Ni rasmi sasa sakata la mchanga litatugharimu

Acacia taarifa yenu siyo ya kweli acheni uhuni mnetuibia sana hatuwezi kuwaamini Hata siku mmoja imejulikana imeshajulikana its time to go hakuna jinsi.

Mmekuwa mnaandika taarifa za kupotosha ionekane mnapata hasira kila mwaka na mnazalisha dhahabu ya kutosha kwa taarifa nyoka washafanya kazi humo ndani na taarifa zote ziko mezani kwa Mkuu wa nchi hatua kwa hatua.hakuna cha kujitetea hapo.

Kafungueni kesi ila Mwisho wenu umefika hatuwezi kuvumilia unyama mnaoufanya na takwimu fake kuwahadaa walimwengu.
Tumewashika pabaya
 
27 Mei 2017
ACACIA MINING PLC

TAARIFA KWA UMMA

Maelezo zaidi juu ya taarifa ya uchunguzi iliyotolewa na kamati ya kwanza ya Rais kuhusu usafirishaji wa makinikia.

Acacia inapenda kuendelea kutoa ufafanuzi kuhusu matokeo ya uchunguzi wa Kamati ya Kwanza ya Rais juu ya kusafirishwa nje kwa makinikia ya dhahabu/shaba. Matokeo hayo ya Kamati yaliwasilishwa na kukabidhiwa kwa Mh. Rais, Dr. John P. Magufuli, tarehe 24 Mei, 2017.
Tumeiomba serikali nakala ya taarifa kamili ya Kamati hiyo lakini bado hatujapatiwa, vile vile tumeomba taarifa ya kina ya utaratibu wa tafiti za sampuli uliotumiwa na Kamati. Tumetathmini matokeo yaliyowasilishwa na Kamati ambayo yamechapishwa na tunapenda kutamka yafuatayo:

• Kulingana na takwimu tulizonazo kwa zaidi ya miaka 20 – ambazo tutazitoa kwa utafiti zaidi – hazioani na matokeo yaliyowasilishwa na Kamati.

• Takwimu hizi za kihistoria zilikusanywa na kuchambuliwa na wataalam na taasisi za Tanzania na Kimataifa, huku zikitoa matokeo yanayofanana mara zote.

• Takwimu hizi ambazo ni huru na zilizohakikiwa na wataalam zimekuwa zikionesha kwamba kiwango cha dhahabu katika makinikia ni pungufu kwa moja ya kumi (1/10) ikilingalishwa na takwimu za utafiti zilizotolewa na Kamati.

• Ni dhahiri kwamba endapo matokeo yaliyochapishwa na Kamati yangetokana na takwimu sahihi, basi migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi ingekuwa inaongoza duniani kwa kuzalisha dhahabu nyingi zaidi.

• Kutokana na utofauti huu mkubwa wa kitakwimu tunaamini kunapaswa kuwepo na ukaguzi huru wa madini yaliyomo kwenye makinikia.

Tutafanya tathmini ya kina zaidi pindi tutakapopokea taarifa kamili ya Kamati. Lakini kwa sasa tunapenda kuwafahamisha yafuatayo kutokana na matokeo ya Kamati:
Kiwango cha dhahabu katika makinikia

Takwimu za uhakika ambazo Acacia inazo zinaonesha kwamba makontena 277 yaliyopo bandari ya Dar es Salaam yana jumla ya ujazo wa wakia 26,000 za dhahabu. Kila kontena lina wastani wa kilo 3 (kama wakia 100) za dhahabu, kilo 3 za madini ya fedha, na kilo 3,000 za madini ya shaba. Matokeo ya Kamati yalionesha kwamba kiwango cha dhahabu katika makontena yote, ambacho ni cha mwezi mmoja tu wa uzalishaji, kilikuwa jumla ya tani 7.8 (au wakia 250,000). Lakini uhalisia ni kwamba mwaka 2016 Acacia ilizalisha na kuuza wakia 250,000 za dhahabu katika makinikia kutoka migodi hii miwili kwa kipindi chote cha mwaka.

2
Kwa mantiki hii, matokeo ya utafiti wa Kamati yanamaanisha kwamba migodi miwili tu ya Bulyanhulu na Buzwagi kila mmoja huzalisha zaidi ya wakia milioni 1.5 za dhahabu kila mwaka. Hii inamaanisha kwamba migodi hii inazalisha dhahabu nyingi kuliko mingine yote duniani; kwamba Acacia ni mzalishaji wa tatu kwa ukubwa kidunia na kwamba Acacia huzalisha dhahabu nyingi zaidi kutoka katika migodi yake mitatu pekee kuliko kiasi ambacho kinazalishwa na Kampuni ya AngloGold Ashanti yenye migodi 19, Goldcorp yenye migodi 11, na Kinross yenye migodi 9.

Uzalishaji wa dhahabu unaotangazwa:
Kampuni ya Acacia inaweka wazi na kutangaza kiwango chote cha dhahabu na mapato ambayo yanawiana kikamilifu na wakia za dhahabu na madini ya fedha na tani za madini ya shaba ambazo Acacia huzalisha, kuuza na kutangaza. Taarifa za uzalishaji na mapato pamoja na takwimu zote hukaguliwa kikamilifu, na zimekuwa zikionesha kwamba Acacia haifaidiki kutokana na dhahabu ya ziada (ile iliyo mara 10 zaidi) ambayo matokeo ya Kamati yanasema Acacia haikutangaza.

Mirahaba kutoka kwenye madini mengine:
Chini ya sheria za Tanzania na makubaliano yetu na serikali, tunalipa asilimia 4 (%) ya mirahaba ya dhahabu, madini ya fedha pamoja na shaba yaliyomo kwenye makinikia. Siku zote Acacia imelipa mirahaba kwa serikali na kuna ushahidi wa kutosha wa ukaguzi ili kuthibitisha jambo hili. Na japokuwa kuna aina nyingine za madini katika makinikia, ikiwemo chuma, sulphur, rhodium na mengineyo, madini haya hayana kiwango kinachofaa kibiashara na hivyo Acacia haipokei mapato kutokana nayo na hivyo hakuna mrabaha unaolipwa.

Historia ya uzalishaji na mapato:
Acacia ni kampuni ilioorodheshwa katika soko la hisa yenye mamia ya wanahisa, taarifa zetu za fedha, uzalishaji na akiba ya dhahabu ardhini hukaguliwa kwa viwango vya kimataifa na wakaguzi wengi walio huru, na tunawajibika kukidhi vigezo vya taasisi za ukaguzi na udhibiti za Tanzania, Uingereza, Canada, na Marekani. Taasisi hizi za udhibiti za kimataifa ni huru na hutekeleza majukumu yake kwa umakini mkubwa, na zinaweza kutoza faini kubwa sana kwa makampuni yasiyotoa taarifa za uzalishaji na mapato kwa usahihi. Hivyo basi, haiwezekani Acacia itoe taarifa za chini ya kiwango kuhusu akiba yake ya dhahabu, uzalishaji na mapato husika hata kwa kipindi kifupi cha muda, achilia mbali ndani ya kipindi cha miaka mingi. Tunashindwa kuelewa ni kwa jinsi gani Kamati iliweza kupata matokeo iliyoyapata bila hata ya kuzishirikisha taasisi hizi huru za ukaguzi na udhibiti.

3
Kama matokeo ya utafiti wa Kamati yangekuwa sahihi, na Buzwagi ingekuwa inazalisha na kuuza mara kumi zaidi ya dhahabu zaidi ya inayotangaza, Acacia ingeongeza shughuli za uchimbaji Buzwagi kwa miaka mingi. Ukweli ni kwamba Buzwagi ni mgodi wenye daraja la chini la dhahabu na dhahabu yenye faida kibiashara inaelekea kuisha .
Usahihi wa vipimo kihistoria:

Tangu mwaka 1977, zaidi ya sampuli 215,000 zimechukuliwa na timu za wataalam wa kijiolojia wa Tanzania kutoka katika mgodi wa Bulyanhulu peke yake na makampuni mengi tofauti ya utafiti na uchimbaji na kufanya uchunguzi wa kina na kuthibitisha kwa kufanya vipimo katika maabara nchini Tanzania na nje ya nchi. Hakuna matokeo yoyote kati ya hayo yaliyofanywa ambayo yanafanana na matokeo yaliyowasilishwa na Kamati ya Rais ambayo kamati ilikusanya sampuli kutoka kwenye makontena kama 44 kati ya makontena 277 ya makinikia yaliyopo bandarini.
Endapo matokeo ya Kamati ya Rais ni sahihi, maana yake ni kwamba makampuni mengi, timu za wanajiolojia na maabara za uchunguzi zilizohusika na mgodi wa Bulyanhulu tangu mwaka 1977 pamoja na ule wa Buzwagi tangu miaka ya 1990 yameshindwa kufanya tafiti za sampuli kwa usahihi, ikiwemo kuzifanyia uchunguzi na kutoa taarifa sahihi juu ya kiwango cha ubora wa dhahabu kilichopo ardhini, na uzalishaji wa dhahabu/shaba/fedha katika vipindi hivi.

Isingewezekana kwa makampuni haya yanayofanyiwa ukaguzi kutoa taarifa za chini ya kiwango kuhusu akiba ya dhahabu na uzalishaji kwa kiwango kikubwa namna hii hata kwa kipindi kifupi tu cha muda, achilia mbali kipindi cha miaka mingi.

Kwa kuhitimisha, tunashindwa kuyaelewa matokeo ya uchunguzi ya Kamati ya Rais na tunaamini kwamba yanatofautiana kwa kiasi kikubwa na takwimu zilizofanyiwa uchunguzi kipindi cha nyuma. Tumekuwa tukilipa mirahaba yote kama itupasavyo kwa madini husika tunayoyazalisha. Usafirishaji wetu wa makinikia nje ya nchi hufanyika kwa kuzingatia kikamilifu sheria za Tanzania na makubaliano ya kisheria ambayo tunayo na serikali ya Tanzania. Katika migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi, jumla ya athari ya moja kwa moja ya zuio la usafirishaji wa makinikia nje ya nchi ni wastani wa hasara ya mapato kwa siku, inayozidi dola za Kimarekani milioni moja (sawa na angalau shilingi bilioni mbili za Tanzania). Kwa hali hii, tunatathimini kila tuwezalo kufanya.
Kwa taarifa zaidi wasiliana na:
Acacia Mining plc
+44 (0)207 129 7150
Giles Blackham, Meneja Uhusiano – Uwekezaji
Nilifikiri umeleta Data zako,kulingana na kichwa cha habari ulivyoandika.Kumbe ni taarifa ya mtuhumiwa,unaiaminije?.
 
HII KITU ILITOKEA MALAYSIA, waliamua ku revoke contract zote za government kwenye minerals ilizo weka na investors! NAONA NA SISI TUIGE HUO MFANO! MAULANA MOLA WETU ATUONGOZE MILELE YOTE!
Hiki ñdicho tulitegemea kifanywe. Ccm wanaogopa nini ku revoke mikatàba yote ilihali waliifanya wao? Kwani Rais hajui alichokuwa anakifanya huko nyuma na wenzake?
 
ACACIA na Deo Mwanyika wao wafungue kesi waache kututisha.Hayo maelezo wakayatoe mahakamani. Kibaya zaidi huyu Deo Mwanyika ni mwanachama wa CCM na alitaka kugombea ubunge jimbo la Njombe kusini mwaka 2015.Alimwaga pesa sana.Lakini dakika za mwisho akagaili.Kikulacho kinguoni mwako.

Kwa hiyo ulitaka yeye kama Deo Mwanyika afanye nini????
 
Hiki ñdicho tulitegemea kifanywe. Ccm wanaogopa nini ku revoke mikatàba yote ilihali waliifanya wao? Kwani Rais hajui alichokuwa anakifanya huko nyuma na wenzake?

Mkuu, tunaishi katika karne ya 21. Hata wao wanajua. You cannot willingly sign a contract and then revoke it......
 
CCM imeifikisha hii nchi pabaya sana sana sana! ni bora ikafunguliwa kesi mahakama ya kimataifa kuishtaki fisiem kwa mikataba mibovu, wizi, ufisadi, uchonganishi, gilba na uchochezi.
 
kwani hyo mikataba tuliyosaini inaruhusu hawa wawekezaji wasitangaze the true value ya contents na financials zake zilizokuwepo katika michanga? Mbona kama vile mnaisemea mikataba msi wai kuiona ata siku moja wazee
Mkuu, nani amekwambia hawakuwa wanatangaza? umesoma kwa makini taarifa hiyo juu? Hata TMAA kazi yao ilikuwa ni kuhakiki kitu hicho hicho unachosema true value. Tuache kusema uongo, hautatusaidia.
 
Hakuna mwenye clip inayoonyesha bunge wakati wa upitishaji wa ile Sheria ya madini mwaka ule? Itasaidia sana kuwafundisha watu fulani humu.....
 
Ni heri tupiganie chetu kwa gharama, kuna siku hata wewe utajitambua! Umaskini wa mawazo ulionao, utakupotea ukiwa radhi!!

Tatizo hamjui/hatujui hata "chenu" ni kiasi gani!!

Matatizo yetu sio mchanga (hiyo ni sehemu ndogo), matatizo yetu ni kwenye Sheria za Madini na Mikataba.

Sote ni Watanzania, tunaipenda nchi yetu lakini lazima tuwe smart kwenye kuingia mikataba, kuitekeleza na kuisimamia; na hapo ndipo CCM kwa miaka walituingiza matatizoni kama Taifa vs Wawekezaji.

Sasa tukitumia kiwango cha akili ile ile na hisia na manguvu kujikwamua tutakwama tu.

Kwa hali iliyvo tunaomba soft copy ya uchunguzi na ripoti iliyowakilishwa kwa Mh Rais wiki iliyopita.
 
27 Mei 2017
ACACIA MINING PLC

TAARIFA KWA UMMA

Maelezo zaidi juu ya taarifa ya uchunguzi iliyotolewa na kamati ya kwanza ya Rais kuhusu usafirishaji wa makinikia.

Acacia inapenda kuendelea kutoa ufafanuzi kuhusu matokeo ya uchunguzi wa Kamati ya Kwanza ya Rais juu ya kusafirishwa nje kwa makinikia ya dhahabu/shaba. Matokeo hayo ya Kamati yaliwasilishwa na kukabidhiwa kwa Mh. Rais, Dr. John P. Magufuli, tarehe 24 Mei, 2017.
Tumeiomba serikali nakala ya taarifa kamili ya Kamati hiyo lakini bado hatujapatiwa, vile vile tumeomba taarifa ya kina ya utaratibu wa tafiti za sampuli uliotumiwa na Kamati. Tumetathmini matokeo yaliyowasilishwa na Kamati ambayo yamechapishwa na tunapenda kutamka yafuatayo:

• Kulingana na takwimu tulizonazo kwa zaidi ya miaka 20 – ambazo tutazitoa kwa utafiti zaidi – hazioani na matokeo yaliyowasilishwa na Kamati.

• Takwimu hizi za kihistoria zilikusanywa na kuchambuliwa na wataalam na taasisi za Tanzania na Kimataifa, huku zikitoa matokeo yanayofanana mara zote.

• Takwimu hizi ambazo ni huru na zilizohakikiwa na wataalam zimekuwa zikionesha kwamba kiwango cha dhahabu katika makinikia ni pungufu kwa moja ya kumi (1/10) ikilingalishwa na takwimu za utafiti zilizotolewa na Kamati.

• Ni dhahiri kwamba endapo matokeo yaliyochapishwa na Kamati yangetokana na takwimu sahihi, basi migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi ingekuwa inaongoza duniani kwa kuzalisha dhahabu nyingi zaidi.

• Kutokana na utofauti huu mkubwa wa kitakwimu tunaamini kunapaswa kuwepo na ukaguzi huru wa madini yaliyomo kwenye makinikia.

Tutafanya tathmini ya kina zaidi pindi tutakapopokea taarifa kamili ya Kamati. Lakini kwa sasa tunapenda kuwafahamisha yafuatayo kutokana na matokeo ya Kamati:
Kiwango cha dhahabu katika makinikia

Takwimu za uhakika ambazo Acacia inazo zinaonesha kwamba makontena 277 yaliyopo bandari ya Dar es Salaam yana jumla ya ujazo wa wakia 26,000 za dhahabu. Kila kontena lina wastani wa kilo 3 (kama wakia 100) za dhahabu, kilo 3 za madini ya fedha, na kilo 3,000 za madini ya shaba. Matokeo ya Kamati yalionesha kwamba kiwango cha dhahabu katika makontena yote, ambacho ni cha mwezi mmoja tu wa uzalishaji, kilikuwa jumla ya tani 7.8 (au wakia 250,000). Lakini uhalisia ni kwamba mwaka 2016 Acacia ilizalisha na kuuza wakia 250,000 za dhahabu katika makinikia kutoka migodi hii miwili kwa kipindi chote cha mwaka.

2
Kwa mantiki hii, matokeo ya utafiti wa Kamati yanamaanisha kwamba migodi miwili tu ya Bulyanhulu na Buzwagi kila mmoja huzalisha zaidi ya wakia milioni 1.5 za dhahabu kila mwaka. Hii inamaanisha kwamba migodi hii inazalisha dhahabu nyingi kuliko mingine yote duniani; kwamba Acacia ni mzalishaji wa tatu kwa ukubwa kidunia na kwamba Acacia huzalisha dhahabu nyingi zaidi kutoka katika migodi yake mitatu pekee kuliko kiasi ambacho kinazalishwa na Kampuni ya AngloGold Ashanti yenye migodi 19, Goldcorp yenye migodi 11, na Kinross yenye migodi 9.

Uzalishaji wa dhahabu unaotangazwa:
Kampuni ya Acacia inaweka wazi na kutangaza kiwango chote cha dhahabu na mapato ambayo yanawiana kikamilifu na wakia za dhahabu na madini ya fedha na tani za madini ya shaba ambazo Acacia huzalisha, kuuza na kutangaza. Taarifa za uzalishaji na mapato pamoja na takwimu zote hukaguliwa kikamilifu, na zimekuwa zikionesha kwamba Acacia haifaidiki kutokana na dhahabu ya ziada (ile iliyo mara 10 zaidi) ambayo matokeo ya Kamati yanasema Acacia haikutangaza.

Mirahaba kutoka kwenye madini mengine:
Chini ya sheria za Tanzania na makubaliano yetu na serikali, tunalipa asilimia 4 (%) ya mirahaba ya dhahabu, madini ya fedha pamoja na shaba yaliyomo kwenye makinikia. Siku zote Acacia imelipa mirahaba kwa serikali na kuna ushahidi wa kutosha wa ukaguzi ili kuthibitisha jambo hili. Na japokuwa kuna aina nyingine za madini katika makinikia, ikiwemo chuma, sulphur, rhodium na mengineyo, madini haya hayana kiwango kinachofaa kibiashara na hivyo Acacia haipokei mapato kutokana nayo na hivyo hakuna mrabaha unaolipwa.

Historia ya uzalishaji na mapato:
Acacia ni kampuni ilioorodheshwa katika soko la hisa yenye mamia ya wanahisa, taarifa zetu za fedha, uzalishaji na akiba ya dhahabu ardhini hukaguliwa kwa viwango vya kimataifa na wakaguzi wengi walio huru, na tunawajibika kukidhi vigezo vya taasisi za ukaguzi na udhibiti za Tanzania, Uingereza, Canada, na Marekani. Taasisi hizi za udhibiti za kimataifa ni huru na hutekeleza majukumu yake kwa umakini mkubwa, na zinaweza kutoza faini kubwa sana kwa makampuni yasiyotoa taarifa za uzalishaji na mapato kwa usahihi. Hivyo basi, haiwezekani Acacia itoe taarifa za chini ya kiwango kuhusu akiba yake ya dhahabu, uzalishaji na mapato husika hata kwa kipindi kifupi cha muda, achilia mbali ndani ya kipindi cha miaka mingi. Tunashindwa kuelewa ni kwa jinsi gani Kamati iliweza kupata matokeo iliyoyapata bila hata ya kuzishirikisha taasisi hizi huru za ukaguzi na udhibiti.

3
Kama matokeo ya utafiti wa Kamati yangekuwa sahihi, na Buzwagi ingekuwa inazalisha na kuuza mara kumi zaidi ya dhahabu zaidi ya inayotangaza, Acacia ingeongeza shughuli za uchimbaji Buzwagi kwa miaka mingi. Ukweli ni kwamba Buzwagi ni mgodi wenye daraja la chini la dhahabu na dhahabu yenye faida kibiashara inaelekea kuisha .
Usahihi wa vipimo kihistoria:

Tangu mwaka 1977, zaidi ya sampuli 215,000 zimechukuliwa na timu za wataalam wa kijiolojia wa Tanzania kutoka katika mgodi wa Bulyanhulu peke yake na makampuni mengi tofauti ya utafiti na uchimbaji na kufanya uchunguzi wa kina na kuthibitisha kwa kufanya vipimo katika maabara nchini Tanzania na nje ya nchi. Hakuna matokeo yoyote kati ya hayo yaliyofanywa ambayo yanafanana na matokeo yaliyowasilishwa na Kamati ya Rais ambayo kamati ilikusanya sampuli kutoka kwenye makontena kama 44 kati ya makontena 277 ya makinikia yaliyopo bandarini.
Endapo matokeo ya Kamati ya Rais ni sahihi, maana yake ni kwamba makampuni mengi, timu za wanajiolojia na maabara za uchunguzi zilizohusika na mgodi wa Bulyanhulu tangu mwaka 1977 pamoja na ule wa Buzwagi tangu miaka ya 1990 yameshindwa kufanya tafiti za sampuli kwa usahihi, ikiwemo kuzifanyia uchunguzi na kutoa taarifa sahihi juu ya kiwango cha ubora wa dhahabu kilichopo ardhini, na uzalishaji wa dhahabu/shaba/fedha katika vipindi hivi.

Isingewezekana kwa makampuni haya yanayofanyiwa ukaguzi kutoa taarifa za chini ya kiwango kuhusu akiba ya dhahabu na uzalishaji kwa kiwango kikubwa namna hii hata kwa kipindi kifupi tu cha muda, achilia mbali kipindi cha miaka mingi.

Kwa kuhitimisha, tunashindwa kuyaelewa matokeo ya uchunguzi ya Kamati ya Rais na tunaamini kwamba yanatofautiana kwa kiasi kikubwa na takwimu zilizofanyiwa uchunguzi kipindi cha nyuma. Tumekuwa tukilipa mirahaba yote kama itupasavyo kwa madini husika tunayoyazalisha. Usafirishaji wetu wa makinikia nje ya nchi hufanyika kwa kuzingatia kikamilifu sheria za Tanzania na makubaliano ya kisheria ambayo tunayo na serikali ya Tanzania. Katika migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi, jumla ya athari ya moja kwa moja ya zuio la usafirishaji wa makinikia nje ya nchi ni wastani wa hasara ya mapato kwa siku, inayozidi dola za Kimarekani milioni moja (sawa na angalau shilingi bilioni mbili za Tanzania). Kwa hali hii, tunatathimini kila tuwezalo kufanya.
Kwa taarifa zaidi wasiliana na:
Acacia Mining plc
+44 (0)207 129 7150
Giles Blackham, Meneja Uhusiano – Uwekezaji
Hakuna kitu ulichoandika, umepoteza mda mwingi kupost utumbo. Sikiliza clip ya Gwajima ndipo utajiona nyanya kabisa.
 
Hiki ñdicho tulitegemea kifanywe. Ccm wanaogopa nini ku revoke mikatàba yote ilihali waliifanya wao? Kwani Rais hajui alichokuwa anakifanya huko nyuma na wenzake?
Nina imani kuwa hicho ndicho kitakacho fuata! Na ninaamini ndivyo atakavyo fanya.., maana Rais wetu ana ma confidence ya hali ya juu ndiyo maana mpaka sasa hajaenda huko kwao kuwaramba miguu kama watu wengine waliopita! Nazidi kumwombea kwa Mwenye Enzi Mungu ampe ujasiri yeye na serikali ya awamu ya 5 atupe hekima na busara!
 
Acacia taarifa yenu siyo ya kweli acheni uhuni mnetuibia sana hatuwezi kuwaamini Hata siku mmoja imejulikana imeshajulikana its time to go hakuna jinsi.

Mmekuwa mnaandika taarifa za kupotosha ionekane mnapata hasira kila mwaka na mnazalisha dhahabu ya kutosha kwa taarifa nyoka washafanya kazi humo ndani na taarifa zote ziko mezani kwa Mkuu wa nchi hatua kwa hatua.hakuna cha kujitetea hapo.

Kafungueni kesi ila Mwisho wenu umefika hatuwezi kuvumilia unyama mnaoufanya na takwimu fake kuwahadaa walimwengu.

Tunakuomba urejee tena humu mambo yakishaharibika kama kule kwenye sakata la samaki. Tatizo hapa si Acacia bali ni mikataba mibovu ambayo serikali ya CCM iliingia na wawekezaji. Mbaya zaidi mikataba hii inafanywa siri hata kwa wabunge!
 
Mimi nachoona hapa ni kwambs Acacia wanaitonya na kuitahadharisha serikali kuhusu mapungufu ya ile ripoti. Na kuwashtua tu kwamba wakienda mahakamani serikali itsshindwa ssubuhi tu! Wanatoa tu mifano michache ya kuonesha u hovyo wa ile ripoti! Lakini serikali ikiamua juendelea kuwa kichwa ngumu nahisi kesi ikienda mahakamani tutalipa fidia itakayoadhiri mpaka wajukuu zetu. Ikumbukwe wanadai kwamba kushikilia yale makontena ya mchanga kwa siku tu wanapata hasara ya 2 bil Tshs! Tunaiomba serikali iwe makini. Tukija kulipishwa mafaini kwa uzembe, itabidi rais awajibike! Ndio maana tunasisitiza umskini na weledi vitawale si kutafuta kiki za kisiasa!
 
Back
Top Bottom