Ni sawa kununua gari ya TZS 15 Million huku ukiwa unaishi nyumba ya kupanga chumba na sebule?

Jua kitu kimoja tu silazima mtu kujenga kila mahala anapofanyia maisha yake .naweza kywa na nyumba kibaha nikaipangisha na mm nikaenda kupanga masaki so it is like swaping houses.
Au nina nyumba bagamoyo maisha yangu(kazi)Dar napangisha nyumba ya bmoyo napanga Dar na usafiri wangu
 
Sioni tatizo lolote lile.

Kama mtu kanunua hilo gari kwa pesa zake na kama kapanga chumba au nyumba kwa pesa zake....tatizo liko wapi?
Wahindi wanakaa kwy nyumba za NHC lakini wanasukuma mpaka magari ya Million 250. Na wana maisha mazuri kuliko wewe mwenye iyo million 15 unakimbilia kujenga. Tumia Pesa kuwekeza katika madili ya Pesa na hata kama iyo nyumba unaijenga sehemu ya bihashara apo vizuri sana
 
Wewe ndio unamawazo hasi. Unadhani gari ni starehe au la anasa tu. Hayo mawazo ya kimasikini sana. Nadhani gari huna na hutegemei kumiliki gari. Hao watu wameshajipanga kwa hilo. Umenikumbusha niliponunua tv wakati mwenye nyumba hana. Maneno yalikuwa kama hayo. Acha ujinga.
Nina ongezea hapo mkuuu huyu Jamaa nimuulize kitu hivi unajua utu wa mtu ulivyo na thamani? Hivi unajua ule msemo kuwa kizuri cha jiuza kibaya cha jitembeza? Unakuwa na marafiki 100 Kati ya hao mia mia wote watajua una gari ila watakaojua una nyumba ni labda kumi tu, Mimi nataka niheshimike ili nipate marafiki kiurahis niweze kufanikiwa mambo yangu yawe yanaenda vizuri sasa nikiwa na gari watu watajua faster Lakini nyumba lazima nitangaze maana unakuwa na nyumba hata marafiki zako wengne wa mtaa huo huo hawajawahi kuiona, pia Rafiki yangu Akiwa na gari nitamheshimu maana atanipa lift Siku nyingne naweza kumuomba nikaendea mahali au nikiwa na sherehe itatumika sasa hilo la kukimbilia nyumba siwezi kuazima nyumba yako na haiwezi kunisaidia hata kidogo

Gari kitu kingne bhana maana hata ukikutana na demu au Rafiki yako mliopoteana Siku nyingi atakuuluza vipi ile gari yako ipo? Mbona hawaulizi nyumba?
 
WanaJF poleni na mihangaiko ya kutwa!

Wale wa mijini hasa Dsm sasaiv wapo kwenye foleni barabarani. Yote maisha.

Nimejiuliza hili swala. Maeneo mengi mjini, watu wengi wanamiliki magari licha ya kwamba wanakaa nyumba za kupanga, mfano unamkuta mtu ana mke na watoto 2 huku akiwa kapanga chumba na sebuleni huko uswazi, lakini wakati huohuo ana miliki gari ya kutembelea ya maana mathalani gari ya kuanzia TZS 10 MIL and above. Mtu huyo unakuta hata kiwanja hana. Hii tabia ipo sana hasa Dsm.

Hii kitu ni sahihi wakubwa au kujikweza na ulimbukeni tu wa maisha ya kuigana?

Mimi ndugu yangu anamiliki gari ya mil 240 . Anakaa nyumba ya kupanga. Kodi $2,500. Lakini ana apartment zake

Sikuhizi gari ni basic need ya kukuingizia pesa, ikiwa tu unafanyabiashara ya inayohitaji utembelee sehemu nyingi au unaumuhimu kuwahi kazini na public transport sio rafiki kuwahi.

Mfano mimi nahitaji gari, sababu natembelea wateja karibu 10-15 kwa siku, nafanya kazi nikiwa kwenye gari zaidi ya ofisini. Kwahiyo hata nisipojenga sahizi ni sawa, maana najikusanya na gari ni kama mtaji wangu pia

Shida inakuja unapoamua kumiliki ili kujifanya au kushindana,
Usiigekuny.... Kwa tembo
 
Wewe usilinganishe gari na nyumba kabisa acha kuunganisha gari na nyumba gari ni kitu kingne mkuuu, unalinganisha gari na nyumba kweli utakuwa wewe ni under 18 hivi unajua faida za gari? Hivi unajua umuhimu wa gari? Hivi unajua heshima Ya gari?

Ukiwa na gari utarahisisha kazi zako Kwa uwepesi zaidi utaenda kazini ukiwa msafi utafika ukiwa msafi utarudi nyumbani ukiwa msafi

Utaenda kanisani na familia Kwa usalama Kwa furaha Kwa heshima mtafika mtarudi mkiwa wasafi
Utaenda kwenye shughuli za kifamilia utafika ukiwa msafi utarudi ukiwa msafi na utafika Kwa Wakati

Utatoka out na familia au mwenyewe utafika Kwa Wakati ukiwa msafi na utarud Kwa Wakati unaoutaka wewe

Sehemu zote hizo utakazoenda utaheshimika na utu wako utaheshimika na wote watakupa heshima yako

Mtu mwenye gari anaheshimika Kwa majirani Kwa marafi Kwa ndugu had kijijini kwenu unaheshimika

Mtu mwenye gari hupata madili mbali mbali madili makubwa na madogo

Mtu mwenye gari hupata mademu kiurahisi na marafiki wa kiume kiurahisi

Mtu mwenye gari hupata marafiki wenye hela mwisho huonyeshwa mbinu za kupata zaidi

Ukiwa na gari Ya 20.000.000 ukifika mahali umekwama utaenda bank utachukua milioni kumi faster utajipanga upya mtu mwenye gari ukikwama utakopa Kwa mtu faster utawekea kadi tofauti na nyumba mtu mwenye gari ukishindwa kabisa utauza gari utajipanga upya gari inauzika kiurahis kuliko nyumba

Ukiona vipi utawekea gari utapata hela utajipanga

Lakini kubwa na zaidi mtu anaemiliki gari usimchezee juu Ya Nyumba huyo ni rahis mno kuja kujenga nyumba kumbuka gari ili uimiliki lazima uwe na hela za pamoja Lakini nyumba mtu unaweza ukaanza kujenga ukiwa na milioni moja

Naomba nikuambie pia kuwa asilimia tisini na tisa wenye majumba Ya kifahari walianza kumilili gari


Hivyo usilinganishe kuanza kumiliki gari au nyumba

Nimependa mistali yako mkuu
Ni mwendo wa usafi tu mwisho utakuwa raisi wa wasafi
Hahaha
Ila kiukweli anayeogopa kununia gari kisa hana nyumba au gharama za uendeshaji gari Huyo muhoga wa maisha na hajui kutafuta pesa
 
Wahindi wanakaa kwy nyumba za NHC lakini wanasukuma mpaka magari ya Million 250. Na wana maisha mazuri kuliko wewe mwenye iyo million 15 unakimbilia kujenga. Tumia Pesa kuwekeza katika madili ya Pesa na hata kama iyo nyumba unaijenga sehemu ya bihashara apo vizuri sana

Ur very genius mkuu
Umetumia mfano hai kabisa wa mhindi asipokuelewa hapo basi tena
 
Nimependa mistali yako mkuu
Ni wa usafi tu mwisho utakuwa rahisi wa wasafi

Ila kiukweli anayeogopa kununia gari Lisa hana nyumba au gharama za uendeshaji gari Huyo muhoga wa maisha na hajui kutafuta pesa
Mkuuu hata nyumba ina garama kila Siku itabidi ufagie nje, ufyeke, ulipe umeme, ulipe maji, ulipe kodi Ya majengo, ulipe kodi Ya Ardhi uifanyie ukarabati
 
Kama ulivyosema kwanza inategemea na eneo lenyewe,kwa Dar kujenga ni gharama kuliko kununua gari ila mikoa mingine iliyobaki kujenga ni gharama ndogo kuliko kununua gari
Miji yote kujenga ni gharama kuliko kununua gari
 
Tuache unafiki, sasa hivi hela ni ngumu sana, mtu huwezi kupanga kununua gari la shilingi mil. 15 wakati hata kiwanja huna, kama utafanya hivyo basi wewe ni mjinga, suala kusema sijui mishemishe za mjini zinahitaji gari hakuna lolote, mafanikio ya mtu ni uwezo katika kujipatia mlo wa kila siku, mavazi na nyumba ya kujenga mwenyewe.
Malazi, kula na kulala ili la kulala kwenye nyumba mwenyewe ni la kwako umeongezea
 
Sasa kiwanja cha 15 mil Dar hii si mbali sana na mjini na utajikuta wachoma sana mafuta kufanya shughuli zako
Binafsi naona bora mtu apange karibu na na anunue gari

Apartments kibao mjini zimejengwa ili watu wasikae mbali na kazini

Mfano mtu anaishi Mbweni huko afu kazi Posta huyu halali usingizi mzuri na anapoteza hela nyingi sana kwenye mafuta ila tu anataka sifa nae ana kwake
Bora ukaishi nje ya mji ila kwako kuliko uishi mjini ambapo 90% ni uswazi kubayaaa sababu wanaoweza kupanga kwenye apartments si wengi, wote mnaishia manzese, tandika, kwakina Chibu halafu mnajisifu mnakaa mjini huku kipaso, sienta and the likes unakipaki CCM
 
Ni suala la mitazamo tu. Mfano kuna watu wanafikiri wakiwa na nyumba ya kuishi ni Asset, Kwa mtazamo mwingine sio kweli, Rich dad alitoa Definition ya Asset and Liability aisee nilimuelewa sana huyu jamaa, hata sasa amenibadilisha sana Fikra zangu
Iko ivi Asset= Something that gives put money in you, Liability= Something that take money from you,
Sasa ukiwa na nyumba ya kuishi, kumbuka utalipia maji, umeme, etc.
lakini Ukiwa na nyumba ya Biashara wewe unachukua hela ya kodi masuala ya maji umeme etc inamuhusu mpangaji.
Kadhalika na gari, ukiwa na Gari ya kutembelea (non_bussines car) utafanya maintenance from your own pocket sio from profit.

So Hakuna shida kununua Gari wakati huna nyumba ni suala la MTAZAMO tu. kama mtazamo wake kwenye gari uko ivyo, hamna shida mwache anunue gari, na kama nyumba basi acha ajenge tu.
Hata gari yawezakua luability
Hata nyumba yawezakua liability
Kama nyumba yako uliyojenga yaweza kua liability vip kuhusu nyumba ya kupanga?
 
utasikia "nina banda langu!!" na hapo hatanii ni banda kweli kaa la kuku mkikutana anaona aibu hata kukukaribisha huko bandani kwake maana heshima itashuka. Wajanja ana capital ya 1bn amepanga national housing maisha yanaenda we unaogopa halafu unatoa mfano wa kitoto eti milioni 15,tu?...watu wanasukuma vitu vya 40 m mbele huko na tunaishi nao humu kino wamepanga....No wonder tunaigana kuanzia ununuzi wa magari etc (Tz ya Toyota)...Ujamaa umetulemaza sana,haki!
We jifariji tu yani aweze kununua gari ya 40m halafu ukadhani hana ujenzi sehemu unaendelea
 
WanaJF poleni na mihangaiko ya kutwa!

Wale wa mijini hasa Dsm sasaiv wapo kwenye foleni barabarani. Yote maisha.

Nimejiuliza hili swala. Maeneo mengi mjini, watu wengi wanamiliki magari licha ya kwamba wanakaa nyumba za kupanga, mfano unamkuta mtu ana mke na watoto 2 huku akiwa kapanga chumba na sebuleni huko uswazi, lakini wakati huohuo ana miliki gari ya kutembelea ya maana mathalani gari ya kuanzia TZS 10 MIL and above. Mtu huyo unakuta hata kiwanja hana. Hii tabia ipo sana hasa Dsm.

Hii kitu ni sahihi wakubwa au kujikweza na ulimbukeni tu wa maisha ya kuigana?
Kuna Muhindi rafik angu ana gorofa mbili kariakoo ,ana gari tatu amepanga gorofa la NHC Pale karibu na kisutu secondary school.Mtanzania anaona kuwa na nyumba ndio kila kitu! Kuna watu wamejenga huko kimara,siju mbezi etc kwa siku mpaka afike posta mpya kazi kwake anaspendi 4500 au 10,000 kwenda na kurudi kwake! Kwa Mwezi mmoja anatumia kiasi kikubwa sana,bora angepanga Sinza akawa anawai mjini na akaokoa garama na muda,tunakufa mapema kwa kuamka saa 11 alfajiri kuwai saa mbili kazini.kirudi nyumbani ni masaa matatu njiani Dar hii hii....kulala late,jumamos na jumapili bize na vikao vya harusi....umejenga jumba kubwa,watoto wakianza secondary na chuo .nyumbani unabki na dada wa kazi na wife....mmoja wenu akiamia dodoma,jumba la 200 millions lipo tu alikusaidii kitu....maisha ni nini???
 
Ni rahisi sana kuwa na gari kuliko Nyumba, muheshimu sana mwenye nyumba narudia nyumba sio kibanda, yani mi hapa nilipofikia japo mdogo mdogo ningekuwa na kichaa cha magari ningekuwa nahesabu mac x tatu na ist moja
 
WanaJF poleni na mihangaiko ya kutwa!

Wale wa mijini hasa Dsm sasaiv wapo kwenye foleni barabarani. Yote maisha.

Nimejiuliza hili swala. Maeneo mengi mjini, watu wengi wanamiliki magari licha ya kwamba wanakaa nyumba za kupanga, mfano unamkuta mtu ana mke na watoto 2 huku akiwa kapanga chumba na sebuleni huko uswazi, lakini wakati huohuo ana miliki gari ya kutembelea ya maana mathalani gari ya kuanzia TZS 10 MIL and above. Mtu huyo unakuta hata kiwanja hana. Hii tabia ipo sana hasa Dsm.

Hii kitu ni sahihi wakubwa au kujikweza na ulimbukeni tu wa maisha ya kuigana?
Unaposema ulimbukeni inamaana kwako wewe unaona kumiliki gari ni anasa? Hivi watu wengine huwa mnawachukuliaje watu wanaomiliki gari probably mnawaona Kama ni vibopa flani Hivi.
Mleta Mada elewa kuwa gari ni chombo cha usafiri tu na sio kwamba Mtu akiwa na gari basi ameamua kujionyesha au kuringa. Huwezi jenga nyumba kwa 10 OR 15 millions.
 
14 Reactions
Reply
Back
Top Bottom