Sultani kama figure head) nakabla ya mapinduzi? Kwa sababu haijawahi kuwepo serikali ambayo imefanya kazi ya "nchi ya zAnzibar" ukiondoa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Amandla.......Kwa sababu kero zote zinatokana na VIONGOZI WENYEWE.. Hivyo viongozi kwa kuelewa hivyo wanasingizia mipaka, nchi na kadhalika kiasi kwamba imeonekana Wazanzibar ndio Wajanja kumbe wanachokifanya ni kuongeza hesabu ya watawala wala kodi zao..Hivi kero za Muungano zinaonekana Zanzibar peke yake? Mbona hatuzungumzii kero wanazopata raia wa JMT ambao sio wenyeji wa Zanzibar? Mbona hatuzungumzii kero inazopata JMT kutokana na Muungano?
Wakiwa ndani ya MUUNGANO wanapiga kura kuunda serikali ya UMOJA wa KITAIFA. Nje ya Muungano mambo yatakuwa magumu zaidi. Kutakuwa na serikali ya SHIRIKISHO.Kila kitu kina mwanzo wake, wakiondoka ndani ya Muungano wataunda seikali yao mpya wanavyopenda wao ili mradi wananchi wake wanaridhika. Lakini najua wazi yatafuata ya Comoro kwani hawa watu maswahiba wangu sana tu, ni wabishi sijapata kuona watatiana vidole vya macho wala haitachukua miaka mingi. Kisha Bara itapigiwa SOS..
Ni makosa kudai kuwa kusema kuwa Zanzibar ni nchi bila kuweka wazi nchi ya pili ni ipi na maana ya hilo neno nchi. ......................... Kilichotakiwa kuwekwa wazi ni kuwa Zanzibar si nchi ndani ya JMT bali ni sehemu iliyopewa haki za pekee za kuwa na uongozi wake na utawala katika baadhi ya mambo. Wanachofanya wenzetu ni kujaribu kuweka neno sovereign kinyemela mbele ya state.
Mi nawapendeni kitu kimoja ndugu zangu wa Tanganyika (japo hampendi kuitwa hivyo lakini kwa kua mimi si mtumwa huwa sikatai asili yangu na kwetu Zanzibar) yaani nyinyi maneno meeeeengi vitendo hamna kitu...hebu iangalieni nchi yenu, Tanganyika, inanajisiwa, inaporwa, inaliwa na wajanja hawazidi sita kwa hisabu ya vidole, inatawaliwa na failed party kwa miongo karibu minne...bado humo mna wasomi wa viwango vikubwa, mabingwa wa kusema, wadadisi...wapiga soga kama walivyo humu JF n.k ...hakuna lolote lililokuwa system ipo pale pale na bado inauhakika wa kushinda kwa kishindo
Wazanzibar waungwana, weshalia sana na adha za CCM na muungano, weshasema sana...hakuna lililokuwa na wameamuwa vitendo sasa. Eeee...! ada ya mja hunena muungwana ni vitendo! ndivyo tutakavyoendelea kufanya kuanzia sasa.
Mi nawapendeni kitu kimoja ndugu zangu wa Tanganyika (japo hampendi kuitwa hivyo lakini mkataa asili huwa mtumwa) yaani nyinyi maneno meeeeengi vitendo hamna kitu.
Hebu iangalieni nchi yenu, Tanganyika, inanajisiwa, inaporwa, inaliwa na wajanja hawazidi sita kwa hisabu ya vidole, inatawaliwa na failed party kwa miongo karibu minne...bado humo mna wasomi wa viwango vikubwa, mabingwa wa kusema, wadadisi...wapiga soga kama walivyo humu JF n.k ...hakuna lolote lililokuwa system ipo pale pale na bado inauhakika wa kushinda kwa kishindo.
Hii ni aibu kuwa nchi zote za Afrika Mashariki zimejaribu kubadili system mpaka Kenya juzi tu wamepata katiba mpya, Watanganyika bado mmekaa tu mmefunga mikono, eti ni wapenda amani na utulivu (upumbavu na uzembe) wa kuleta mabadiliko.
Nawashangaza mnain'gan'gania Zanzibar wakati ni wazi kuwa hiyooo inaondoka pendeni msipende...badala ya ku'ngan'gania watawala wenu wabovu waondoke kwa kushindwa kupunguza, (si kuondosha), ujinga, maradhi na umasikini kwa miaka 40 sasa...mnatazama macho na kupiga soga tu, maneno tele, no actions.
Wazanzibar waungwana, weshalia sana na adha za CCM na muungano, weshasema sana...hakuna lililokuwa na wameamuwa vitendo sasa. Eeee...! ada ya mja hunena muungwana ni vitendo! ndivyo tutakavyoendelea kufanya kuanzia sasa.
Nimesikia Chikawe,juzi alimuamuru AG wa Zanzibar(tuna AG Zanzibar, Mbeya hakuna), aje Dar afafanuwe kilichotokea...jibu alilolipata...kamwachia naibu mwanasheria mkuu,Masaju ajitowe kimaso maso..."you can't boss us anymore...yale ni maamuzi BLW, kama yalivyokuwa siku hizo...what 's new there".
Hebu soma maelezo yeke kwenye vyombo vya habari Chikawe hajuwi anasema nini..mimi sijamuelewa hasa!kadhalika na DAG wake.
Ndugu zangu Watanganyika nakuombeni, acheni maneno, acheni bwabwaja..haziwasaidii...mtabaki mnaburutwa na CCM maisha yenu...fanyeni kama walivyofanya Wazanzibar, Wakenya...vitendo..japo kama hamuwezi kudai Tanganyika yenu basi daini...heshima yenu kwa kuwaondoa madhalimu (CCM) madarakani, nitawaona mumefanya la maana sana kuliko hizi bwabwaja za kila siku humu, shauri yenu...si tushangóa nanga!
Mwanakijiji umeshawahi kupitia web ya mzalendo.net?, kama bado hebu jaribu kuingia huko uone kinachoendelea. Wamekopi thread yako hii na inachambuliwa huko, eeh, hivi kumbe wenzetu wamefikia hatua hii!. Usoni tu ndugu rohoni wanaumia!
Mkuu,Mwana kijiji ndio nani ?jamaa anauka Uongo amekuwa na wafuwasi wake hapa analolisema hawakawii kutowa asante leo hii anajifanya profisa mchundo na kutafsi katiba ambayo haijuwi nini kimo ndani yake ,binafsi ningemuomba arudi tena na akufahamisheni jee alikosea katika kutowa tasmini zake au ndio miongoni mwaprofisa wa Jf hutafuta wale wasiokuwa na mbele wala nyuma na kuwahada kuwa wao wanaelewa ukweli wa Mungano ( unapoambiwa ujiambie )
Mwana kijiji ndio nani ?jamaa anauka Uongo amekuwa na wafuwasi wake hapa analolisema hawakawii kutowa asante leo hii anajifanya profisa mchundo na kutafsi katiba ambayo haijuwi nini kimo ndani yake ,binafsi ningemuomba arudi tena na akufahamisheni jee alikosea katika kutowa tasmini zake au ndio miongoni mwaprofisa wa Jf hutafuta wale wasiokuwa na mbele wala nyuma na kuwahada kuwa wao wanaelewa ukweli wa Mungano ( unapoambiwa ujiambie )
Viongozi wa Zanzibar wanataka madaraka zaidi na kwa bahati mbaya hakuna sehemu kubwa ya kuchukua madaraka hayo isipokuwa sehemu ndogo ya wananchi wa visiwa vya Zanzibar. Hivyo kinachofanyika ni kuunda serikali kubwa yenye ulaji kwa kila mtu wakisingizia mipaka ya Zanzibar na kadhalika. Wananchi wanafurahia kutia changa la macho mchana kweupeee. My take: makamu wawili wa rais!!
Mimi nawaomba sana viongozi wa Zanzibar kama kweli wanasimamia mawazo ya wananchi wake waombe kuuvunja Muiungano kisha yatakayofuatia baada ya hapo wagawane madaraka wanavyopenda. Lakini hawawezi kutumia nafasi ya Muungano kuleta madai kama vile mtu asiyeridhika ndani ya ndoa lakini hataki kuomba talaka isipokuwa kila siku kuongeza madai ili mradi kumuudhi mwenza wake akiwa ndani ya ndoa.
Zanzibar hawajawahi kusema wanataka kuuvunja Muungano na Bara ikawakatalia kama wailivyokuwa Nigeria. Biafra hawakutaka kujua nafasi yao ktk Muungano kuunda Nigeria, wao walitaka kujitenga kabisa na sio kuweka masharti ya ku share uongozi au kujitangaza kwamba wao ni nchi ndani ya Jamhuri kwani walikuwa nchi ndani ya Jamhuri!.
Kama Zanzibar wanataka kuuvunja Muungano kama wale Biafra waseme wazi! Nina hakika hakuna Mbara atakayewazuia isipokuwa tutakachowaomba ni utaratibu wa kisheria. Wapige kura za maoni kwa wananchi wao, wawaeleze hasara zitakazotokana na kuuvunja Muungano na kama wengi bado wataafiki na kura za ndiyo zikachukua ushindi bila shjaka tutavunja Muungano.
Lakini hatuwezi kuvumilia upuuzi huu unaotokea leo wa madai ya viongozi waliodandia Mapinduzi ambayo hawajui kwanza huu Muungano ulikuwa na maana gani kwa wananchi wake. Sijasikia kiongozi hata mmoja akizungumzia hizo kero za wananchi. mambo muhimu yanayowagusa Wazanzibar zaidi ya hii mipaka na kugawana vyeo hali pato la nchi nzima ya Zanzibar kwa mwaka halipishani na manispaa ya Ilala (Kariakoo).