Ni sahihi kusema miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania?

Lord OSAGYEFO

JF-Expert Member
Feb 19, 2021
3,086
4,881
Wadau nawasalimu nimekuwa anafuatilia matangazo ya maadhimisho ya sherehe za miaka 60 ya Uhuru kupitia TBC.

Kinachonishangaza ni watangazaji wa TBC wanatangaza kuwa tunaadhimisha miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania. Kama haitoshi kuna mc hapo uwanjani nae anatangaza kuwa ni sherehe ya Uhuru wa Tanzania Bara

Najiuliza hivi hawa TBC kwanini wanapotosha umma ? Hivi hawa watangazaji hawajui kuwa ni Tanganyika ndio ilikuwepo mwaka 1961?

Je, tarehe 9 Desemba 1961 nchi ya Tanzania ilikuwepo?

Na huyu mc anasema Uhuru wa Tanzania bara hiyo nchi ipo?

Tafadhalini tbc huo ni upotoshaji wa wazi

Miaka 60 ni ya uhuru wa nchi ya Tanganyika na wala sio Tanzania au Tanzania Bara.

1639033248127.jpg
 
Hakuna uhuru wa Tz, ni uhuru wa Tanganyika jamani. ccm mnapotosha sana wanannchi na vizazi vijavyo!
 
Back
Top Bottom