Van Halen
Senior Member
- Dec 4, 2013
- 111
- 188
Kumlaza mtoto chali wakati ukimlisha au kumywesha, ni hatari sana. Inatakiwa umweke kwenye hali ya kuinuka kidogo, ili chakula kishuke vizuri. But pia kuna kumlisha haraka haraka nalo pia ni tatizo. Mnaweza kuja kuua watoto.
Sent using Jamii Forums mobile app
Binafsi sitasahau Siku moja wakati namvalisha mwanangu akiwa na Miezi 3 baada ya kumuogesha nilishangaa maziwa yanatoka puani na mdomoni na hapo hapo mtoto akawa hawezi kupumua vizuri.
Nilipaniki nikakimbilia nje nkamtupia mama mmoja mtu mzima mtoto Huku Nikilia. Yule mama alinishauri tumpatie maji lakini bado mtoto aliendelea kukosa pumzi Huku mapovu yaliyochangamana na maziwa na mate mazito yanayovutika yakiendelea kutoka mdomoni na puani.
Nilikimbilia hospitali moja kwa moja mpaka chumba cha Daktari bila kupita mapokezi na kwa haraka sana wakachukua bomba flani flani za plastic wakazidumbukiza puani na mdomoni kwa wakati tofauti na kuanza kuvuta vyakula . Walipomaliza alipata sindano mbili akatulia.
Baada ya hapo walimlaza style ya recovery position na taratiiibu mtoto akapata nafuu nzuri tukaruhusiwa kurudi nyumbani.
Wewe ni tukio gani la kutisha lilikutokea wakati wa kulea mtoto mchanga Hadi alipojitambua na kuanza kuongea??
Sent using Jamii Forums mobile app