Ni tukio gani hutalisahau katika malezi ya mtoto kuanzia age 0?

Mrs Bishanga

JF-Expert Member
Jun 30, 2013
1,002
2,272
Binafsi sitasahau Siku moja wakati namvalisha mwanangu akiwa na Miezi 3 baada ya kumuogesha nilishangaa maziwa yanatoka puani na mdomoni na hapo hapo mtoto akawa hawezi kupumua vizuri.

Nilipaniki nikakimbilia nje nkamtupia mama mmoja mtu mzima mtoto Huku Nikilia. Yule mama alinishauri tumpatie maji lakini bado mtoto aliendelea kukosa pumzi Huku mapovu yaliyochangamana na maziwa na mate mazito yanayovutika yakiendelea kutoka mdomoni na puani.

Nilikimbilia hospitali moja kwa moja mpaka chumba cha Daktari bila kupita mapokezi na kwa haraka sana wakachukua bomba flani flani za plastic wakazidumbukiza puani na mdomoni kwa wakati tofauti na kuanza kuvuta vyakula . Walipomaliza alipata sindano mbili akatulia.

Baada ya hapo walimlaza style ya recovery position na taratiiibu mtoto akapata nafuu nzuri tukaruhusiwa kurudi nyumbani.

Wewe ni tukio gani la kutisha lilikutokea wakati wa kulea mtoto mchanga Hadi alipojitambua na kuanza kuongea??
 
Mimi alinitisha kipindi anachelewa kulala,analala sita au saa saba usiku!!!! Alfajiri nasikia mtu ananing'ata ng'ata sikio,kumbe na anaamka kabla yangu saa 11 hiyo!!!! Halafu na mchana halali!!!! Halafu kachangamka full time yaani yupo full mzuka 24/7!!!!....Yaani bado najiuliza huyu dogo ni wapi? Katokea wapi? Kafikaje hapa
 
ilinitokea hio pia, ilikua usiku tatizo ni kua nilimnyonyesha halaf nikawa nambadili hivo vile kumuinua ndio kulisababisha na kumgeuza huku na huko kizuri nilikua nakaribia kumaliza 40 nilikua nyumbani mama alinisaidia kumueka begani lakini mtoto alikua ahemi vizur niliogopa mama akanituliza akakaa tu sawa

matukio ni mengi kuna zile sindano za paja kalivyoanza zile za mwez kilio mpaka homalikapanda ikafikia hatua halali analia na akilia kama amashtuka hivi mim ni kupaniki tu nikamnywesha panadol at least ikapunguza japo tulikesha
 
Alikuwa bado hajaanza kula vitu solid.
Ana miezi 7 ile kumpa mpa uji smoothie na kunyonya.
Usiku hajalala anahangaika sana nikajua anaumwa tunbo basi alfjr nasema nampeleka hospital heee naamka nampikia uji na kunywa ametulia na kucheza alikunywa sana.
Kumbe ilikuwa njaa bwana.

mama wawili
 
tukio hili lilimtokea mdogo wangu, mama alinituma maji safi ya uhai kwa aajili ya kunywa mtoto, nikamletea, sasa baadae mama akajichanganya akachukua chupa ya mafuta ya taa iliyofanana na ile ya maji, akamnywesha dogo wese tena akiwa na miezi kazaa, tunakuja kustuka baadae mtoto kalegea hatari hapigi kelele, tukajua anaumwa, sijui nini kilimstua bi mkubwa aangalie yale maji aliyompa dogo, ndo kugundua ni wese bhana, alipiga ukelele wa ajabu na kumuwahi mtoto na kukimbilia nje kwa majirani huku analia, majirani walimsaidia kumuwahisha dogo hosp ndo ikawa pona yake. leo hii dogo yupo 4m3 tukikaa na bi mkubwa namkumbushiaga kile kisa, anabaki kucheka tu.
 
nikiwa nimerud hme kichanga kimelazwa nishasahau kama kuna kichanga, sinikajitupia dah! naskia tu kinalia nilihisi nimeua bt mungu ni mkubwa sana wakuu.. watoto hulindwa na malaika wa mungu coz kama sivyo kichanganya kisingepona maana kilo zangu 75 zililala juu ya kichanga, hadi leo hua siamini na nikikasimulia hua tunacheka tu
 
tukio hili lilimtokea mdogo wangu, mama alinituma maji safi ya uhai kwa aajili ya kunywa mtoto, nikamletea, sasa baadae mama akajichanganya akachukua chupa ya mafuta ya taa iliyofanana na ile ya maji, akamnywesha dogo wese tena akiwa na miezi kazaa, tunakuja kustuka baadae mtoto kalegea hatari hapigi kelele, tukajua anaumwa, sijui nini kilimstua bi mkubwa aangalie yale maji aliyompa dogo, ndo kugundua ni wese bhana, alipiga ukelele wa ajabu na kumuwahi mtoto na kukimbilia nje kwa majirani huku analia, majirani walimsaidia kumuwahisha dogo hosp ndo ikawa pona yake. leo hii dogo yupo 4m3 tukikaa na bi mkubwa namkumbushiaga kile kisa, anabaki kucheka tu.
Nakumbukaga kuna maza mmoja nae ashawahi fanyajaga hii kitu kwa mwananaye pia alimpa wese badala ya maji

yess BishOoo haSwaaaaaaaH
 
Hiyo ya kwako ya mtoto kutoa maziwa puani na povu.ilinitokea.
Nilimbeba pekupeku kwa jirani kuomba msaada.wakanituliza kisha wakanambia nimnyonye pua.nikafanya hivyo.
Alipona sijampeleka hata hospital.ila nililia balaa
 
Back
Top Bottom