Labda wewe ulimchagua; ninachojua mimi alitangazwa na tume ya uchaguzi hizo kura kama alipata hutakuja kuziona mahali popote.Ni sifa zipi ambazo watanzania tuliziona kwa muheshimiwa kikwete nakupelekea tukamchagua kwa kura lukuki.wanaohijua historia yake kiuongozi ebu nisaidieni.au tulimchagua kwa staili bendera ufata upepo.
Am happy sikumpigia kura, sababu sikuona chochote ndani yake.
Kama tu Membe na mvi.
me nachojua uadilifu wake aliiba ubwabwa KAMBI YA RUVU,NA AFANDE UBWABWA ALIMUONALabda wewe ulimchagua; ninachojua mimi alitangazwa na tume ya uchaguzi hizo kura kama alipata hutakuja kuziona mahali popote.
Kiuongozi hakuna kitu; maana Monduli walikataa kumpa kamisheni ya uafisa kwa saqbabu hakukidhi viwango labda ingekuwa sasa lukuvi afanye "standarsation".
Ila usisahau hii nchi ni ya amani na utulivu haturuhusiwi kuhoji cho chote.
Ni sifa zipi ambazo watanzania tuliziona kwa muheshimiwa Kikwete nakupelekea tukamchagua kwa kura lukuki wanaohijua historia yake kiuongozi ebu nisaidieni au tulimchagua kwa staili bendera ufata upepo.
nakupongeza kwa kufanya kitubio. Mwenzio mimi nilishtuka toka mapema. Kura yangu 2005 ilikwenda kwa freemana mbowe.
Yupo rafiki yake jk mmoja aitwaye remmy alikuwa mwandishi wa habari na mmoja wa watu wanaomtafutia viburudisho, remmy alipinga sana kitendo cha jk kugombea urais na alikuwa akisema siku zote kuwa jamaa hafai kuwa rais.
Sasa hivi ni marehemu, angelikuwepo nafikiri angekuwa ni mmoja wa watiu ambao wangekuwa na raha sana kuona alichokisema 2005 kimetimia.
Mnaikumbuka sera ya;
HARI MPYA, NGUVU MPYA na KASI MPYA?
Na Je, Swala la Ajira Nyingi kwa Vijana?.
Na ss, juzi tu serikali imeruhusu wananchi wa Afrika Mashariki kuja kufanya kazi ktk vyuo vya binafsi.... Kazi ipo.
Vipi, sera imekidhi haja ya Wa-Tz wengi?
Wengi walipiga kura kwa ushabiki tu bila kujua wanayemchagua ana sifa zipi na hasa za kiuongozi.
Na kwa mshangao mkubwa naona baadhi ya watanzania wanaelekea kurudia kosa hilo hilo la kuweka maisha yao rehani tena kwa miaka mingine mitano au kumi endapo Edward Lowassa atateuliwa na chama chake kugombea urais 2015. Hiyu jamaa amekua serikalini miaka nenda rudi lakini ni kitu gani ambacho amefanya ambayo inaweza kuwafanya watanzania wamuamini na kumchagua? Isije ikawa majuto kama wanavyojuta waliomchagua JK.
Naamini watanzania hawakotayari tena kupoteza muda kusubiri kuona wenzao wa mataifa mengine yakiendelea wao wakiendelea kuupa ufisadi nafasi ya kutamalaki.