Duh! Kali ya mwakaNini gari, mie hiyo 15M namuhonga Sanchoka ananipa tiGo...kujenga ujanani ni ushamba na uoga wa maisha
Kweli mkuu, sometimes humu watu wanajitoa ufahamu kabisa ktk hili.Tuache unafiki, sasa hivi hela ni ngumu sana, mtu huwezi kupanga kununua gari la shilingi mil. 15 wakati hata kiwanja huna, kama utafanya hivyo basi wewe ni mjinga, suala kusema sijui mishemishe za mjini zinahitaji gari hakuna lolote, mafanikio ya mtu ni uwezo katika kujipatia mlo wa kila siku, mavazi na nyumba ya kujenga mwenyewe.
Basi labda huelewi maana nzima ya gari ya anasa.Sijaona gari ya anasa hapo mkuu
Dah safi sana kiongozi, hayo ndio nayaita maujanja mzee. Kwa hio akili gari yako haiwezi kuwa ya anasa maana inakuingizia pesa ndefu. Gari ya anasa ni ile inayokutia umaskini tu pasi na kukuzalishia pesa.Mkuu hizi gari siku hizi zinapiga hela atari...
Mm mwenyewe nilikua na mindset kama hiyo nikanunua uwanja huko madale kabla hata sijanunua gari eti nijenge kwanza...
Sasa hiv nimekiuza kiwanja nimenunua IST nime muajiri dereva kwa wiki ananiletea laki mbili nakula laki nane kwa mwezi, huu uchawi unao itwa UBER bora usikie kwa jirani ako. Kwa sasa nimeagiza honda fit ili niongeze nguvu niwe nakula 1.6m kwa mwezi sina shida na nyumba, nipo zangu Gomz chumba 45,000 kwa mwezi.
kila mtu na maisha yake...
wengine gari ndio itamuwezesha kuwai mambo yake na kumsaidia kujenga nyumba siku moja..
je nyumba utajenga kwa milion 10...
kwa shida ya usafiri wa Dar wacha tu waanze kununua magari kwa kweli, hilo gari ndilo litamrahisishia kuwai mipango ya kujenga
Kila mtu na maisha yake. Akilala njaa utamsaidia? Pesa nitafute mm halafu unipangie cha kufanya? Mind your own business
We nenda kapande mwendokasi/daladala huku ukipapasawa papaswa na vijeba.Oooooh,now I know why many of you want cars,misifa.Na wewe uonekane umo.Mbaya zaidi gari yenyewe ni ya mkopo.Aibu sana.
Kwani marejesho/makato ya huo mkopo utalipa wewe au yeye aliyekopa?Sasa mtu mwingine anakopa gari 25mil halafu anaenda kulipaki ccm.Hana hata kiwanja cha 6mil....
kila mtu na vipaumbele vyake!Tuache unafiki, sasa hivi hela ni ngumu sana, mtu huwezi kupanga kununua gari la shilingi mil. 15 wakati hata kiwanja huna, kama utafanya hivyo basi wewe ni mjinga, suala kusema sijui mishemishe za mjini zinahitaji gari hakuna lolote, mafanikio ya mtu ni uwezo katika kujipatia mlo wa kila siku, mavazi na nyumba ya kujenga mwenyewe.
Kabisa. Inategemea kipaumbele ni nini kwa wakati huo.Huwa wanashangaza!.. Ila kila MTU na mipango yake
umeongoza kwa Ban hapa jf, hongera sanaSioni tatizo lolote lile.
Kama mtu kanunua hilo gari kwa pesa zake na kama kapanga chumba au nyumba kwa pesa zake....tatizo liko wapi?
Wewe usilinganishe gari na nyumba kabisa acha kuunganisha gari na nyumba gari ni kitu kingne mkuuu, unalinganisha gari na nyumba kweli utakuwa wewe ni under 18 hivi unajua faida za gari? Hivi unajua umuhimu wa gari? Hivi unajua heshima Ya gari?WanaJF poleni na mihangaiko ya kutwa!
Wale wa mijini hasa Dsm sasaiv wapo kwenye foleni barabarani. Yote maisha.
Nimejiuliza hili swala. Maeneo mengi mjini, watu wengi wanamiliki magari licha ya kwamba wanakaa nyumba za kupanga, mfano unamkuta mtu ana mke na watoto 2 huku akiwa kapanga chumba na sebuleni huko uswazi, lakini wakati huohuo ana miliki gari ya kutembelea ya maana mathalani gari ya kuanzia TZS 10 MIL and above. Mtu huyo unakuta hata kiwanja hana. Hii tabia ipo sana hasa Dsm.
Hii kitu ni sahihi wakubwa au kujikweza na ulimbukeni tu wa maisha ya kuigana?
Wewe ndio unamawazo hasi. Unadhani gari ni starehe au la anasa tu. Hayo mawazo ya kimasikini sana. Nadhani gari huna na hutegemei kumiliki gari. Hao watu wameshajipanga kwa hilo. Umenikumbusha niliponunua tv wakati mwenye nyumba hana. Maneno yalikuwa kama hayo. Acha ujinga.WanaJF poleni na mihangaiko ya kutwa!
Wale wa mijini hasa Dsm sasaiv wapo kwenye foleni barabarani. Yote maisha.
Nimejiuliza hili swala. Maeneo mengi mjini, watu wengi wanamiliki magari licha ya kwamba wanakaa nyumba za kupanga, mfano unamkuta mtu ana mke na watoto 2 huku akiwa kapanga chumba na sebuleni huko uswazi, lakini wakati huohuo ana miliki gari ya kutembelea ya maana mathalani gari ya kuanzia TZS 10 MIL and above. Mtu huyo unakuta hata kiwanja hana. Hii tabia ipo sana hasa Dsm.
Hii kitu ni sahihi wakubwa au kujikweza na ulimbukeni tu wa maisha ya kuigana?