Ni rasmi sasa sakata la mchanga litatugharimu

Ni heri tupiganie chetu kwa gharama, kuna siku hata wewe utajitambua! Umaskini wa mawazo ulionao, utakupotea ukiwa radhi!!
Mpiganie nini wanafiki na wezi wakubwa nyie, wakati mnapitisha sheria usiku na bila akidi kutimia huku mkinanga wapinzani kutoka nje ya bunge kutokana na sheria hizo kuwa za kinyonyaji hamkuwa na Akili timamu za kupigania taifa?!! Lissu, Mnyika na hata Zitto kuadhibiwa na bunge sababu ya kupigania mikataba na sheria za madini ziwe na usawa mlikuwa mnashangilia na kuwazomea. Wapuuzi wakubwa nyie ingekuwa China mngenyongwa nyote na viongozi wenu wa kijani....pumbavu kabisa
 
Kipindi kile mambo yalikua yanafata kanuni na weredi sio kwa kukurupuka!!
Kwani kulikuwa na .com? Acha kumwogopa jambazi anaye kuibia nyumbani kwako!
Kipindi hicho tulikuwa tunaimba mashuleni:
MCHAKAMCHAKA CHINJA MAKABURU YOTE CHINJA!
Haki ya Mola hakuna kitu kizuri kama kuwa nama confidence!
Tulikuwa kama Daudi na Goliati..afanalek!
 
Acacia taarifa yenu siyo ya kweli acheni uhuni mnetuibia sana hatuwezi kuwaamini Hata siku mmoja imejulikana imeshajulikana its time to go hakuna jinsi.

Mmekuwa mnaandika taarifa za kupotosha ionekane mnapata hasira kila mwaka na mnazalisha dhahabu ya kutosha kwa taarifa nyoka washafanya kazi humo ndani na taarifa zote ziko mezani kwa Mkuu wa nchi hatua kwa hatua.hakuna cha kujitetea hapo.

Kafungueni kesi ila Mwisho wenu umefika hatuwezi kuvumilia unyama mnaoufanya na takwimu fake kuwahadaa walimwengu.
Ujinga mnao nyie mliosaini mikataba na sheria usiku wa manane kwa mbwembwe na kupongezana, leo mnawaona wezi kwa lipi hasa! Wezi ni ninyi
 
Dah! !?what a dumb nation like this? ? Rais anapigania mikataba ya madini ikae sawa watu eti wanamsikilizia ajikwae? ?tuwe na huruma kwa vizazi vyetu vijavyo guys we are too much selfish
Siyo anapigania Bali anahadaa umma tu, huyu pamoja na wana ccm wenzie ndio walioshiriki kuipitisha mikataba ya kinyonyaji na hana hata rekodi ya kuipinga hii mikataba, kaangalie Hansard za bunge kwa miaka yote 20 aliyokuwa mbunge kama utaona anapinga zaidi ya kuunga mkono, kichwa na miguu mia kwa mia. Akina Lissu wametukanwa, wamezomewa, wametiwa korokoroni kwa kutetea mikataba na sheria yenye usawa kati ya mwekezaji na mzawa
 
kwani hyo mikataba tuliyosaini inaruhusu hawa wawekezaji wasitangaze the true value ya contents na financials zake zilizokuwepo katika michanga? Mbona kama vile mnaisemea mikataba msi wai kuiona ata siku moja wazee
 
ACACIA na Deo Mwanyika wao wafungue kesi waache kututisha.Hayo maelezo wakayatoe mahakamani. Kibaya zaidi huyu Deo Mwanyika ni mwanachama wa CCM na alitaka kugombea ubunge jimbo la Njombe kusini mwaka 2015.Alimwaga pesa sana.Lakini dakika za mwisho akagaili.Kikulacho kinguoni mwako.
Sasa mbona mnakataa kuwapa nakala ya report ili iwe kama reference muhimu kwenye kufungua kesi ,
 
NIMEIOKOTA SEHEMU: Kuna sababu za msingi hapa serikali ishaurike! Huyu ameshauri hivi:

Huenda uchunguzi wa madini ndani ya mchanga ukaishia kuwa swala la JPM kutafuta sifa tu na usiwe na manufaa kwa umma kwa sababu zifuatazo:

1. Acacia kama ilivyo migodi mingine Tanzania ni mali ya wawekezaji na siyo mali ya serikali maana stahili ya serikali ni asilimia 4 tu ya thamani ya madini yanayochimbwa. Serikali kufungua container za acacia na kuchukua sampuli bila kuwashirikisha acacia ni kosa.

2. Sampuli za mchanga zilizochukuliwa na kaati ya rais zimepimwa kwenye maabara bila uwakilishi wa acacia na ni kosa maana tayari acacia wamesema hawatambui huo uchunguzi na kwa hivyo serikali haiwezi kutumia matokeo ya ripoti hiyo kudai fidia mahali po pote.

3. Mikataba kama huo wa acacia inapotokea kutoelewana mahali pa kutafuta suluhu ni mahakama ya kimataifa ya usuluhishi na mahakama hiyo pia haitatambua matokeo kwenye ripoti ya kamati ya rais. Mahakama utatumia ripoti ya SGS maana inatambulika kimataifa au serikali ikikataa ripoti ya SGS mahakama itateua chombo kingine huru cha kimataifa kurudia uchunguzi wa mchanga kwenye container. Kama vipimo vya kiasi cha madini kwenye mchanga kitafanana na zile za SGS basi serikali ya Tanzania itabwagwa chini na acacia na kutakiwa kulipa gharama za kufidia kwa acacia.

4. Kuna uwezekano pia acacia wakasema mchanga kwenye container siyo wa kwao maana serikali imefungua container bila wao kuwepo na kupelekea uwezekano wa mchanga wao kutolewa na serikali kuweka mchanga mwingine.

5. Kwenye sakata hili uwezekano mkubwa ni serikali kupoteza na siyo kupata. Mikataba ya kimataifa inahitaji weledi na wala siyo mihemko ya kisiasa na ubabe wa serikali.

Mkinga mkinga
 
Sasa mbona mnakataa kuwapa nakala ya report ili iwe kama reference muhimu kwenye kufungua kesi ,

Wasubiri wana haraka gani? Watakabidhiwa report zote mbili kwa pamoja ili wapate reference za kutosha kufungulia kesi yao. Kinacho tushangaza wengi kwa nini wanahangaika kama kuku anayetafuta sehemu ya kutagia?
[HASHTAG]#Ramadan[/HASHTAG] karim.

Na washawasha!
 
Hivi Waliosaini Nchi kupata 4% ya mrahaba kwanini tusiwanyonge????

Hivi kweli watanzania tunashindwa kuona kuwa hili ni tatizo letu wenyewe Na sio hao accasia ??!!!!

Kweli asilimia 4%????????

Na hawa waliosaini wapo hai... Mchawi wetu sio wawekezaji, sisi ndio wachawi wa maendeleo yetu ... Kama mlikubaliana na mkasaini mkataba kuwa asilimia 4% ya mrahaba kwenye mauzo itahusu madini ya aina tatu tu!!!!!

Leo mnapima mnakuta kwenye makontena kuna sulphur n.k mnaanza kulia.....

Mh Raisi naomba tufanye maamuzi magumu waliotufikisha hapa wengi wapo hai pleaaaaaaaaase ni kuwapoteza tu
 
Siyo anapigania Bali anahadaa umma tu, huyu pamoja na wana ccm wenzie ndio walioshiriki kuipitisha mikataba ya kinyonyaji na hana hata rekodi ya kuipinga hii mikataba, kaangalie Hansard za bunge kwa miaka yote 20 aliyokuwa mbunge kama utaona anapinga zaidi ya kuunga mkono, kichwa na miguu mia kwa mia. Akina Lissu wametukanwa, wamezomewa, wametiwa korokoroni kwa kutetea mikataba na sheria yenye usawa kati ya mwekezaji na mzawa
Kwahiyo mkuu unadhani hatua hii iliyochukuliwa. ..unadhani Rais anahadaa umma for what? ? Kama Ana hadaa for how long will t last? ? Jamaa now hatafuti Kiki ili umpigie kura. ..anayatimiza yale aliyoyaahidi na anayodhani yanatija kwa watanzania makabwera ambao ndio wengi. ..kiufupi hata kama unamchukia jamaa basi suport hata juhudi anazozionyesha coz tukiungana mim na wew kwa pamoja tutapata Tanzania tuliyoitaka iwe..unless otherwise utakua unaichukia Tanzania Hutaisuport hii vita aloianzisha
 
Dah! !?what a dumb nation like this? ? Rais anapigania mikataba ya madini ikae sawa watu eti wanamsikilizia ajikwae? ?tuwe na huruma kwa vizazi vyetu vijavyo guys we are too much selfish
You are getting it wrong my dear. Hii nchi ni yetu na tunatamani sana kuona utawala wenye unyenyekevu, sikivu, makini na shirikishi. Sisi hatukuchagua Rais wa kutupigania, kutukomboa bali wa kutuongoza na kutusikiliza. Uongozi ni kuileta pamoja jamii ili iwe na maono (vision) yanayofanana kuhusiana na mustakabali wao. Tulichagua viongozi wa kutuleta pamoja tuweze kujiletea wenyewe maendeleo. Viongozi tuliowachagua wanapokuwa arrogant, all-knowing, impulsive, populist na kutaka kutuaminisha kuwa waliopita walikuwa hovyo, lazima tupate hofu. Hofu inakuwa kubwa zaidi pale watu wanapoona masuala ya kisheria yanashughulikiwa kisiasa tena kwa mbwembwe. Kigezo kimoja tu cha umakini wa uongozi ni jinsi maamuzi yanavyofanyika; kwa subira na mashauriano.
 
Ni bora ingeundwa tume humu JF tukawaweka wajuaji kadhaa pale na mimi nikiwepo kusaidia kwenye mahesabu ya kuzidisha na kugawanya,kuliko juu uwongo wa mchana
 
Dah! !?what a dumb nation like this? ? Rais anapigania mikataba ya madini ikae sawa watu eti wanamsikilizia ajikwae? ?tuwe na huruma kwa vizazi vyetu vijavyo guys we are too much selfish
Lini kapigania mikataba ya madini irekebishwe mnaona kwenye mchanga ndo tunapoibiw sana kuliko kwenye madini yenyewe
 
27 Mei 2017
ACACIA MINING PLC

TAARIFA KWA UMMA

Maelezo zaidi juu ya taarifa ya uchunguzi iliyotolewa na kamati ya kwanza ya Rais kuhusu usafirishaji wa makinikia.

Acacia inapenda kuendelea kutoa ufafanuzi kuhusu matokeo ya uchunguzi wa Kamati ya Kwanza ya Rais juu ya kusafirishwa nje kwa makinikia ya dhahabu/shaba. Matokeo hayo ya Kamati yaliwasilishwa na kukabidhiwa kwa Mh. Rais, Dr. John P. Magufuli, tarehe 24 Mei, 2017.
Tumeiomba serikali nakala ya taarifa kamili ya Kamati hiyo lakini bado hatujapatiwa, vile vile tumeomba taarifa ya kina ya utaratibu wa tafiti za sampuli uliotumiwa na Kamati. Tumetathmini matokeo yaliyowasilishwa na Kamati ambayo yamechapishwa na tunapenda kutamka yafuatayo:

• Kulingana na takwimu tulizonazo kwa zaidi ya miaka 20 – ambazo tutazitoa kwa utafiti zaidi – hazioani na matokeo yaliyowasilishwa na Kamati.

• Takwimu hizi za kihistoria zilikusanywa na kuchambuliwa na wataalam na taasisi za Tanzania na Kimataifa, huku zikitoa matokeo yanayofanana mara zote.

• Takwimu hizi ambazo ni huru na zilizohakikiwa na wataalam zimekuwa zikionesha kwamba kiwango cha dhahabu katika makinikia ni pungufu kwa moja ya kumi (1/10) ikilingalishwa na takwimu za utafiti zilizotolewa na Kamati.

• Ni dhahiri kwamba endapo matokeo yaliyochapishwa na Kamati yangetokana na takwimu sahihi, basi migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi ingekuwa inaongoza duniani kwa kuzalisha dhahabu nyingi zaidi.

• Kutokana na utofauti huu mkubwa wa kitakwimu tunaamini kunapaswa kuwepo na ukaguzi huru wa madini yaliyomo kwenye makinikia.

Tutafanya tathmini ya kina zaidi pindi tutakapopokea taarifa kamili ya Kamati. Lakini kwa sasa tunapenda kuwafahamisha yafuatayo kutokana na matokeo ya Kamati:
Kiwango cha dhahabu katika makinikia

Takwimu za uhakika ambazo Acacia inazo zinaonesha kwamba makontena 277 yaliyopo bandari ya Dar es Salaam yana jumla ya ujazo wa wakia 26,000 za dhahabu. Kila kontena lina wastani wa kilo 3 (kama wakia 100) za dhahabu, kilo 3 za madini ya fedha, na kilo 3,000 za madini ya shaba. Matokeo ya Kamati yalionesha kwamba kiwango cha dhahabu katika makontena yote, ambacho ni cha mwezi mmoja tu wa uzalishaji, kilikuwa jumla ya tani 7.8 (au wakia 250,000). Lakini uhalisia ni kwamba mwaka 2016 Acacia ilizalisha na kuuza wakia 250,000 za dhahabu katika makinikia kutoka migodi hii miwili kwa kipindi chote cha mwaka.

2
Kwa mantiki hii, matokeo ya utafiti wa Kamati yanamaanisha kwamba migodi miwili tu ya Bulyanhulu na Buzwagi kila mmoja huzalisha zaidi ya wakia milioni 1.5 za dhahabu kila mwaka. Hii inamaanisha kwamba migodi hii inazalisha dhahabu nyingi kuliko mingine yote duniani; kwamba Acacia ni mzalishaji wa tatu kwa ukubwa kidunia na kwamba Acacia huzalisha dhahabu nyingi zaidi kutoka katika migodi yake mitatu pekee kuliko kiasi ambacho kinazalishwa na Kampuni ya AngloGold Ashanti yenye migodi 19, Goldcorp yenye migodi 11, na Kinross yenye migodi 9.

Uzalishaji wa dhahabu unaotangazwa:
Kampuni ya Acacia inaweka wazi na kutangaza kiwango chote cha dhahabu na mapato ambayo yanawiana kikamilifu na wakia za dhahabu na madini ya fedha na tani za madini ya shaba ambazo Acacia huzalisha, kuuza na kutangaza. Taarifa za uzalishaji na mapato pamoja na takwimu zote hukaguliwa kikamilifu, na zimekuwa zikionesha kwamba Acacia haifaidiki kutokana na dhahabu ya ziada (ile iliyo mara 10 zaidi) ambayo matokeo ya Kamati yanasema Acacia haikutangaza.

Mirahaba kutoka kwenye madini mengine:
Chini ya sheria za Tanzania na makubaliano yetu na serikali, tunalipa asilimia 4 (%) ya mirahaba ya dhahabu, madini ya fedha pamoja na shaba yaliyomo kwenye makinikia. Siku zote Acacia imelipa mirahaba kwa serikali na kuna ushahidi wa kutosha wa ukaguzi ili kuthibitisha jambo hili. Na japokuwa kuna aina nyingine za madini katika makinikia, ikiwemo chuma, sulphur, rhodium na mengineyo, madini haya hayana kiwango kinachofaa kibiashara na hivyo Acacia haipokei mapato kutokana nayo na hivyo hakuna mrabaha unaolipwa.

Historia ya uzalishaji na mapato:
Acacia ni kampuni ilioorodheshwa katika soko la hisa yenye mamia ya wanahisa, taarifa zetu za fedha, uzalishaji na akiba ya dhahabu ardhini hukaguliwa kwa viwango vya kimataifa na wakaguzi wengi walio huru, na tunawajibika kukidhi vigezo vya taasisi za ukaguzi na udhibiti za Tanzania, Uingereza, Canada, na Marekani. Taasisi hizi za udhibiti za kimataifa ni huru na hutekeleza majukumu yake kwa umakini mkubwa, na zinaweza kutoza faini kubwa sana kwa makampuni yasiyotoa taarifa za uzalishaji na mapato kwa usahihi. Hivyo basi, haiwezekani Acacia itoe taarifa za chini ya kiwango kuhusu akiba yake ya dhahabu, uzalishaji na mapato husika hata kwa kipindi kifupi cha muda, achilia mbali ndani ya kipindi cha miaka mingi. Tunashindwa kuelewa ni kwa jinsi gani Kamati iliweza kupata matokeo iliyoyapata bila hata ya kuzishirikisha taasisi hizi huru za ukaguzi na udhibiti.

3
Kama matokeo ya utafiti wa Kamati yangekuwa sahihi, na Buzwagi ingekuwa inazalisha na kuuza mara kumi zaidi ya dhahabu zaidi ya inayotangaza, Acacia ingeongeza shughuli za uchimbaji Buzwagi kwa miaka mingi. Ukweli ni kwamba Buzwagi ni mgodi wenye daraja la chini la dhahabu na dhahabu yenye faida kibiashara inaelekea kuisha .
Usahihi wa vipimo kihistoria:

Tangu mwaka 1977, zaidi ya sampuli 215,000 zimechukuliwa na timu za wataalam wa kijiolojia wa Tanzania kutoka katika mgodi wa Bulyanhulu peke yake na makampuni mengi tofauti ya utafiti na uchimbaji na kufanya uchunguzi wa kina na kuthibitisha kwa kufanya vipimo katika maabara nchini Tanzania na nje ya nchi. Hakuna matokeo yoyote kati ya hayo yaliyofanywa ambayo yanafanana na matokeo yaliyowasilishwa na Kamati ya Rais ambayo kamati ilikusanya sampuli kutoka kwenye makontena kama 44 kati ya makontena 277 ya makinikia yaliyopo bandarini.
Endapo matokeo ya Kamati ya Rais ni sahihi, maana yake ni kwamba makampuni mengi, timu za wanajiolojia na maabara za uchunguzi zilizohusika na mgodi wa Bulyanhulu tangu mwaka 1977 pamoja na ule wa Buzwagi tangu miaka ya 1990 yameshindwa kufanya tafiti za sampuli kwa usahihi, ikiwemo kuzifanyia uchunguzi na kutoa taarifa sahihi juu ya kiwango cha ubora wa dhahabu kilichopo ardhini, na uzalishaji wa dhahabu/shaba/fedha katika vipindi hivi.

Isingewezekana kwa makampuni haya yanayofanyiwa ukaguzi kutoa taarifa za chini ya kiwango kuhusu akiba ya dhahabu na uzalishaji kwa kiwango kikubwa namna hii hata kwa kipindi kifupi tu cha muda, achilia mbali kipindi cha miaka mingi.

Kwa kuhitimisha, tunashindwa kuyaelewa matokeo ya uchunguzi ya Kamati ya Rais na tunaamini kwamba yanatofautiana kwa kiasi kikubwa na takwimu zilizofanyiwa uchunguzi kipindi cha nyuma. Tumekuwa tukilipa mirahaba yote kama itupasavyo kwa madini husika tunayoyazalisha. Usafirishaji wetu wa makinikia nje ya nchi hufanyika kwa kuzingatia kikamilifu sheria za Tanzania na makubaliano ya kisheria ambayo tunayo na serikali ya Tanzania. Katika migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi, jumla ya athari ya moja kwa moja ya zuio la usafirishaji wa makinikia nje ya nchi ni wastani wa hasara ya mapato kwa siku, inayozidi dola za Kimarekani milioni moja (sawa na angalau shilingi bilioni mbili za Tanzania). Kwa hali hii, tunatathimini kila tuwezalo kufanya.
Kwa taarifa zaidi wasiliana na:
Acacia Mining plc
+44 (0)207 129 7150
Giles Blackham, Meneja Uhusiano – Uwekezaji
Wezi tu. .. Kwanini wasisubiri maoni ya time ya pili?
 
Kwahiyo mkuu unadhani hatua hii iliyochukuliwa. ..unadhani Rais anahadaa umma for what? ? Kama Ana hadaa for how long will t last? ? Jamaa now hatafuti Kiki ili umpigie kura. ..anayatimiza yale aliyoyaahidi na anayodhani yanatija kwa watanzania makabwera ambao ndio wengi. ..kiufupi hata kama unamchukia jamaa basi suport hata juhudi anazozionyesha coz tukiungana mim na wew kwa pamoja tutapata Tanzania tuliyoitaka iwe..unless otherwise utakua unaichukia Tanzania Hutaisuport hii vita aloianzisha
Msome Lissu vizuri namna alivyotoa ushauri wake katika kudeal na hili jambo, kk hakuna hata mmoja aliyeko upande wa wanyonyaji, hapa nafikiri tunatofautiana na namna approach yake ya kudeal na hii issue
 
27 Mei 2017
ACACIA MINING PLC

TAARIFA KWA UMMA

Maelezo zaidi juu ya taarifa ya uchunguzi iliyotolewa na kamati ya kwanza ya Rais kuhusu usafirishaji wa makinikia.

Acacia inapenda kuendelea kutoa ufafanuzi kuhusu matokeo ya uchunguzi wa Kamati ya Kwanza ya Rais juu ya kusafirishwa nje kwa makinikia ya dhahabu/shaba. Matokeo hayo ya Kamati yaliwasilishwa na kukabidhiwa kwa Mh. Rais, Dr. John P. Magufuli, tarehe 24 Mei, 2017.
Tumeiomba serikali nakala ya taarifa kamili ya Kamati hiyo lakini bado hatujapatiwa, vile vile tumeomba taarifa ya kina ya utaratibu wa tafiti za sampuli uliotumiwa na Kamati. Tumetathmini matokeo yaliyowasilishwa na Kamati ambayo yamechapishwa na tunapenda kutamka yafuatayo:

• Kulingana na takwimu tulizonazo kwa zaidi ya miaka 20 – ambazo tutazitoa kwa utafiti zaidi – hazioani na matokeo yaliyowasilishwa na Kamati.

• Takwimu hizi za kihistoria zilikusanywa na kuchambuliwa na wataalam na taasisi za Tanzania na Kimataifa, huku zikitoa matokeo yanayofanana mara zote.

• Takwimu hizi ambazo ni huru na zilizohakikiwa na wataalam zimekuwa zikionesha kwamba kiwango cha dhahabu katika makinikia ni pungufu kwa moja ya kumi (1/10) ikilingalishwa na takwimu za utafiti zilizotolewa na Kamati.

• Ni dhahiri kwamba endapo matokeo yaliyochapishwa na Kamati yangetokana na takwimu sahihi, basi migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi ingekuwa inaongoza duniani kwa kuzalisha dhahabu nyingi zaidi.

• Kutokana na utofauti huu mkubwa wa kitakwimu tunaamini kunapaswa kuwepo na ukaguzi huru wa madini yaliyomo kwenye makinikia.

Tutafanya tathmini ya kina zaidi pindi tutakapopokea taarifa kamili ya Kamati. Lakini kwa sasa tunapenda kuwafahamisha yafuatayo kutokana na matokeo ya Kamati:
Kiwango cha dhahabu katika makinikia

Takwimu za uhakika ambazo Acacia inazo zinaonesha kwamba makontena 277 yaliyopo bandari ya Dar es Salaam yana jumla ya ujazo wa wakia 26,000 za dhahabu. Kila kontena lina wastani wa kilo 3 (kama wakia 100) za dhahabu, kilo 3 za madini ya fedha, na kilo 3,000 za madini ya shaba. Matokeo ya Kamati yalionesha kwamba kiwango cha dhahabu katika makontena yote, ambacho ni cha mwezi mmoja tu wa uzalishaji, kilikuwa jumla ya tani 7.8 (au wakia 250,000). Lakini uhalisia ni kwamba mwaka 2016 Acacia ilizalisha na kuuza wakia 250,000 za dhahabu katika makinikia kutoka migodi hii miwili kwa kipindi chote cha mwaka.

2
Kwa mantiki hii, matokeo ya utafiti wa Kamati yanamaanisha kwamba migodi miwili tu ya Bulyanhulu na Buzwagi kila mmoja huzalisha zaidi ya wakia milioni 1.5 za dhahabu kila mwaka. Hii inamaanisha kwamba migodi hii inazalisha dhahabu nyingi kuliko mingine yote duniani; kwamba Acacia ni mzalishaji wa tatu kwa ukubwa kidunia na kwamba Acacia huzalisha dhahabu nyingi zaidi kutoka katika migodi yake mitatu pekee kuliko kiasi ambacho kinazalishwa na Kampuni ya AngloGold Ashanti yenye migodi 19, Goldcorp yenye migodi 11, na Kinross yenye migodi 9.

Uzalishaji wa dhahabu unaotangazwa:
Kampuni ya Acacia inaweka wazi na kutangaza kiwango chote cha dhahabu na mapato ambayo yanawiana kikamilifu na wakia za dhahabu na madini ya fedha na tani za madini ya shaba ambazo Acacia huzalisha, kuuza na kutangaza. Taarifa za uzalishaji na mapato pamoja na takwimu zote hukaguliwa kikamilifu, na zimekuwa zikionesha kwamba Acacia haifaidiki kutokana na dhahabu ya ziada (ile iliyo mara 10 zaidi) ambayo matokeo ya Kamati yanasema Acacia haikutangaza.

Mirahaba kutoka kwenye madini mengine:
Chini ya sheria za Tanzania na makubaliano yetu na serikali, tunalipa asilimia 4 (%) ya mirahaba ya dhahabu, madini ya fedha pamoja na shaba yaliyomo kwenye makinikia. Siku zote Acacia imelipa mirahaba kwa serikali na kuna ushahidi wa kutosha wa ukaguzi ili kuthibitisha jambo hili. Na japokuwa kuna aina nyingine za madini katika makinikia, ikiwemo chuma, sulphur, rhodium na mengineyo, madini haya hayana kiwango kinachofaa kibiashara na hivyo Acacia haipokei mapato kutokana nayo na hivyo hakuna mrabaha unaolipwa.

Historia ya uzalishaji na mapato:
Acacia ni kampuni ilioorodheshwa katika soko la hisa yenye mamia ya wanahisa, taarifa zetu za fedha, uzalishaji na akiba ya dhahabu ardhini hukaguliwa kwa viwango vya kimataifa na wakaguzi wengi walio huru, na tunawajibika kukidhi vigezo vya taasisi za ukaguzi na udhibiti za Tanzania, Uingereza, Canada, na Marekani. Taasisi hizi za udhibiti za kimataifa ni huru na hutekeleza majukumu yake kwa umakini mkubwa, na zinaweza kutoza faini kubwa sana kwa makampuni yasiyotoa taarifa za uzalishaji na mapato kwa usahihi. Hivyo basi, haiwezekani Acacia itoe taarifa za chini ya kiwango kuhusu akiba yake ya dhahabu, uzalishaji na mapato husika hata kwa kipindi kifupi cha muda, achilia mbali ndani ya kipindi cha miaka mingi. Tunashindwa kuelewa ni kwa jinsi gani Kamati iliweza kupata matokeo iliyoyapata bila hata ya kuzishirikisha taasisi hizi huru za ukaguzi na udhibiti.

3
Kama matokeo ya utafiti wa Kamati yangekuwa sahihi, na Buzwagi ingekuwa inazalisha na kuuza mara kumi zaidi ya dhahabu zaidi ya inayotangaza, Acacia ingeongeza shughuli za uchimbaji Buzwagi kwa miaka mingi. Ukweli ni kwamba Buzwagi ni mgodi wenye daraja la chini la dhahabu na dhahabu yenye faida kibiashara inaelekea kuisha .
Usahihi wa vipimo kihistoria:

Tangu mwaka 1977, zaidi ya sampuli 215,000 zimechukuliwa na timu za wataalam wa kijiolojia wa Tanzania kutoka katika mgodi wa Bulyanhulu peke yake na makampuni mengi tofauti ya utafiti na uchimbaji na kufanya uchunguzi wa kina na kuthibitisha kwa kufanya vipimo katika maabara nchini Tanzania na nje ya nchi. Hakuna matokeo yoyote kati ya hayo yaliyofanywa ambayo yanafanana na matokeo yaliyowasilishwa na Kamati ya Rais ambayo kamati ilikusanya sampuli kutoka kwenye makontena kama 44 kati ya makontena 277 ya makinikia yaliyopo bandarini.
Endapo matokeo ya Kamati ya Rais ni sahihi, maana yake ni kwamba makampuni mengi, timu za wanajiolojia na maabara za uchunguzi zilizohusika na mgodi wa Bulyanhulu tangu mwaka 1977 pamoja na ule wa Buzwagi tangu miaka ya 1990 yameshindwa kufanya tafiti za sampuli kwa usahihi, ikiwemo kuzifanyia uchunguzi na kutoa taarifa sahihi juu ya kiwango cha ubora wa dhahabu kilichopo ardhini, na uzalishaji wa dhahabu/shaba/fedha katika vipindi hivi.

Isingewezekana kwa makampuni haya yanayofanyiwa ukaguzi kutoa taarifa za chini ya kiwango kuhusu akiba ya dhahabu na uzalishaji kwa kiwango kikubwa namna hii hata kwa kipindi kifupi tu cha muda, achilia mbali kipindi cha miaka mingi.

Kwa kuhitimisha, tunashindwa kuyaelewa matokeo ya uchunguzi ya Kamati ya Rais na tunaamini kwamba yanatofautiana kwa kiasi kikubwa na takwimu zilizofanyiwa uchunguzi kipindi cha nyuma. Tumekuwa tukilipa mirahaba yote kama itupasavyo kwa madini husika tunayoyazalisha. Usafirishaji wetu wa makinikia nje ya nchi hufanyika kwa kuzingatia kikamilifu sheria za Tanzania na makubaliano ya kisheria ambayo tunayo na serikali ya Tanzania. Katika migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi, jumla ya athari ya moja kwa moja ya zuio la usafirishaji wa makinikia nje ya nchi ni wastani wa hasara ya mapato kwa siku, inayozidi dola za Kimarekani milioni moja (sawa na angalau shilingi bilioni mbili za Tanzania). Kwa hali hii, tunatathimini kila tuwezalo kufanya.
Kwa taarifa zaidi wasiliana na:
Acacia Mining plc
+44 (0)207 129 7150
Giles Blackham, Meneja Uhusiano – Uwekezaji
Mimi nadhani utaelewa mwenyewe kwamba watanzanoa walitakiwa kukaa kimya au kuchunguza kama wanaibiwa?
Hapa wamegundua wanaibiwa kimsingi wana haki ya kuonesha wazalendo namna walivyoibiwa endelelea kuwajuza wabongo mamma mlivyozulumu!
 
Back
Top Bottom