Ni sawa kununua gari ya TZS 15 Million huku ukiwa unaishi nyumba ya kupanga chumba na sebule?

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,302
2,000
WanaJF poleni na mihangaiko ya kutwa!

Wale wa mijini hasa Dsm sasaiv wapo kwenye foleni barabarani. Yote maisha.

Nimejiuliza hili swala. Maeneo mengi mjini, watu wengi wanamiliki magari licha ya kwamba wanakaa nyumba za kupanga, mfano unamkuta mtu ana mke na watoto 2 huku akiwa kapanga chumba na sebuleni huko uswazi, lakini wakati huohuo ana miliki gari ya kutembelea ya maana mathalani gari ya kuanzia TZS 10 MIL and above. Mtu huyo unakuta hata kiwanja hana. Hii tabia ipo sana hasa Dsm.

Hii kitu ni sahihi wakubwa au kujikweza na ulimbukeni tu wa maisha ya kuigana?
 
tukunyemamzee

Member
Feb 20, 2014
90
125

We unadhani utajenga kwa 15M?
 
mwanawao

JF-Expert Member
Aug 18, 2010
2,289
2,000
Usiishi maisha kwa kuiga ya wengine. Ishi maisha yako unayopenda na utakayofurahia.

Kama furaha yako ipo kwenye nyumba jenga nyumba. Kama mwingine furaha yake ni kwenye magari mwache atanue na magari yake.

Usilazimishe mtu kuishi maisha yako meen
 
Nyamanoro

JF-Expert Member
Feb 11, 2011
649
1,000
Sioni tatizo lolote lile.

Kama mtu kanunua hilo gari kwa pesa zake na kama kapanga chumba au nyumba kwa pesa zake....tatizo liko wapi?

Tuache unafiki, sasa hivi hela ni ngumu sana, mtu huwezi kupanga kununua gari la shilingi mil. 15 wakati hata kiwanja huna, kama utafanya hivyo basi wewe ni mjinga, suala kusema sijui mishemishe za mjini zinahitaji gari hakuna lolote, mafanikio ya mtu ni uwezo katika kujipatia mlo wa kila siku, mavazi na nyumba ya kujenga mwenyewe.
 
mangatara

JF-Expert Member
Jul 6, 2012
14,560
2,000
Miye ningelisema hivi;
Kwanza ajiulize, ni nini kinamfanya apangishe vyumba 2 tu halaf awe na gari. Pili, gari lake ni la kustarehe au kwa ajili ya shughuli za kumletea kipato. Naomba watu tusiwe na mawazo ati kuwa na gari ni ufahari. Tuondoke huko tuseme gari ni means of life too. Unaweza kuwa na gari lako likakutajirisha pia. Unaweza kuwa na nyumba ikakufilisi pia. Kama utabaki kuirembesha kwa vitu vya hali ya juu nayo si majanga?? Chochote bila mpangilio ni majanga tu
 
Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
87,788
2,000
Tuache unafiki, sasa hivi hela ni ngumu sana, mtu huwezi kupanga kununua gari la shilingi mil. 15 wakati hata kiwanja huna, kama utafanya hivyo basi wewe ni mjinga, suala kusema sijui mishemishe za mjini zinahitaji gari hakuna lolote, mafanikio ya mtu ni uwezo katika kujipatia mlo wa kila siku, mavazi na nyumba ya kujenga mwenyewe.

Usijifanye mjuzi wa mipango ya watu.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom