Ni tangazo lipi la biashara la TV au redio unalichukia/unalipenda?

four eyes

JF-Expert Member
Jan 11, 2017
905
1,406
Habar wadau,
Sanaa ya utengenezaji matangazo ya biashara Sasa hv imekua Sana na hata nchini kwetu si haba imeboreka Sana. Zamani matangazo ya biashara katika TV au redio ilikuwa ni kero kubwa kutokana na mengi kujali tu kuitangaza biashara husika Bila kumfanya msikilizaji kulipenda tangazo lenyewe

Kwa nchi za wenzetu matangazo haya huwa wanayajali Sana kiasi cha kuhakikisha yanavutia mno, Kwa wale watumiaji wa ving'amuz mtakuwa mnaona station za nje zilivyo na matangazo ya biashara ya kuvutia,mfano ukiwa unaangalia mpira Kwa supersports kabla ya mpira kuanza au halftime huwa Kuna matangazo ya biashara lakini yanavutia mno kiasi kwamba huwa ni sehemu ya burudani kuyatazama na huachoki.

Binafsi hapa Tanzania Kuna matangazo huwa siyapend balaa,mfano Kuna lile la timiza,yupo jamaa flan kashika gitaa kavaa viatu vya ajabu anaimba timiza timiza timiza ni mkombozi,silipendi kwelkwel,jingine la benk flan ni la redio yupo jamaa anaulizwa vitu na Dada flan yeye anajibu tofauti kama amechanganyikiwa,lengo la tangazo lilikuwa ni kulifanya lichekeshe lakini Kwa kuwa mwanaume yule anaongea Kwa kusoma skripti limekuwa baya tu,

Zaman clouds walikuwa na jamaa anayeigiza kikurya ktk matangazo ya redio niliyapenda Sana na yalikuwa yanachekesha mno. Juzjuz kulikuwa na tangazo la Tigopesa la mama wa nyumban yuko na mwanae mdogo yule mtoto siku anaanza kuongea anatamka ni tigopesa nililipenda Sana lile sikuwah kulichoka lakini limepotea ghafla, matangazo mengine nisiyoyapenda ni Yale ya mpoto dah siyapend kwelkwel.

Karibu mdau uchangie nawewe kuhusiana na tasnia hii ya matangazo ya biashara yapi yanakuboa na yapi unayapenda
49a560c81a72dd2754d45bc6bb2c6f1f.jpg
 
tangazo la LAPF lililofanywa na King Majuto ni tangazo bovu kuliko yote tanzania


Kweli kbs. Tangazo hovyo sana. Halina ubunifu wowote. Kuna na lile jingine la profesa chapati, yani buree kabisaaa!!.
Tangazo bora ni lile la Coca Cola la wale machali wawili, mtu na mdogo wake.. boooonge la tangazo asee. Mi mpaka nimeli download kwenye simu yangu
 
matangazo yote ya sabuni za unga
nayachukia sana kwa uongo uliopitiliza
halafu kuna lile la godoro host ni monalisa
na matangazo yote ya coca-cola sio kama mabaya yanapata air time ya kutosha mpaka yanakera
by the way for me coca-cola ndiyo kampuni inayotengeneza matangazo mazuri kupita kampuni yoyote ile duniani
 
Kuna tangazo la Tigo wamecopy wakakosea kupaste.(sijui kuku akifungwa kamba......)
Nadhani wewe ndio haujajua Lengo la tangazo na bidhaa inayotangazwa ndiomana huelewi kinachoendelea kwenye tangazo lile
 
nilikuwa nayapenda sana matangazo ya "" Haki Elimuuu"' mfano lile la '' alright student - ah students'' Mengine yale ya Fataki, yaani nilikuwa nayapenda ; kuna tangazo moja Fataki anajifanya anajua sana kucheza bao '' eti yuko leo nakutwanga , cheza cheza sasa , cheza ! afu jamaa anamwambia ' tulishakustukia fatakiiii, hapa nia yetu tukupotezee tu kusubiri wanafunzi wa kike, afu lifataki linaondoka linalaumu; kazi kuharibia dili za wenzenu, lingine nalolipenda lile la Redio one - Haijalishi uko pande gani , kitaani ama nyumbani kipindi kiko hewani sikiliza... nisiyoyapenda yako kibao, moja ni lile la joti la tigo, sijui lulu anasema babu mi nilitaka ujibu swali la archmedes principle , silipendi
 
Kuna tangazo la Tigo wamecopy wakakosea kupaste.(sijui kuku akifungwa kamba......)
Hilo silipend kwelkwel hata mm,yule jamaa kaharibu Kwa kuongea huku anasoma script bas linaboa hatar na clouds kila dakika wanaliweka
 
Nachukia lile tangazo la timiza
Eti mi nimekopa zaidi ya laki
Sita sijui nimenunua vifaa vya bandi yangu
Kisha yule jamaa anaanza kuimba imba

Timiza timiza, yani likipita tu nahama kabisa hiyo channel
Hata mm aisee,kwanza jamaa ivyo na anavyoimba dah hovyo kwelkwl
 
matangazo yote ya sabuni za unga
nayachukia sana kwa uongo uliopitiliza
halafu kuna lile la godoro host ni monalisa
na matangazo yote ya coca-cola sio kama mabaya yanapata air time ya kutosha mpaka yanakera
by the way for me coca-cola ndiyo kampuni inayotengeneza matangazo mazuri kupita kampuni yoyote ile duniani
Kwel coca Cola Wana ubunifu kupita kiasi,na ukitaka kuwapenda zaidi ni wakati WA christmass huwa Wana matangazo mazuri Sana wakati huo
 
nilikuwa nayapenda sana matangazo ya'' Haki Elimuuu'' mfano lile tangazo la -alright student- ah students, menginge niliyokuwa nayapenda ni matangazo ya Fataki, kuna tangazo Fataki eti anajifanya anajua sana kucheza Bao-yuko; ''leo nakukomesha, cheza ,cheza sasa, jamaa linajibu, we leo tulitaka kukuharibia tu, maana hiyo tabia ya kufuatilia vitoto vya shule inatukera sana hapa mtaani, afu li fataki linajibu- mijitu mingine bwana, kazi kuharibu dili za wenzao tu ! lingine ni kale ka wimbo ka Redio One, Haijalishi uko pande gani, kitaani ama nyumbani, kipindi kiko hewani sikiliza.... ambalo silipendi ni lile la Tigo ambapo Lulu anamwambia babu ulitakiwa kujibu swali la archmedes principle , silipendi.
 
Nadhani wewe ndio haujajua Lengo la tangazo na bidhaa inayotangazwa ndiomana huelewi kinachoendelea kwenye tangazo lile
Sio kwel bwana,Lengo tunajua lilikuwa kuonyesha kuchanganyikiwa na mambo mwanzoni mwa mwaka kutokana na mambo kuwa mengi,lakini walitaka pia kuiga vichekesho flan ktk huyo mtu anayeongea vitu tofauti na alivyoulizwa lakini wakafeli limeboa badala yake
 
Back
Top Bottom