Ni sawa kununua gari ya TZS 15 Million huku ukiwa unaishi nyumba ya kupanga chumba na sebule?

Akili zilizopinda kabisa hizi.Hivi hujisikii vibaya kweli owning a car, hata kama ni Vitz au Suzuki Swift, halafu unakaa kwenye nyumba ya kupanga!? Yaani you park your car outside a house you have rented,and seriously you say you are comfortable.I don't believe it,there must be something seriously wrong with your upstairs.Nadhani tatizo ni kutafuta sifa na utukufu wa wanadamu.Utaonekanaje kwamba wewe ni mtu katika watu, bila kuwa na gari?Sifa za kijinga kabisa.
Una mawazo ya kizee sana
 
Mkuu hivi unapochukua mkopo bank wanakuambia uweke dhamana gari au nyumba?Kama huambiwi gari,basi ujue kwamba sio kitu cha maana sana,ingawa kwa akili zetu crooked tunaona ni kitu cha maana.Kwangu mimi a car is anonymous to a shirt.
Umeshasema "kwako wewe".

Sasa usitulazimishe na sisi tufuate msimamo/mtazamo wako!!!!

Wewe nunua kiwanja, jenga nyumba then panda daladala.

Mimi ninanunua gari, then nitanunua kiwanja na nitajenga.

Simple tu
 
WanaJF poleni na mihangaiko ya kutwa!

Wale wa mijini hasa Dsm sasaiv wapo kwenye foleni barabarani. Yote maisha.

Nimejiuliza hili swala. Maeneo mengi mjini, watu wengi wanamiliki magari licha ya kwamba wanakaa nyumba za kupanga, mfano unamkuta mtu ana mke na watoto 2 huku akiwa kapanga chumba na sebuleni huko uswazi, lakini wakati huohuo ana miliki gari ya kutembelea ya maana mathalani gari ya kuanzia TZS 10 MIL and above. Mtu huyo unakuta hata kiwanja hana. Hii tabia ipo sana hasa Dsm.

Hii kitu ni sahihi wakubwa au kujikweza na ulimbukeni tu wa maisha ya kuigana?

Ni maamuzi ya mtu kutegemea na kipi anakipa kipaumbele
 
Unaweza jenga kwa 15m
 
Nini gari, mie hiyo 15M namuhonga Sanchoka ananipa tiGo...kujenga ujanani ni ushamba na uoga wa maisha
 
Mleta mada bila shaka we ni wa mkoani,ingawa nyumba inaitajika sana lakini maisha ya hapa dar ni tofauti pia sana.huko mkoani 10m unajenga lakini sio dar,dar iyo ni bei ya kiwanja tu.
 
Mimi nilikuwa mpangaji tena chumba kimoja nilikwenda mgodini nikabahatisha 97 million, kutokana na umasikini uliokithir nikashauriwa kujenga nyumba yangu na wazazi wangu, lakini nikawaza baada ya ujenzi nini kitafuata? Nikapiga chini ujenzi nikaenda kuchomoa John Deer tractor na Diesel pump kubwa nikajificha polini hakika kila mwaka naingiza 120-150 milioni kwa zao la mpunga nilisha jenga mijengo ya kutosha nikafungua kituo cha kukoboa na kuuza mchele pale kuna mashine za kumenya aina ya SATAKI vijana wapo kibao wanapush life pia nimeshaongeza tractor nyingine FORD 6600 sasa kupanga ni kuchagua kwangu kujenga si hoja ila hoja ni mtaji utakaokufanya ujenge bila stress lakini kama unakimbilia kujenga halafu ukimaliza na pesa imekata huko ni kupalilia umasikini hata kama umejenga Bungallow au Mansion ni hayo tu karibuni kilosa
 
Mbona kama imekuuma sana?

Calm down. Kuna kitu kinaitwa PRIORITY.... Jifunze hilo kwanza halafu urudi kuchangia
Mkuu inaelekea hata maana ya priority hujui.Unapo-prioritize you start with the most important,the last item
in your priority list being the least important.Sasa priority list gani inayoanza na the least important.Mapya hayo.Hata sijui mmesomea shule gani ninyi watu,your minds are so skewed.Anyway Mimi nimefunga mjadala huu,tukubaliane kutokukubaliana.
 
Ubaya ni kwamba mtoa mada hakumaanisha gari ya kazi kwa alivyojipambanua. Kwa maelezo yake amelenga wale wamiliki wa gari za anasa kama brevis, mark 2 grande, mark x, premio, allion, carina, vits, passo, ist, starlet, run x, verossa n.k
Mkuu hizi gari siku hizi zinapiga hela atari...
Mm mwenyewe nilikua na mindset kama hiyo nikanunua uwanja huko madale kabla hata sijanunua gari eti nijenge kwanza...
Sasa hiv nimekiuza kiwanja nimenunua IST nime muajiri dereva kwa wiki ananiletea laki mbili nakula laki nane kwa mwezi, huu uchawi unao itwa UBER bora usikie kwa jirani ako. Kwa sasa nimeagiza honda fit ili niongeze nguvu niwe nakula 1.6m kwa mwezi sina shida na nyumba, nipo zangu Gomz chumba 45,000 kwa mwezi.
 
Mimi nilikuwa mpangaji tena chumba kimoja nilikwenda mgodini nikabahatisha 97 million, kutokana na umasikini uliokithir nikashauriwa kujenga nyumba yangu na wazazi wangu, lakini nikawaza baada ya ujenzi nini kitafuata? Nikapiga chini ujenzi nikaenda kuchomoa John Deer tractor na Diesel pump kubwa nikajificha polini hakika kila mwaka naingiza 120-150 milioni kwa zao la mpunga nilisha jenga mijengo ya kutosha nikafungua kituo cha kukoboa na kuuza mchele pale kuna mashine za kumenya aina ya SATAKI vijana wapo kibao wanapush life pia nimeshaongeza tractor nyingine FORD 6600 sasa kupanga ni kuchagua kwangu kujenga si hoja ila hoja ni mtaji utakaokufanya ujenge bila stress lakini kama unakimbilia kujenga halafu ukimaliza na pesa imekata huko ni kupalilia umasikini hata kama umejenga Bungallow au Mansion ni hayo tu karibuni kilosa
Ndicho nilichokuwa nawaambia watu hapa.Kuwa siyo lazima kuanza kujenga.Inategemea Na mipango.Maana hii formula ya kusema lazima uanze kujenga mie ni mhanga wa hii formula ndio maana naipinga.Kuna kihela nikabahatisha kujenga bahati mbaya ujenzi haukufikia mwisho.Mpaka Sasa hivi nasubiri tena miaka kadhaa nipate vihela niendeleze ligi.
Wakati rafiki yangu ye aliinvest ile hela mpaka Sasa inamzungushia mtaani inarudisha return Nzuri tu mpaka Sasa anajenga kwa Kasi nadhani atakuwa na kwake soon.Wakati mie nikiwa najichanga Mia Mia ndio nisogeze ka mjengo
 
Mkuu hizi gari siku hizi zinapiga hela atari...
Mm mwenyewe nilikua na mindset kama hiyo nikanunua uwanja huko madale kabla hata sijanunua gari eti nijenge kwanza...
Sasa hiv nimekiuza kiwanja nimenunua IST nime muajiri dereva kwa wiki ananiletea laki mbili nakula laki nane kwa mwezi, huu uchawi unao itwa UBER bora usikie kwa jirani ako. Kwa sasa nimeagiza honda fit ili niongeze nguvu niwe nakula 1.6m kwa mwezi sina shida na nyumba, nipo zangu Gomz chumba 45,000 kwa mwezi.
Hongera sana kwa maamuzi na bahati uliyoipata
Kwani kutusua Pesa hiyo nayo si mchrzo mchezo, mwanga mbinu hapa mkuu.
 
Mkuu inaelekea hata maana ya priority hujui.Unapo-prioritize you start with the most important,the last item
in your priority list being the least important.Sasa priority list gani inayoanza na the least important.Mapya hayo.Hata sijui mmesomea shule gani ninyi watu,your minds are so skewed.Anyway Mimi nimefunga mjadala huu,tukubaliane kutokukubaliana.
Gari ni least important KWAKO.

Kwangu mimi Gari ndio the MOST important KWA SASA,kwa wakati huu.

Ni kipaumbele changu, usitoke povu. Wewe kipaumbele chako ni nyumba and that is Okay.

Get on your senses bro,usilazimishe priority zako ziwe za watu wote. Wa wapi wewe?
 
Watanzania wengi kwa maoni yangu wanamatatizo makubwa mawili katika matumizi ya pesa, moja ni ulimbukeni na mbili ni kutojua vipaumbele katika maisha yetu. ... Nakupongeza uliyechokoza mada hii
 
Back
Top Bottom