Ni sahihi kumuacha Mkeo aparangane na biashara za masafa ya Mbali?

britanicca

JF-Expert Member
May 20, 2015
15,644
30,007
Ni asubuhi nyingine, matumaini ni kuwa mmeamka salama.

Je, ni sahihi kumuacha mkeo kufanya biashara ya kusafiri kwenda mbali kufuata mzigo au bidhaa akiwa mwenyewe? Mfano, mke kusafiri kwenda mikoani kununua mazao ya nafaka na kupeleka dar ambako anamuacha mme wake. Au kusafiri kwenda Dubai ,China au Nairobi kufuata mzigo wa kuuza kama nguo, Mikoba n mitumba, akakaa siku 2 mpaka week 1.

Je, Ina madhara kwa mahusiano?

Muhimu: Jumbe nazoweka hapa si lazima ziwe zinanigusa mimi moja kwa moja bali zitasaidia wengi wanaotaka kujua baadhi ya mambo

Britannica
 
Wangari Maathai

Kimalezi ya familia inaweza kuwa shida kama mna watoto ambao bado wadogo sana. Chini ya miaka 14.
Kama unamaanisha kiuaminifu kwangu huwa nasema mtu akiamua kufanya umalaya kokote anafanya.
 
Mithali 31:10 Mke mwema, ni nani awezaye kumwona?Maana kima chake chapita kima cha marijani.
11 Moyo wa mumewe humwamini,Wala hatakosa kupata mapato.
12 Humtendea mema wala si mabaya,Siku zote za maisha yake.
13 Hutafuta sufu na kitani;Hufanya kazi yake ya mikono kwa moyo.
14 Afanana na merikebu za biashara;Huleta chakula chake kutoka mbali.
15 Tena huamka, kabla haujaisha usiku;Huwapa watu wa nyumbani mwake chakula;Na wajakazi wake sehemu zao.
16 Huangalia shamba, akalinunua;Kwa mapato ya mikono yake hupanda mizabibu.
17 Hujifunga nguvu viunoni kama mshipi;Hutia mikono yake nguvu.
18 Huona kama bidhaa yake ina faida;Taa yake haizimiki usiku.
19 Hutia mikono yake katika kusokota;Na mikono yake huishika pia.
20 Huwakunjulia maskini mikono yake;Naam, huwanyoshea wahitaji mikono yake.
21 Hawahofii theluji watu wa nyumbani mwake;Maana wote wa nyumbani mwake huvikwa nguo nyekundu.
22 Hujifanyia mazulia ya urembo;Mavazi yake ni kitani safi na urujuani.
23 Mume wake hujulikana malangoni;Aketipo pamoja na wazee wa nchi.
24 Hufanya nguo za kitani na kuziuza;Huwapa wafanya biashara mishipi.
25 Nguvu na hadhi ndiyo mavazi yake;Anaucheka wakati ujao.
26 Hufumbua kinywa chake kwa hekima,Na sheria ya wema i katika ulimi wake.
27 Huangalia sana njia za watu wa nyumbani mwake;Wala hali chakula cha uvivu.
28 Wanawe huondoka na kumwita heri;Mumewe naye humsifu, na kusema,
29 Binti za watu wengi wamefanya mema,Lakini wewe umewapita wote.
30 Upendeleo hudanganya, na uzuri ni ubatili;Bali mwanamke amchaye BWANA, ndiye atakayesifiwa.
31 Mpe mapato ya mikono yake,Na matendo yake yamsifu malangoni.
 
Unawasiwasi wa kukongewa sio, Kama ndio Basi hta asipo safiri atachezea koni tu kwa mabaharia waliopnda.

Mwache tu apalangane ugali uje mezani swala la kuchapiwa funga Kama hulijui.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom