Ni shida

Ok9

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2013
Posts
4,554
Reaction score
4,171
“Ha ! Ha ! Ha ! Huyo binti yako anaitwa nani ?”
“Ah ! Achana naye, naona hasira hata kulitaja
jina lake, ” alisema mama Juliana huku
akionesha hasira za waziwazi kwa binti yake
huyo .
Muda wa makesheshe uliwadia , mama Juliana
ndiye aliyeanza kumchokoza kijana wake huyo
huku akiwa anahema kwa mihemo ya kimahaba
niue…
“Mpenzi wangu Bitungu , ” alisema mama Juliana
huku akichekacheka kimahaba.
Bitungu hakumwitikia mama Juliana bali
alimshika na kumwangushia kitandani…
“Lakini leo sitaki ile njia yako , nataka njia
yangu, ” alisema mama Juliana.
“Noo ! Sitaki mpenzi , nilishakwambia tangu siku
ya kwanza uliponionjesha njia ile kwamba sitaki
kusikia njia nyingine , ulitaka mwenyewe lazima
tuitumie njia hiyo , ” alisema kijana huyo kwa
sauti iliyojaa uchu .
Mama Juliana hakuwa na jinsi ilibidi akubaliane ,
walipanda kitandani na kuanza kuchezeana
kwanza katika hali ya kupasha misuli ili waingie
uwanjani.
“Mpenzi , hebu nionjeshe njia nyingine basi
jamani, ” mama Juliana alijaribu bahati yake
lakini Bitungu akakataa katakata.
Muda ulifika , mama Juliana akajitega kwa njia
ile ili mambo yaishe ambapo Bitungu naye
akaingia uwanjani kuanza soka .
***
Mara ya kwanza , Bitungu kukutana na mama
Juliana alishangaa sana . Sehemu kubwa ya
kufahamiana kwao kulianzishwa na mwanamke
huyo licha ya kuwa na umri mkubwa na kijana
huyo alikuwa kama mwanaye tu .
Siku walipokwenda kwa mara ya kwanza gesti ,
Butungu alishtuka wakati wa mechi kuanza
kumwona mwanamke huyo anamwelekeza kupita
kwenye njia tofauti kabisa na aliyoizoea.
Hali hiyo ilimpa wakati mgumu sana Bitungu ,
hata mama Juliana alilijua hilo . Lakini kwa vile
alikuwa akimpa pesa nyingi kijana huyo ,
akajikuta anazoea mpaka mwishowe akawa
hataki njia nyingine zaidi ya ile aliyofundishwa
na mwanamke huyo .
Tabia hiyo ndiyo iliyosababisha Bitungu
akaachana na demu wake , Siliani baada ya
kukutana naye siku moja na kutaka kumpitia
kwa njia aliyofundishwa na mama Juliana. Mzozo
mkubwa uliibuka mpaka Siliana akataka kumvaa
Bitungu.
***
Baada ya siku hiyo kwa mama Juliana, Bitungu
aliendelea na mambo yake kwa ahadi ya
kukutana siku tatu mbele . Walikuwa wakikutana
mara tatu au nne kwa wiki moja yenye siku
saba.
***
Siku hiyo isiyokuwa na jina , simu ya Bitungu
iliita , alipoangalia jina halikuwepo, akaipokea …
“Haloo …”“ Haloo, naitwa Juliana, tulikutana
benki …”
“Ooo , baby wangu , vipi ?” alisema Bitungu…
“Poa , mzima wewe ?”
“Mi mzima sweetheart, umenitosa halafu
mbaya zaidi siku ile namba hukunipa zaidi ya
wewe kuchukua ya kwangu ukasema utanibip
lakini hukufanya hivyo. ”
“Mambo mengi jamani, nisamehe bure . ”
“Nimeshakusamehe baby, niambie. ”
“Uko wapi ?”
“Nipoo … nipo wapi hapa, panaitwaaaa … yaani ni
jirani na Amana…”
“Ndiyo unaishi hapo au?”
“Hapana , kuna mtu nilikuwa naongea naye
ndiyo nimemalizana naye sasa . Je , naweza
kukuona ? Si uliniambia unaishi Ilala !”
“Yap ! Unataka nije ?”
“Ndiyo maana yake jamani Juliana…”
“Basi nakuja. ”“ Chukua Bajaj , ukifika jirani na
Amana nipigie please . ”
“Poa . ”
Bitungu alijipongeza sana kupigiwa simu na
binti mzuri kiasi kile , hakuamini hata chembe
hivyo alikaa mkao wa kusubiri…“Ikibidi
nisimkawize , leoleo nikamalizane naye. Tena siku
ile alionekana kama ni mtoto wa mjini , si ajabu
anajua kutumia njia ile , ” alisema moyoni
Bitungu.
Je, unajua nini kiliendelea?
 
“Ikibidi nisimkawize , leoleo nikamalizane naye.
Tena siku ile alionekana kama ni mtoto wa
mjini, si ajabu anajua kutumia njia ile , ” alisema
moyoni Bitungu .
ENDELEA SASA …
Ndani ya dakika kumi, simu ya Bitungu iliita ,
aliyepiga Juliana…
“Umefika wapi baby?”
“Ndiyo nashuka kwenye Bajaj hapa Amana. ”
“Oke, utaona baa kushoto kwako kama unaenda
Boma . ”
“Nimeiona . ”
“Njoo hapa. ”
Juliana alitembea hadi kwenye baa hiyo na
kuungana na Bitungu ambaye alisimama na
kumbusu Juliana baada ya kufika huku akimwita
baby kibao .
“Karibu ukae mama . ”
“Asante, ” aliitika Juliana . Moyoni Bitungu
alipenda sana anavyomwita Juliana mama na
yeye amwite baba. Au baby na yeye amwite
sweet lakini Juliana kwake ilikuwa ni mapema
sana kufanya hivyo.
Juliana alifikia kuagiziwa kinywaji chenye pombe
lakini si kali . Katika kunywa, maongezi
yalikuwepo pia . Muda mwingi Bitungu ndiye
alikuwa msemaji , Juliana anajibu mpaka pale
naye Juliana alipoanza kuchangamka kwa pombe
wakaanza kwenda sawasawa.
“Kwani we huna mchumba ?” aliuliza Juliana kwa
sauti ya kukatakata …
“Sina mama . ”
“Mpenzi je?”
“Hata mpenzi sina . ”
“Mmmh ! Rafiki wa kike je?”
“Pia sina. ”
“Huo uongo sasa. ”
“Hata huo sina. ”
“Nini ?”
“Huo uongo. ”
Kifupi walishakolea wote, wakacheka na
kuendelea kunywa . Mara simu ya Bitungu iliita ,
akawahi kuangalia kwenye kioo …
“Huyu mwanamke naye msumbufu sana, ”
alisema .
“Ni nani kwani ?”
“Ah ! Mama mmoja hivi , ananisumbua sana. ”
“Anataka nini kwani ?”
“Eti anataka awe mpenzi wangu . ”
“Si umkubalie sasa ?”
“Baby, kumbe hunipendi wewe. Nimkubalie
wakati ni mke wa mtu . ”
“Sasa kama ni mke wa mtu kwa nini
anakufuatafuata?”
“Si ndiyo namshangaa, halafu muda mrefu sana
sipokei lakini haachi kunipigia . ”
“Achana naye, ukiona hivyo si ajabu hata huyo
mume hana anajishaua tu, ” alisema Juliana bila
kujua kwamba mwanamke mwenyewe
anayepondwa hapo ni mama yake mzazi na wala
maneno ya kijana huyo hayakuwa yakitoka
moyoni .
“Sasa inakuaje baby?” Bitungu aliuliza swali
hilo …
“Kuhusu ?”
“Si tunaondoka ?”
“Kwenda wapi ?”
“Aaa! Maeneo . ”
“Maeneo ndiyo wapi ?”
Bitungu akagundua kwamba, Juliana ni
msichana anayependa uwazi , hivyo akaamua
kumpasukia …
“Twende gesti. ”
“Poa , ” Juliana alijibu kwa mkato kiasi kwamba,
Bitungu alihisi hajasikia japokuwa alisikia …
“Umejibuje ?”
“Nimesema sawa. ”
“Sawa nini?”
“Si umesema twende gesti. ”
“Oke, basi tumalizie vinywaji vyetu twende. ”
Juliana alivuta kinywaji chake na kuanza
kusimama huku Bitungu naye akimalizia, naye
akasimama . Simu ya Juliana iliita , akaiangalia
na kusema …
“Mama huyo anapiga . ” Alimwangalia Bitungu
kama anayeomba msaada kwake amjibu nini
mama yake…
“Pokea , mwambie upo kwa rafiki yako . ”
“Haloo mama … eee… . nipo kwa Zaina hapa
nyuma … sichelewi mama … kweli tena . ”
Baada ya kukata simu , Bitungu alimuuliza
Juliana kama anaishi na baba pia …
“Ndiyo, lakini baba si mkali sana lakini hata
mama yangu si mkali kabisa ila hapendi
ujingaujinga japokuwa na yeye huwa
simwelewagi . ”
“Humwelewagi kivipi ?”
“Yaani nahisi kama anachepuka. ”
“He ! Yaani mama yako unasema anachepuka ,
we vipi ?”
“Si ndiyo ukweli lakini . ”
Walifika gesti, wakapanga chumba kwa siku
nzima japokuwa Juliana alisema hataweza
kulala .
Ilikuwa dakika chache lakini zenye mahaba
mazito kwani Bitungu alianza na
kumchezeachezea Juliana sehemu mbalimbali za
mwili wake huku msichana huyo naye akionesha
ushirikiano wa hali ya juu .
Mchezo ulipoanza , Juliana alishtuka na kuruka
baada ya kubaini kwamba, Bitungu alikuwa
akitaka kumpitia kwa njia nyingine .
“He ! Vipi tena ?” aliuliza Juliana akiwa
amemsukumia mbali Bitungu …
“Kwani vipi ?”
“Kwani vipi kivipi ? Unakwenda wapi huko ?”
“Aaa! Ina maana hujui?”
“Aka! Sitaki sitaki sitaki , kumbe ndivyo ulivyo,
doo ! Basi mi naondoka . ”
“Sikia Juliana. Unajua kupenda kunajumuisha na
mambo mengi ikiwa ni pamoja na kukubaliana
na ujinga wa mwenzako , kama mimi nakupenda
kweli , hata ujinga wako unakuwa wangu , siwezi
kusema sikupendi kwa sababu una kidonda , sasa
kama umeona mimi nina kidonda ambacho kina
kukera kubaliana nacho tu, ” alisema Bitungu
kwa sauti iliyojaa ushawishi wa hali ya juu .
Je, unajua nini kiliendelea?
 
cc nyambari Nyangwine uje utuchambulie huku...
 
Last edited by a moderator:
Huyo mdudu anahema hivyo binadamu ni zaidi. ....
 
Kilicho endelea ni wewe kututaka sie tutumie akili zetu kuendeleza hadithi yako ya mpenda kula viboga
 
ILIPOISHIA RISASI JUMAMOSI :
“Sikia Juliana. Unajua kupenda kunajumuisha na
mambo mengi ikiwa ni pamoja na kukubaliana
na ujinga wa mwenzako , kama mimi nakupenda
kweli , hata ujinga wako unakuwa wangu , siwezi
kusema sikupendi kwa sababu una kidonda , sasa
kama umeona mimi nina kidonda ambacho
kinakukera kubaliana nacho tu, ” alisema
Bitungu kwa sauti iliyojaa ushawishi wa hali ya
juu .
JIACHIE MWENYEWE …
“Pamoja na lugha tamu anko , lakini mimi siko
tayari kwa matumizi hayo , sijawahi kujihusisha
hata siku moja, ” alisema Juliana kwa sauti
iliyojaa masikitiko…
“Hata hiyo uliyoizoea si ulianza siku moja
kwanza Juliana?”
“Ndiyo. ”
“Sasa inakuwaje unashindwa hilo ?”
“Hapana kwa kweli , siwezi anko . ”
Bitungu aliamini kuwa , Juliana alikuwa hajui
hata hiyo njia halali . Na kama atakuwa anajua
basi ni juujuu tu lakini si kwa kina maana alijua
mademu wote wa mjini ni watundu siku hizi .
“Angekuwa mtundu kwanza asingeniita anko
wakati tumekuja wote mpaka chumbani gesti
sasa uanko unatokea wapi ?” alijihoji mwenyewe
Bitungu akiwa amekata tamaa kupita kwa
Juliana kwa kutumia njia ile nyingine .
Ilibidi akubaliane na matakwa ya Juliana,
kwenda kwa njia ya kawaida ambapo walianza
kwa kuchezeana kwanza huku Juliana akiwa
tayari ameanza kuhema kwa nguvu kuashiria
kwamba, tayari alikuwa amefika mbali na
alichotaka kwa wakati ule ni uhalisia tu.
Bitungu aliishangaa sana hali ya Juliana , hasa
alipomwona amebadilika kwa kila namna ,
akihema sana , akiwa hatulii kitandani na zaidi
sana akionesha macho yaliyojaa ulegevu wa
kimahaba.
“Juliana baby, ” aliita kijana huyo .
“Niambie anko …”
“Aaah ! Mimi siyo anko wako bwana , mimi ni
mpenzi wako . ”
“Jamani… hilo litakuja automatiki, ” alijibu
Juliana huku akiweweseka pale kitandani.
Ni Juliana ndiye aliyetoka kitandani na
kusimama kisha akamshika mkono Bitungu na
kumtoa kitandani, wakasimama wote.
Juliana alianza kumvua nguo jamaa akianzia na
juu hadi chini . Alipomaliza akajigeukia yeye,
akajivua nguo zote na kutangulia kitandani.
***
Mama Juliana alimpigia simu Bitungu kwa
dakika tano nzima lakini ilikuwa ikiita tu bila
kupokelewa…
“Huyu leo ana nini? Mbona si kawaida yake
kutopokea simu, ameiacha wapi ?” alisema
mwanamke huyo huku akiwa amejiinamia ,
akakumbuka kwamba, Juliana naye licha ya
kumwambia yupo jiraji na kwamba hatachelewa
kurudi lakini alikuwa hajarudi , akashikwa na
hasira…
“Huyu mtoto naye mpaka saa hizi ? Amekwenda
wapi ? Na hii tabia ya kuchelewa kurudi
nyumbani kisa yuko kwa majirani ameianza lini
kwanza?”
Alichukua simu na kumpigia Juliana. Simu iliita
kwa muda mpaka ikakata yenyewe. Wakati simu
hiyo ikikata, Juliana alikuwa katikati ya uwanja
akiserebuka na Bitungu.
Ilikuwa ni mara ya kwanza kwa kijana huyo
kuoneshwa staili mbalimbali za uwanjani na
mwanamke. Hakuzoea, mara nyingi yeye ndiyo
anayekuwa kiongozi wa staili .
“Baby, twende chini sasa , ” alisema Juliana
akiwa tayari ameshuka…
“Baby turudi kitandani…”
“Baby wewe kaa kwa hivi . ”
“Baby geukia kule mimi nigeukia kwa hivi . ”
Hayo yote yalikuwa maneno ya Juliana kwa
Bitungu kiasi cha kumchanganya kijana huyo na
kujikuta hajui amweke kwenye fungu gani
msichana huyo . . .
“Kumbe kuniita baby lilikuwa suala la muda tu, ”
alisema moyoni Bitungu akiwa anatoka jasho na
kufutwa kwa shuka huku akiangaliwa usoni kwa
macho yaliyojaa mahaba mazito kwake .
Hata pale Bitungu alipotangaza kuwasili kwenye
kituo cha safari yake, Juliana alimwambia bado,
avute subira kidogo .
Bitungu alipata mtihani mzito, alikuwa akijizuia
kwa kupunguza kasi , wakati mwingine
alipozidisha kasi na kutangaza kufika safari
yake akaambiwa bado, alisema moyoni …
“Nimepatikana leo. ”
Kumbe kwa Juliana, dakika arobaini na tano
nzima za mchezo bado anakuwa moto , kuanzia
hapo ndipo anaweza kutangaza kufika kwenye
kilele cha mlima wanaoupanda. Sasa Bitungu
yeye alizoea dakika saba au kumi za mchezo
awe kama amecheza kipindi cha kwanza.
Ilikuwa wakati Bitungu yu hoi kabisa akitamani
Juliana augue ghafla ili waache , ndipo
alipotangaziwa kuwa sasa wafike wote lakini
wakati huo kijana huyo alikuwa amejizuia kiasi
cha kuwaza mambo mengine tena yale ambayo
ni kero ili amudu kwenda na biti za demu huyo .
“Haa ! Haa ! Daa !” alikuwa akihema Bitungu
huku Juliana akiwa katika pozi la kawaida sana
kama vile alitoka kubeba godoro tu kutoka
sebuleni kupeleka chumbani .
“We Juliana, ” aliita Bitungu …
“Abee …”
“Abee nani?” Bitungu aliuliza akitaka kujua
kama bado anakubalika kuitwa baby au lilikuwa
jina la kitandani tu!
“Abee sweetheart. ”
Bitungu akafurahi sana kusikia kwamba hata
nje ya kitanda ameitwa jina zuri zaidi
kimahaba…
“Hivi nani amekufundisha ?”
“Nini ?”
“Kufanya haya uliyonifanyia kitandani leo?”
“Mimi mwenyewe utundu wangu . ”
“Mh! Usiniache baby?” alisema Bitungu .
“Siwezi kukuacha dear labda uniache wewe .
Mimi nataka tufike mbali sana zaidi ya hapa. ”
“Hata mimi, natamani ikibidi tufunge ndoa. ”
“Kweli sweet ?”
“Sana tu. ”
Simu ya Juliana iliita tena …
“Mungu wangu … yaani huyo ni mama bila ubishi
wala kujiuliza , ” alisema Juliana akiifuata simu
yake…
“Si nilisema… sasa ngoja niweke loud speaker
usikie mitusi yake, ” alisema Juliana huku
akiiseti simu hiyo .
“We nguchiro usiyefaa kufungwa na binadamu ,
mwana wa shetani mtesa wanadamu, kenge
mwenye mabaka uko wapi ?”
Je, unajua nini kiliendelea?
 
ILIPOISHIA
“Mungu wangu … yaani huyo ni mama bila ubishi
wala kujiuliza , ” alisema Juliana huku akiifuata
simu yake…“ Si nilisema … sasa ngoja niweke loud
speaker umsikie mitusi yake, ” alisema Juliana
na kuiseti simu hiyo ili sauti ya mpigaji isikike .
“We nguchiro usiyefaa kufugwa na binadamu,
mwana wa shetani mtesa wanadamu, kenge
mwenye mabaka , uko wapi ?”
JIACHIE KIVYAKO…
“Nipo njiani narudi mama …”
“Nipo njiani narudi mama , ” mama mtu aliirudia
kauli ya bintiye huku akiwa ameziba pua…
“Unarudi na ndege au gari dogo, mbona sisikii
kelele ?”
“Natembea kwa miguu mama . Si nilikwambia
nipo hapa jirani . ”
“ Nakuuliza mbona sisikii kelele ?”
“Mama , mtaa huu watu wametulia sana , si
kama hapo kwetu, ndiyo maana . ”
“Kwa hiyo unataka kuniambia wewe ni mwenyeji
sana na huo mtaa kuliko mimi mama yako
siyo?”
“Hapana mama . ”
Wakati Juliana anazungumza na mama yake,
Bitungu alimsogelea hadi jirani ili kuisikiliza
sauti hiyo vyema kama anayeijua …“Mh, ”
aliguna Bitungu .
Baada ya kukata simu , Juliana alimuuliza ni kwa
nini alimsikilizia kwa karibu sana…
“Sauti kama naijua kwa mbali . ”
“Kama ya nani?”
“Mtu mmoja hivi lakini najua siye , ” alisema
Bitungu. Waliachana na hayo , Juliana alijiandaa
harakaharaka na kuondoka baada ya kumpiga
busu zito kijana huyo …
“Nitakumisi sana baby, ” alisema Juliana .
“Hata mimi. ”
***
Bitungu alikaa kitandani akijifikiria . Alimuwaza
Juliana akahisi kama anafaa kuwa mpenzi wake
wa moja kwa moja…
“Sijui ndiyo awe mchumba wangu ?” alijiuliza
Bitungu. Mara simu yake iliita , alikuwa mama
Juliana. Safari hii akaipokea …
“Jamani baby, mbona hukuwa unapokea simu
yangu, ulikuwa na malaya gani leo?”
“Hamna baby bwana , nililala sehemu sikuwa
najisikia vizuri . ”
“Ulilala sehemu wapi , ina maana si nyumbani
kwako siyo?”
“Siyo. ”
“Wapi ?”
“Nipo hapa Ilala Amana . ”
“Ilala Amana ? Uko na nani ?”
“Mwenyewe. ”
“We mwongo , kama kweli niruhusu nije . ”
“Njoo . ”
Mama Juliana alikata simu bila kutaka kuuliza
Amana sehemu gani . Alimpigia simu mumewe
kumuuliza anarudi saa ngapi , akamwambia
atachelewa .
“Oke, ” mama Juliana alikata simu kwa mumewe.
Akaondoka muda huohuo , anafika nje
anapishana na Juliana…“Ndiyo unafika sasa,
siyo?”
“Ndiyo mama . ”
“Mimi narudi muda si mrefu. ”
“Kwani unakwenda wapi ?”
“We , koma ukomaye . Swali gani unaniuliza mimi
mama yako ?”
***
Mama Juliana aliposhuka Amana ndiyo
akampigia simu Bitungu na kumuuliza aliko …
“Ukishashuka vuka barabara, mbele kuna mtaa
umeingia, fuata huo hadi jirani na nyumba
moja ina genge nje utaona gesti kwa mbele , ”
alisema Bitungu akiwa anatoa maelekezo kwa
mama Juliana.
Kwa jinsi mama Juliana alivyokuwa na hamu na
kijana huyo , hakusema sawa baada ya
maelekezo , yeye alikata simu tu na kuanza
kutembea kuelekea alikoelekezwa .
Aliingia kwenye gesti hiyo akiwa amesahau
kumuuliza Bitungu namba ya chumba. Mbaya
zaidi simu yake ilizima chaji, hivyo aliamua
kugonga kila chumba na kuuliza …
“Ngo ngo ngo!” aligonga mlango akasimama
mwanaume…
“Nikusaidie ?”
“Samahani , kumbe si hapa!”
Akaenda mlango mwingine… .
“Ngo ngo ngooo!”
Akatoka msichana , akasimama mlangoni akiwa
na taulo…
“Unamjua Bitungu ?”
“Bitungu ! Ndiyo nani?”
“Kijana mmoja hivi , nilidhani uko naye. ”
Yule msichana aligeuka kuangalia ndani, mama
Juliana akaamini kweli msichana huyo alikuwa
na Bitungu ndiyo maana aligeuka kuangalia
ndani, akamsukuma msichana yeye akazama
ndani…
“He ! We mama vipi ?”
“Bitungu unadiriki kuni… oooh ! Sorry kijana,
nisamehe bure nilidhani ni Bitungu. ”
Kijana aliyelala kitandani akiwa kama
alivyozaliwa alimrukia mama Juliana akitaka
ajue ni kwa nini aliingia bila maelewano…
“Huwezi kusema sorry halafu ukavamia hivihivi ,
nani amekwambia mimi ni Bitungu?” alihoji
kijana huyo , akamshika mama Juliana na
kumwangusha kitandani na kutaka kumwingia
kwa mabavu…
“Noo , Bwakila usifanye hivyo, ” alisema yule
msichana …
“Noo , huyu mama ndiyo dawa yake hii , ndicho
alichotaka lazima akipate. ”
Ilibidi yule msichana amkabe kwa nguvu Bwakila
ili amtoe mama Juliana ambaye wakati huo
alishashindwa kwa pumzi na nguvu
pia. “Mwanangu nisamehe sana , kweli kabisa
nilidhani wewe ni Bitungu, nisamehe sana
baba. ”
Je, unajua nini kiliendelea? Usikose kusoma
chombezo hili jipya
 
ILIPOISHIA RISASI JUMAMOSI :
“Noo , Bwakila usifanye hivyo, ” alisema yule
msichana …
“Noo , huyu mama ndiyo dawa yake hii , ndicho
alichotaka lazima akipate. ”
Ilibidi yule msichana amkabe kwa nguvu Bwakila
ili amtoea mama Juliana ambaye wakati huo
alishashindwa kwa pumzi na nguvu pia.
“Mwanangu nisamehe sana , kweli kabisa
nilidhani wewe ni Bitungu, nisamehe sana
baba. ”
TAMBAA NAYO MWENYEWE …
Bwakila aliamua kusamehe na kumpa onyo
kwamba akirudia tabia ile sehemu nyingine
atajikuta akibakwa …“ Ni kweli mwanangu
maneno yako , ” alisema mama Juliana akitoka
na jasho jembamba .
Alikwenda kubisha hodi kwenye mlango
mwingine, akafungua mtu mzima f ’ lani ,
alipokutana macho na mama Juliana, mtu
mzima huyo akaanza kuachia tabasamu …
“Ni wewe ?” aliuliza yule mtu mzima fulani …
“Aliye ?” alihoji mama Juliana akidhani labda
mtu huyo yupo ni Bitungu …
“Tuliyekuwa tukiwasiliana kwenye Facebook, si
tumekubaliana kukutana hapa?”
“Akha !” mama Juliana akaondoka hapo ,
akaenda kugonga mlango chumba kingine ndiyo
akatokea Bitungu sasa.
Mama Juliana aliingia ndani na kuangukia
kitandani huku akichuruzika machozi …
“Vipi tena ?” alihoji Bitungu …“Kidogo nibakwe. ”
“Kidogo ubakwe ! Na nani ?”
Mama Juliana alisimulia kisa chote kuanzia
kuzimikiwa na simu na yaliyompata ndani ya
gesti ile .
“Duu ! Pole sana. ”“ Kiranga chote kimeniishia , ”
alisema mama Juliana huku akijifuta machozi na
kumkumbatia kijana huyo kama anayasema
‘ afadhali nijipoze na wewe sasa ’ .
Bitungu alichoshwa sana na majambozi ya
Juliana mwenyewe , sasa mama mtu kufika pale
naye akawa anataka kwa sehemu
yake. Alimchombezachombeza kijana huyo kwa
kumshikashika sehemu mbalimbali za mwili ili
kumchajisha na huku akimbembeleza kwa
maneno matamumatamu ya mahaba…
“Bitungu …”
“Naam…”
“Unajua wewe ulitakiwa uwe mume wangu ?”
“Kweli mpenzi ?”“Kweli kabisa . Wewe unadhani
nani alistahili kuwa mume wangu miye?”
“Ni mimi mpenzi . ”
“Kumbe unajijua, yaani nakupenda wewe mpaka
basi jamani, ” alisema mwanamke huyo mtu
mzima huku akiwa anashughulika na kipaza
sauti . Ilifika mahali Bitungu akachaji, kila kona
ya mwili wake ikakaa sawasawa kwa mechi ya
kirafiki isiyokuwa na refa .
“Leo nataka njia ile nyingine , ” alisema Bitungu
lakini mama Juliana akakataa …
“Mimi nataka njia ya siku zote mimi na wewe, ”
alisema mwanamke huyo huku akimfosi kijana
huyo kuanza mpambano kwa kumwingiza
mwenyewe uwanjani.
Ulikuwa mpambano wenye kumwelemea Bitungu
kwa namna yoyote ile . Alionesha uchovu wa
waziwazi mpaka mwanamke huyo
akamuuliza …“Mpenzi leo vipi , umevurugwa na
nani kabla yangu?” aliuliza mama Juliana lakini
kabla hajajibiwa , simu ya Bitungu iliita .
Kwa kuwa pozi lao la muda huo , mama Juliana
ndiye aliyekuwa upande wa stuli yenye simu,
aliichukua na kuiangalia skrini kidogo aliyepiga
huku akiipeleka kwa Bitungu . Kwenye skrini
ilionekana jina Julie …
“Ah ! Nitampigia baadaye , ” alisema Bitungu
akikata simu hiyo kisha kuizima kabisa …
“Julie ndiyo nani ?” mama Juliana aliuliza akiwa
amebadilika sura ghafla.
“Mtoto wa shangazi yangu bwana, anataka
nimtafutie kazi . ”
“Mh!”
“Mbona umeguna ?”
“Nimeguna maana na mimi nina mtoto anaitwa
Julie , ” alisema mwanamke huyo akimaanisha
kifupi cha Juliana ni Julie lakini Bitungu
akampuuza na wala hakutaka kujiongeza
kwamba pengine Julie wa mwanamke huyo ndiye
Juliana anayemjua yeye.
Aliamini Julie si Juliana akafurahi moyoni
kwamba, amemchenga mwanamke huyo kwa
kumsevu Juliana kama Julie …“ Mbalimbali, huyu
ni Julie mtoto wa shangazi yangu. Labda wewe
ndiyo uwe huyo shangazi yangu, ” alisema
Bitungu…
“Naweza kuwa , maana hata mimi Julie wangu
anatafuta kazi , ” mama Juliana alitia neno
kidogo likamwingia Bitungu kwani ni kweli
Juliana alimwambia anatafuta kazi wakati
wamekaa baa walipokutana kabla ya kwenda
gesti.
Ikumbukwe kwamba wakati wanayazungumza
hayo walikuwa wakiendelea na mechi kama
kawaida kwa kutumia njia ile ya mama Juliana
na si ya Juliana mwenyewe .
Mama Juliana ndiye aliyeanza kutangaza kupata
ushindi kwani Bitungu alikuwa mchovu kwa
wakati huo .
Ilishindikana kabisa kwa Bitungu kukamilisha
ngwe ya safari yake na hivyo kutoka uwanjani
akiwa ameshindwa kukomboa.
***
Ilikuwa siku ya pili , simu ya Juliana iko mezani
sebuleni, mama yake akiwa anapita hapo , mara
simu hiyo iliita , akaangalia kwenye skrini huku
akimwita Juliana mwenyewe …
“Simu yako inaita huku wewe … Bituu , ” alisema
mama Juliana.
Juliana alifika akiwa mbio na kuhema juu …
“Bituu anapiga . ” Juliana aliichukua simu na
kwenda mbali …
“Haloo … sijambo … niko nyumbani mbona … haya
sawa… haya. ”
Baada ya kukata simu , mama Juliana aliita…
“Juli …”
“Abee mama . ”
“Bituu ni nani?”
“Siyo Bituu mama , nilikosea kusevu tangu
mwanzo, ni Bitte. ”
“Ndiyo nani?”
“Nilisoma naye kule chuo mama . ”
“Hebu namba yake, ” alisema mama Juliana
huku akinyoosha mkono kutaka simu ya
mwanaye huyo .
Je, unajua nini kiliendelea? Usikose kusoma
chombezo hili jipya
 
ILIPOISHIA RISASI JUMATANO :
“Abee mama . ”
“Bituu ni nani?”
“Siyo Bituu mama , nilikosea kusevu tangu
mwanzo, ni Bitte. ”
“Ndiyo nani?”
“Nilisoma naye kule chuo mama . ”
“Hebu namba yake, ” alisema mama Juliana
huku akinyoosha mkono kutaka simu ya
mwanaye huyo .
SONGA NAYO MWENYEWE …
Wakati Juliana anampa mama yake simu , mkono
ukalegea, ikaanguka chini na kuvunjika kioo …
“Mama simu yangu jamani. ”
“Mbona umelegea mikono wewe, ala !” alifoka
mama mtu . Akaendelea …
“Hakijaaribika kitu , toa laini niweke kwenye
simu yangu , nataka kumjua huyo Bitte
unayemsema wewe ni nani ?”
“Kwani mama wewe umefikiria ni nani ?”
“Ndiyo nataka kumjua . ”
Moyoni Juliana akasema …
“Ungejua si Bitte ni Bitungu …”
Naye mama mtu moyoni akasema …
“Ungejua nafananisha jina hilo na la dogodogo
wangu Bitungu . ”
Juliana alitoa laini, akampa mama yake huku
simu yake ikiwa imezima baada ya kuanguka .
Naye mama mtu aliichukua laini na kuipachika
kwenye simu yake, akawasha. Yalikuja majina
mengi sana lakini jina la Bitte halikuwepo .
Maana yake ni kwamba, jina liliseviwa kwenye
simu yenyewe ‘ hand set’ , au wanasema ‘ phone
book’ .
“Hebu lete simu yako . ”
Juliana alimpa mama yake simu, akatoa laini na
kuipachika humo tena , akawaisha , simu
haikuwaka kutokana na kule kuanguka.
Akamtupia simu mtoto wake huku akisema…
“Nitataka kumjua huyo Bitte. ”
“Sawa mama . ”
***
Bitungu alishangaa kumkosa Juliana kwa siku
hiyo , kila alipompigia ilionekana simu yake
imezimwa…
“Huyu leo vipi tena ?” alijiuliza kijana huyo .
Juliana alifika kwa fundi na kueleza shida ya
simu yake, akaambiwa ni lazima ibadilishwe kioo
lakini gharama aliyotajiwa ilimshinda, akaamua
kwenda kununua simu ya tochi kwanza .
Hata hivyo, alijua hataweza kumpata Bitungu
kwa sababu namba zake ziko kwenye simu
iliyokufa kioo .
Alinunua simu, akarudi nayo nyumbani ili
kuiweka kwenye chaja kwa muda . Lakini
nyumbani hakumkuta mama yake na akashindwa
kujua aliko .
Baada ya nusu saa , Juliana alichomeka laini
kwenye simu yake ya tochi , akaiwasha . Ndani
ya dakika moja meseji kibao zikaanza kuingia
mfululizo , ikiwemo ya mama yake akimwambia
anatoka kidogo .
Ikaingia nyingine iliyomwonesha kwamba ni ya
Bitungu kwani ilisema …
“Baby mbona sikupati hewani ? Ujue unanipa
wakati mgumu sana mwenzio ?”
Juliana aliipiga simu hiyo . Wakati simu inaita,
Bitungu alikuwa amekaa na mama Juliana …
“Hebu pokea simu kwanza mpenzi wangu ndiyo
tuendelee na mambo mengine , ” alisema mama
Juliana, lakini naye Bitungu alipoona ni Juliana
aliogopa . Hata hivyo , ili kuua soo aliipokea huku
akipunguza sauti …
“We vipi mbona hupatikani kwenye simu?”
“Simu mbovu my dear, kweli tena !”
“Pole sana, mi nilikuwa sijui . ”
“Ndiyo hivyo. Uko wapi ?”
“Nipo mitaa ya Sinza Palestina , nitakutafuta
baadaye . ”
“Poa . ”
Baada ya kukata simu , mama Juliana
alishangaa kuona simu yake iikimpa mrejesho
kwamba meseji aliyotuma kwa Juliana muda
fulani ndiyo inamfikia sasa , akampigia…
“Umetengeneza simu?”
“Bado mama , pesa ni nyingi nimeamua kununua
simu ya tochi kwanza . ”
“Sawa, ilimradi simu . ”
“Uko wapi mama ?”
“Nipo maeneo ya Sinza Palestina japokuwa
sipendi kuulizwa nilipo na wewe , ” alisema
mwanamke huyo huku akimshikashika mwilini
Bitungu. Walikuwa ndani ya gesti.
Baada ya kukata simu , Juliana alijiuliza maswali
mawili ya msingi sana…
“Mama anasema yupo maeneo ya Sinza
Palestina, Bitungu naye anasema yupo mitaa ya
Sinza Palestina. Inawezekana wapo wote?
“Mmh !” aliguna baada ya kukosa jibu na
kuamua kuachana na hayo .
Muda ulivyozidi kwenda alihisi kwamba mama
yake akirudi lazima atataka kumjua Bitte kwa
maana ya kumuuliza maswali mengi. Lakini pia
aliisevu namba ya Bitungu upya, akaandika
Stella Goms , yaani Stella wa Gongo la Mboto.
***
Siku hiyo , Bitungu kwa hasira za kumkosa kwa
muda mrefu Juliana, msichana aliyempenda
sana na furaha ya kumpata baadaye , aliamua
kumchakaza mama Juliana kwa mechi kali
isiyokuwa na mfano huku akitumia njia ambayo
mama Juliana ndiyo anaitaka .
***
Mama Juliana alikuwa sebuleni kwake amechoka
sana na mechi ya Bitungu , akamwita
mwanaye …
“Abee mama . ”
“Kaa hapa. ”
Juliana alikaa sawasawa na maelekezo ya mama
yake…
“Bitte ni nani ?”
“Mama si nilikwambia nimesoma naye kule
chuo. ”
“Unaweza kumfuata ukamleta hapa?”
“Ndiyo. ”
“Mfuate haraka sana . ”
Kwa Juliana zilikuwa habari njema kwani ilikuwa
saa kumi na mbili jioni, kupewa kibali cha yeye
kutoka Ilala kwenda hadi Gongo la Mboto ni
furaha kwake . Alipanga akitoka tu akaonane na
Bitungu popote alipo .
Alijiandaa harakaharaka na kuchomoka zake…
“Haya mama nakwenda kumleta , ” alisema
Juliana akiwa na amani jambo lililomshangaza
sana mama yake.
Je, unajua nini kiliendelea? Usikose kusoma
chombezo hili jipya
 
Kkkkk mbona mnaisingizia bangi nyie waungwana?
Nalog off
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…