Ni Rais gani katika Afrika mwenye rekodi nzuri ya kuhudhuria mikutano ya kimataifa?

Gosbertgoodluck

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
2,855
401
Wazee,
Najua waandaaji wa mikutano au vikao vya kimataifa hualika viongozi wengi kutoka nchi mbalimbali duniani. Lakini najua vilevile kwamba siyo viongozi wote wanaoalikwa huhudhuria vikao hivyo na hata kutuma wawakilishi wao kwa sababu mbalimbali. Kwa mfano, nakumbuka nimewahi kusikia kwenye vyombo vya habari kuwa Bingu Mutharika wa Malawi amegoma mara kadhaa kuhudhuria mikutano mbalimbali ya kimataifa kwa maelezo kuwa ni gharama kubwa.

Sasa wazee ebu tumwage data hapa. Je, ni rais gani katika bara la Afrika mwenye rekodi nzuri ya kuhudhuria vikao vya kimataifa?
 
Si mwingine ni yule yule Raisi aliyewahi kuvunja rekodi yake mwenyewe ya kukaa nje ya nchi kwa zaidi ya siku 22... Dr... Dr... Dr... Jamani Dr... Dr... Dr... Jamani Dr... JMK
 
Duuuu, hizo PhD zimeniacha hoi kabisa. Ni kama ulichoka kutaja ukataka kuacha vile!! Ungekuwa karibu mkwere angeagiza uletewe tusker bariiiiiiiiiiiiiidi.
 
Wazee,
Najua waandaaji wa mikutano au vikao vya kimataifa hualika viongozi wengi kutoka nchi mbalimbali duniani. Lakini najua vilevile kwamba siyo viongozi wote wanaoalikwa huhudhuria vikao hivyo na hata kutuma wawakilishi wao kwa sababu mbalimbali. Kwa mfano, nakumbuka nimewahi kusikia kwenye vyombo vya habari kuwa Bingu Mutharika wa Malawi amegoma mara kadhaa kuhudhuria mikutano mbalimbali ya kimataifa kwa maelezo kuwa ni gharama kubwa.

Sasa wazee ebu tumwage data hapa. Je, ni rais gani katika bara la Afrika mwenye rekodi nzuri ya kuhudhuria vikao vya kimataifa?

Ni Vasco Da Gama oh samahani ni JK wa Tz, huyu mr hajawahi kukosa mikutano mpaka amekuwa maarufu, na kuwa mwenyekiti kutokana na ushiriki wake kwenye mikutano hizo!
 
Nani zaidi ya Kikwete, hadi kuzindua kaburi Malawi alienda mwenyewe kitu ambacho balozi angeweza kufanya. He gat nothing to do in TZ.
 
kuanzia 20005 mpaka sasa naamini rais wa tanzania mh. jakaya kikwete ndiye anaongoza
 
Back
Top Bottom