Ni rekodi gani iliyompandisha chati Kikwete kiasi kile mwaka 2005? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni rekodi gani iliyompandisha chati Kikwete kiasi kile mwaka 2005?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mchapaji, May 12, 2010.

 1. Mchapaji

  Mchapaji Member

  #1
  May 12, 2010
  Joined: Mar 22, 2010
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mnaikumbuka sera ya;

  HARI MPYA, NGUVU MPYA na KASI MPYA?

  Na Je, Swala la Ajira Nyingi kwa Vijana?.​

  Na ss, juzi tu serikali imeruhusu wananchi wa Afrika Mashariki kuja kufanya kazi ktk vyuo vya binafsi.... Kazi ipo.

  Vipi, sera imekidhi haja ya Wa-Tz wengi?
   
 2. Dr. Chapa Kiuno

  Dr. Chapa Kiuno JF-Expert Member

  #2
  May 12, 2010
  Joined: Sep 11, 2009
  Messages: 445
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Ha ha ha! Machungu Moyoni....
   
 3. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #3
  May 12, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Kwa taharifa yako hata kama hizo sera hazijatekelezwa lakini Watanzania bado watawarudisha hao watu madarakani tena kwa kishindo.
  Inasikitisha sana.
   
 4. Dr. Chapa Kiuno

  Dr. Chapa Kiuno JF-Expert Member

  #4
  May 12, 2010
  Joined: Sep 11, 2009
  Messages: 445
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Ha Ha Ha...
   
 5. Gobret

  Gobret JF-Expert Member

  #5
  Sep 1, 2010
  Joined: Jun 11, 2010
  Messages: 320
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Nilishiriki Uchaguzi mkuu kwa mara ya kwanza mwaka 1995. Wakati huu nilikuwa na umri wa miaka 20 hivi. Wakati wa uchaguzi mkuu; Kwa kujiamini kabisa nilitoa kura yangu kwa NCCR-Mageuzi (Rais , Mbunge na Diwani) hali kadhalika mwaka 2000. Mwaka 2005, nilivutiwa kidogo na Kikwete wala siyo CCM. Nikampigia kura kwa kudanganyika nikidhani kuwa CCM si wale tena kuwa wamebadilika. Kumbe siyo kabisa. Hakika niliumia sana moyoni mwangu kwa kitendo cha madudu ya Kikwete.

  Mambo aliyovurunda ni mengi mno kuliko hata kufikiria kuongelea mazuri ya kufikirika. Yote haya pamoja na matusi aliyonitukana siku anajibu hoja ya TUCTA nimeyavumilia. Nimevumilia nikijua kuwa kura yangu ilichangia kuwa na kiburi na pia ushindi wa kishindo ndio unaomzuzua. Chagua langu la rais 1995 na 2000 lilishindwa lakini sikuumia moyoni kwa kuwa niliyetaka achaguliwe hakupata nafasi. Ilikuwa nia sawa kwani wananchi waliamua. Chaguo la 2005 lilifanikiwa. Mategemeo yangu yalikuwa makubwa kuwa atarekebisha nchi na mafisadi watakiona cha mtema kuni, EHEEEEEEEEE! wapi bwana, kumbe na yeye ni walewale. Hapa tunatukanwa na rais na wasaidizi wake;; kosa??????????????????.Ndugu Watz. tuamkeni, chagua MAENDELEO YAKO na Ya Watz. Usichague bora CHAMA. CCM na CHADEMA zitapita lakini sisi tutabaki kuwa Watanzania. Tutabaki na umaskini wetu. Tumchague rais mwenye kutetea haki za walioonewa, walibaguliwa, walionyanyaswa au waliokosa tumaini la kuishi. Kwa mwitikio moja tuwachague viongozi wanaotufaa. Soma sera za vyama vyao.

  CCM wanamaneno mazuri yakuelezea sera zao lakini MATENDO yao ni KANDAMIZI. Sera Za CCM ZIMECHAKACHULIWA SANA HAZIFAI HATA KIDOGO. Hazitufai sisi tulionyonywa na kukandamizwa na utawala mbovu wa CCM. Kwa KAULI NZURI, SERA NZURI, MWENENDO MZURI, UPENDO KWA WATANZANIA: TUMCHAGUE DK SLAA. UTAUSHANGAZA ULIMWENGU HUU KAMA WATZ. WATAONA NDANI YAKO NIA NJEMA ULIYONAYO KWAO. I AM PRAYING FOR YOU. MAY GOD BLESS YOU.WITO WANGU: TUMCHAGULIE DK SLAA WABUNGE NA MADIWANI WA CHADEMA. NA PALE AMBAPO CHADEMA IMEKOSA KUSIMAMISHA MTU TUCHAGUE WAPINZANI TU. (1) "Kama hutaki shinikizo la damu chagua CCM". (2) "Bora kutopiga kura kuliko kuipa kura CCM". (3) "Hakuna Amani kama haitoki Moyoni"
   
 6. Mentee

  Mentee Senior Member

  #6
  Sep 1, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 142
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Yaliyopita si ndwele. Ganga yajayo.... , bado hujachelewa kuchagua SLAA. Waelimishe ulio karibu nao kwamba wasichague Chama ila wachague MTU
   
 7. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #7
  Sep 1, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,356
  Likes Received: 3,122
  Trophy Points: 280
  Mwaka kura yako kwa nani?????????
   
 8. Gobret

  Gobret JF-Expert Member

  #8
  Sep 1, 2010
  Joined: Jun 11, 2010
  Messages: 320
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Hata wewe bobi nini sijui, unafahamu kuwa Kuipa CCM ni sawa na kupoteza haki yako ya kupiga kura. Chagua maendeleo, Chagua DK SLAA. Usichague Mbayuwayu ambaye hajui kwa nini watu wanamkejeli kwa kumwita dokta. Nenda shule usome uitwe dokta. Siyo udokta wa kupewa. Cheki mkapa naye alikuwa dokta na sasa udokta wake umestaafu. Inapendeza mtu kuitwa Prof Lipumba au Dk Slaa kwa maana ya usomi wao.GO DK SLAA
   
 9. Freetown

  Freetown JF-Expert Member

  #9
  Sep 27, 2010
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  watu wanaoambukizwa virusi vya ukimwi inatokana na kiherehere chao

  wanafunzi wanaopata mimba na wanaoambukizwa virusi vya ukimwi inatokana na kiherehere chao

  Watanzania wenye maisha duni inatokana na kiherehere chao kunichagua 2005

  Kwa kiherehere chenu nichagueni lala salama nikabidhi madaraka kwa Salma/Riz one 2015 maana hii ishakuwa ni kitu ya kifamily unabisha??? kalaghabaho.

  Mtanzania mwenye uelewa amka kumekucha, acha kuvuta shuka, basi linakuacha
   
 10. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #10
  Oct 11, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,748
  Likes Received: 416,592
  Trophy Points: 280
  Katika makosa niliyowahi kuyafanya maishani mwangu ni kumpa kura yangu JK na CCM yake mwaka 2005. Ni makosa nitakayoyajutia katika uhai wangu uliobakia na sasa nitajifariji kwa kuwanyima kura yangu JK na CCM...for taking my vote for granted.

  Makosa hayo ya mwaka 2005, niliyafanya kwa ghiliba za CCM na JK wake zifuatazo:-

  1) JK na CCM waliniahidi "ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya."

  Mimi nilifikiri ni mabadiliko ya kimfumo wa uendeshaji wa Nchi. Kwa kuwa na katiba mpya, uhuru wa vyombo vya habari na taasisi za utawala bora - viongozi wake kuteuliwa na bunge niliamini JK na CCM kwa kuyafanya haya wangelidhibiti kwa kiwango kikubwa dhuluma kwa wanyonge iliyokithiri kila mahali kupitia tanuru ya ufisadi.

  Lakini miaka 5 ya JK na CCM yake nimebaini ya kuwa ilikuwa ni ya "ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya" ya kulinda dhuluma dhidi ya raia hususani wanyonge na wala siyo kumkomboa mtanzania.

  Angalia katika historia yetu hatujawahi kughubikwa na kashfa nzito za ufisadi kama kipindi hiki cha miaka mitano iliyopita. Ungelitegemea JK na CCM yake kutuahidi kuubadilisha mfumo uliopo kwa kuwa na katiba mpya yenye kuziimarisha taasisi za umma badala ya mfumo uliopo unaotukuza watu hususani Raisi na ufisadi.

  Lakini JK na CCM yake sasa wanatuahidi "Ari zaidi, nguvu zaidi na kasi zaidi" ya kuchakachua matokeo ili waendeleze ubabe wa kulinda uozo wa mfumo uliopo wa uendeshaji Nchi. JK na CCM yake wanaahidi miundo mbinu "zaidi" bila ya kutafakari mbona pesa nyingi zimekuwa zikielekezwa huko lakini mchwa wa CCM umekuwa unazitafuna na hakuna tija yoyote ile.
  Hivyo basi, miundo mbinu zaidi haina tija kama mfumo wa kifisadi utaendelea kutamba siku zijazo na kamwe hautarekebishwa.

  2) Sababu ya pili iliyonifanya nifanye makosa ambayo nitayajutia kwa siku zote zilizobaki za uhai wangu ulitokana na upinzani kuweka wagombea dhaifu mno kama Prof. Lipumba na Bw. Mbowe. Ninamshukuru Mwenyezi Mungu, Chadema hili wameling'amua na wamejirekebisha kwa kumteua Dr. Slaa kuwa mgombea Uraisi.

  Dr. Slaa ameahidi mfumo mpya kupitia kuandika katiba mpya ndani ya miezi sita ya utawala wake na huku JK na CCM yake wanasema hakuna matatizo ya kimfumo na hata huu ufisadi ulioshamiri hauna tatizo lolote!!!!!!!!!!! GOD FORBIDS ANOTHER FIVE YEARS OF THE SAME MEDIOCRITY.......

  NINA UHAKIKA SAFARI HII SITAJUTIA KURA YANGU KUMPA DR. SLAA NA CHADEMA KWA KUNIAHIDI MPIGA KURA MFUMO MPYA WA UENDESHAJI WA NCHI HII UTAKAOFUTILIA MBALI DHALIMU ZA KIFISADI NCHINI MWETU............CHAGUA DR. SLAA..................... CHAGUA CHADEMA..........
   
 11. M

  Martinez JF-Expert Member

  #11
  Oct 14, 2010
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 518
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 60
  Kila mtu anajutia makosa kama hayo! Ujue tu kuwa JK ni msanii sana. Sasa hivi kagundua hawezi kuwadanganya wa mjini, amehamia vijijini.
   
 12. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #12
  Oct 14, 2010
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  nakupongeza kwa kufanya kitubio. Mwenzio mimi nilishtuka toka mapema. Kura yangu 2005 ilikwenda kwa freemana mbowe.

  Yupo rafiki yake jk mmoja aitwaye remmy alikuwa mwandishi wa habari na mmoja wa watu wanaomtafutia viburudisho, remmy alipinga sana kitendo cha jk kugombea urais na alikuwa akisema siku zote kuwa jamaa hafai kuwa rais.

  Sasa hivi ni marehemu, angelikuwepo nafikiri angekuwa ni mmoja wa watiu ambao wangekuwa na raha sana kuona alichokisema 2005 kimetimia
  .
   
 13. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #13
  Oct 14, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Vijijini hawadanganyiki

  Mwaka huu ni tofauti kabisa, ccm na kikwete hawatakiwi
  katika vijiji vya ndani kabisa ya Tanzania nilivyozungukia tangu mwezi August
   
 14. Xuma

  Xuma JF-Expert Member

  #14
  Oct 14, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 631
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Mimi toka mwanzo 2005 nilitaka rais awe dr. Salm A Salm iliposhndkana yeye kusimamishwa sikugpa kura kabsa.
   
 15. Kingcobra

  Kingcobra JF-Expert Member

  #15
  Feb 5, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,008
  Likes Received: 137
  Trophy Points: 160
  Wakuu,
  Kwa jinsi nchi inavyoenenda sasa, nashindwa kujizuia kuuliza maswali kadha wa kadha kuhusu uwezo na uzalendo wa Kikwete katika kuongoza nchi. Imefika wakati najiuliza kwamba hivi watanzania tulilishwa nini kiasi cha kufumbwa macho yasione waziwazi udhaifu wa huyu jamaa??? Ni jambo gani la maana alilofanya miaka ya nyuma linalodhihirisha uzalendo na uwezo wake katika kukabiliana na changamoto za uongozi wa nchi kiasi cha kumfanya kuwa kinara na kupendwa zaidi ya Mzee Salim A. Salim??? Wenye data watusaidie.
   
 16. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #16
  Feb 5, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Tupo busy na maswali yanayoikabili nchi sasa hivi baadhi yetu hatutapoteza muda kujadili mambo yaliyopita tuulize mikakati ipi itaisaidia Serikali yetu ku move na kuelekea kwenye slogan ya maisha bora kwa kila Mtanzania. Maswali kama GPA ya JK na ya mfano yako ni yakupunguza kasi watu kufikiri na kuona matatizo yanayowakabili sasa. Nadhani mambo yaliyopita yaache yapite lets look forward.
   
 17. Kingcobra

  Kingcobra JF-Expert Member

  #17
  Feb 5, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,008
  Likes Received: 137
  Trophy Points: 160
  Nakubaliana na hoja yako lakini historia inatupatia funzo zuri litakalosaidia tafakuri ya mikakati ya kujikomboa siku za usoni. Lakini historia inatusaidia pia kutorudia makosa yaliyofanywa nyuma. So, for me the question is still valid. We need to ask ourselves such questions so that in the course of answering them, we pay a way for our future. That's my opinion.
   
 18. LordJustice1

  LordJustice1 JF-Expert Member

  #18
  Feb 5, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,264
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Wewe unavyoona kuna mwelekeo wa maisha bora chini ya JK? Kama sivyo ni vema tukajiuliza ni nini kilichotuloga kumpa "kula" za kishindo mwaka 2005 ili tusije kufanya kosa kama hilo wakati mwingine! Mimi nionavyo JK alivinunua vyombo vya habari na kuweka mtandao mzito wa kumnadi! Tunaona hadi kufikia uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 vyombo vya habari vilimgeuka na mtandao ulisambaratika na kubakia yeye (JK) na familia yake tu, yaani BMW - Baba, Mama na Watoto!
   
 19. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #19
  Feb 5, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Mathalani tuseme JK halifanyi kitu chochote Taifa miaka ya nyuma lakini yeye sasa hivi sio Mwenyekiti wa chama tu bali ni Rais wa Tanzania kujua kwako uzalendo na aliyoyafanyia Tanzania kabla ya kuwa Rais hakuathiri kitu chochote kwenye madaraka aliyopewa na Katiba. Pili Hoja yako imekaa kihuni na ukosefu wa adabu kwa kiongozi wa nchi, nasema kiongozi wa nchi kwa kuwa Katiba ndio inamtambua na sote tumeambiwa tuwa heshimu viongozi (mamlaka) kwenye vitabu vya dini. Sikuelewi unapomwita Rais "huyu jamaa" kama kweli unamtendea haki au baadhi yetu humu kumdhihaki na kumwita "kilaza" sisi ni watu wazima inatupasa kuwa na hoja zenye heshima na adabu ili hata wao wakipata fursa ya kusoma basi waone yale tunayoyajadili na kuyafanyia kazi. Hivi ingekuwa wewe ndio JK halafu unaingia JF unakuta unakejeliwa na kudhihakiwa na kupostiwa picha za mwanamke mwenye sura yako will you spend your time kusoma maoni ya members wanaokushambulia kwa kejeli? hebu jiweke kwenye nafasi yake then uone kuwa utaona hawa ni wapuuzi na wenye wivu na wengi wao ni wahuni na ndio maana wanajiita "kingcobra" kwanini hawakujiita majina yao? atapata jibu kwasababu hawataki kutambulika na wengine ni watumishi wa umma!

  Kwahiyo mheshimiwa siasa sio kama wewe unavyoifikiria unaweza ukawa hujafanya lolote la maana kabla lakini ukashitukia wewe ni mtu muhimu sana kwa taifa. Naomba nikuulize swali ukilijibu vizuri then mimi na wewe leo kutwa nzima tutajuzana ya maana yaliyofanywa na JK kabla. Je Marehem Dr. Omar Ali Juma alifanya jambo gani la maana la kizalendo kabla ya kuwa Makamu wa Rais? je Dr Mohamed Shein aliemrithi Marehemu Dr Omar alikufanyia nini wewe pamoja na taifa jambo la maana kabla ya kuchukua nafasi ya Dr Omar? Unamkumbuka waziri mkuu mstaafu Mhe Fedrick Tulway Sumaye? aliifanyia nini Tanzania jambo la maana la kukumbukwa kabla hajateuliwa na Mkapa kuwa waziri mkuu? ulikuwa unamjua vipi Sumaye kabla hajawa waziri mkuu?

  Ukiwalinganisha hao niliowataja amabao hatukujua hata siku moja na si kuwa sie tu hatukujua kama watashika nyadhifa hizo hata wao hawakuota kama watakuwa na nafasi hizo kwenye siasa. Ni kwamba waliaminiwa kuwa wanaweza wakapewa nafasi kutekeleza azma za kulipeleka taifa mbele na hapo ndipo wakaanza kulitumikia Taifa na kuonekana walichokuwa nacho.

  Naomba niishie hapa.
   
 20. Dumelambegu

  Dumelambegu JF-Expert Member

  #20
  Feb 5, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,052
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Naungana na wewe. Historia inatufundisha nini tulikosea ili uchaguzi mwingine ukifika tusifanye makosa tena. Hatuwezi kupanga mikakati kama hatujatambua wapi tulikosea. Kwa mfano, watanzania wengi sasa wamebaini kwamba vyombo vya habari vingi vilinunuliwa ili kumpamba mtu ambaye hakuwa na hata chembe ya sifa ya kuwa rais wa nchi. In fact, inasemekana hata Mzee Madiba (Nelson Mandela) alishangaa aliposikia kwamba Dr. Salim A. Salim amedondoshwa na chama chake kwenye kinyang'anyiro cha urais. Inasemekana alishangaa na kuishia kusema kwamba kama Dr. Salim ameshindwa, basi Tanzania ina hazina kubwa ya viongozi!!!
   
Loading...