Ni tukio gani limewahi kukufurahisha, kukuhuzunisha au kukushangaza ulipohudhuria sherehe?

Mcheza Viduku

JF-Expert Member
Jun 24, 2020
1,049
2,535
.............hapo kwenye hizo nukta nukta ni sehemu ya salamu na kila mtu atajibu vile atahisi nimemsalimia.

Wapwa kwenye hizi sherehe zetu huwa kuna mambo mengi sana yanatokea, mimi nikiwa mdau mkubwa wa hizi sherehe (MC) ninazo shuhuda nyingi sana za yanayotokea kumbini.

Hapo chini nitaziweka chache, na wewe mwanasherehe mwenzangu unaweza kutushirikisha siku ulipohudhuria sherehe yoyote nini kiliwahi;

Kukufurahisha sana
Kukuchekesha sana
Kukukera sana
Kukuudhi sana
Kukusononesha sana
Kukufedhehesha sana
Kukukasirisha sana
Kukushangaza sana

Kutoka kwa MC, mgeni mualikwa mwenzio, mwanakamati au familia ya wahusika wa sherehe, na ilikuwaje hebu tushirikishane hapa.

USHUHUDA WA KWANZA; kuna baadhi ya sherehe unapofika muda wa chakula taratibu huwa ziko wazi kabisa, wanatangulia maharusi, wanafuatia best man na best lady, halafu wale ma maids wao, baada ya hapo watainuliwa wazazi wa pande zote mbili nk, lakini cha kusikitisha ni kwamba wakitangulia maharusi tu tayari wageni waalikwa wanasimama na kuweka foleni ndeeeeeefu kama vile wanaenda kuchukua mahindi ya msaada kwenye ofisi za kata, HILI JAMBO HUWA LINASIKITISHA SANA.

USHUHUDA WA PILI; Wakati wa kutoa zawadi kuna baadhi ya Mc's wenzangu huwa wanafanya kama kuwadhalilisha wageni kwa kutoa maneno yasiyokuwa na staha kabisa kama vile "wewe kwa suti hiyo uliyovaa huwezi kukosa sh elfu 10 bwana, usiwaangushe wenye suti wenzio, HILI HUWA LINADHALILISHA SANA.

USHUHUDA WA TATU; Wakati huohuo wa zawadi, muda umeshakuwa sio rafiki sana na MC anajitahidi kukimbizana na muda, lakini wanakuja mashangazi na pea ya khanga, pea ya kitenge vikombe vya plastiki na shuka, wataomba mic wanataka waongeeeeee, MC akijaribu kuwasihi kuwa muda sio rafiki utawasikia wanasemea pale pale kwenye mic "MC tumekulipa utufanyie kazi yetu huna mamlaka ya kutupangia fuata matakwa yetu usitupeleke peleke bwana, unakuwa na haraka kama CHA KWANZA" HILI HUWA LINAMDHALILISHA MC, NA WAZAZI.

USHUHUDA WA NNE; Nikiwa mgeni mualikwa siku hiyo Mc aliyekuwa anaongoza ile sherehe alimuita babu aje afungue champagne wakati anajua mzee hawezi, akachombeza eti "babu kama inakushinda tumia meno" mzee akaanza kutumia meno ile champagne ikafunguka na kummwagikia usoni, wapuuzi kama yeye walicheka na kufurahi lakini pale Mc alifanya tendo la kumdhalilisha sana yule mzee, hakuishia hapo......kesho akaitundika mtandaoni kwenye page yake.

Haya ni machache sana kati ya mengi tunayokutana nayo huko ukumbini, kwako wewe ni yapi uliyowahi kuyaona/kuyasikia?

KWAKO MWALIMU KASHASHA.....
 
Usisikie utamu wa biriani la kwenye sinia:

1694609810829.png
 
Hakuna kitu sipendi kama chakula kuchelewa kwenye sherehe, ndio wapo mtakaosema mimo ni mroho lakini hapana fikiria waalikwa umewapeleka kanisani tangu saa saba halafu ukumbini wanywe soda moja chakula kifuate huko saa tano na nusu hii sio sawa

Sherehe kama mbili hivi niliondoka nikakabidhi zawadi kwa mtu
 
Bibi na wewe huwa unaenda kwenye sherehe
Sana tena sana, kwa siku hizindiyo wasaa wa kukutana na ndugu, jamaa na marafiki.

Kwetu mpaka leo nimeukataza na nnaupinga kaboisa kabisa utamaduni wa kualikana kwa kadi kwenye sherehe za harusi, ajae na aje. Tunaalikana kwa kwenda physically kila nyumba na unaemkuta hapo unamwambia waambie na wenzako.

Mpaka watoto na wajukuu wengine wanasema "huyu bibi kakaa kizamani".

Nawaonea huruma tu, hawaelewi mapenzi ya ndugu, jamaa na marafiki huzidi wanapokutana na kujiwachia free. Kama hajaonekana mmoja basi yeyote kwenye sherehe anashangaa na kustuka, fulani yuko wapi?, siyo kuulizana "fulani hajaalikwa"/ Ujinga mtupu.
 
Yah zamani mwaliko ulikuwa hivyo ila sikuiz umeisha

Nimekuja kuona mtwara bado wanaendeleza mwenye sherehe anatembea nyumba kwa nyumba na akikukuta njian anakupa kadi
 
Pale utaratibu wa kula unaofanywa na wagawaji wa sahani za vyakula bila foleni, mmekaa ukumbini sahani zinakuruka kama hawakuoni. Mwisho unakosa chakula kimeisha. Unaanza kuhaha kwenda kutafuta chakula kwingine nje ya ukumbi. Pia kuna kujikuta unapanga foleni na watoto wadogo kwenda kuambulia walau ukoko tu ule. Kwa kweli kuna visa vingi sana wakati wa kula kutegemeana na utaratibu uliopangwa na hadhi za harusi zenyewe kwa bajeti zao
 
Ahahahha umeenda harusi mchango ulikuwa single 20k? Sio
 
Na za uchoyo
Siku moja nimeletewa kadi, nilikuwa sifahamu ya nini, nimeipokea nikajisemea ntaisoma baadae, kuja kuisoma, kumbe ya mchango wa harusi. Nikaiweka pembeni.

Mara siku hiyo aliyeniletea kadi kanipigia simu, ananiuliza vipi, mbona bado? Nikamuulliza bado nini? Akanambia si umeipokea kadi? Nikamwabia ndiyo nimeipokea, akanambia kwa hiyo changia, nikamuuliza nichangie nini? Akanambia isome kadi, nikamwambi subiri, kuisoma, mchango 100,000 kima cha chini.

Nikamwambia huwa sichangii hatusi, akanambia kwanini uliipokea kadi? Nikamwambia shika adabu yako na adabu ikushike, njoo chukuwa kadi yako utaikuta nje hapo nimekuwekea. Nikalivurumisha kadi nje huko.

Toka siku hiyo sipokei kadi yoyote ile. Mtu akitaka kunipa tu, namwambia ondoka nayo.

Tumefikia pabaya sana. Hata undugu, ujamaa, urafiki wa siku hizi ni kwa maslahi tu.
 
Siku moja nimeletewa kadi, nilikuwa sifahamu ya nini, nimeipokea nikajisemea ntaisoma baadae, kuja kuisoma, kumbe ya mchango wa harusi. Nikaiweka pembeni.

Mara siku hiyo aliyeniletea kadi kanipigia simu, ananiuliza vipi, mbona bado? Nikamuulliza bado nini? Akanambia si umeipokea kadi? Nikamwabia ndiyo nimeipokea, akanambia kwa hiyo changia, nikamuuliza nichangie nini? Akanambia ssome kadi, nikamwambi subiri, kuisoma, mchango 100,000 kima chini.

Nikamwambia huwa sichangii hatusi, akanambia kwanini uliipokea kadi? Nikamwambia shika adabu yako na adabu ikushike, njoo chukuwa kadi yako utaikuta nhe hapo nimekuwekea.

Toka siku hiyo sipokei kadi yoyote ile. Mtu akitaka kunipa tu, namwambia ondoka nayo.

Tumefikia pabaya sana. Hata undugu, ujamaa, urafiki wa siku hizi ni kwa maslahi tu.
Kabisa bibi ila mimi mjukuu wako nikioa najua utanichangia tu 😂
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom