Ni rahisi kuwatambua

SI unit

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
1,953
766
Watanzania ni wamoja lakini ni rahisi kumgundua kila mtu na kabila lake kwa kuzingatia lafudhi na matamshi ktk lugha yetu ya kiswahili:
Wahaya-mara nyingi utasikia wakichanganya kiswahili na ki-ingilish bila kusahau neno 'of couz', 'kwa kweeri mama koku', n.k
Wachaga-ni wazito kuongea, mara nyingi alfabeti "v" huchanganywa na "f" mfano "fiatu fyako" badala ya "viatu vyako", 's' na 'z' mfano maandasi badala ya maandazi.
Wasukuma- Wanatumia nguvu sana kuongea (wakandamizaji), mara nyingi kila neno wanaloongea wanamalizia na "ga" mwishoni mfano, naendaga badala ya 'naenda'
Endelea...
 
wandengereko na kabila lingine kama hilo nimelisahau almaarufu waswahili wao huongea kama chereani, hawaongei kwa nukta
 
Warangi wao siyo kwnye lafudhi!! wao hupenda sana chini!!
MP.
 
Kuna wale tunaochanganya 'R' na 'L' (tupo wengi hapa) mfano 'kamari' inatamkwa kama 'kamali', 'limao'='rimao'.. AFANDE MWITA HEBU RIRETE HIRO RIKIBAKA KITUONI MARA MOJA!
Haaaahaaaa ukipita mtwara utakutana NTWARA...NKUU WA NKOA...NKEWE yan mkewe...mkuu wa mkoa....dah ila MFUPA tu ndo wanaweza kulitamka
 
Haaaahaaaa ukipita mtwara utakutana NTWARA...NKUU WA NKOA...NKEWE yan mkewe...mkuu wa mkoa....dah ila MFUPA tu ndo wanaweza kulitamka

Mmakonde mmoja aliambiwa atamke neno sigara, akasea Chitaki.
chitaki=sitaki.
"Akina njomba nchumali mpo?" mie chichemi neno! Duh!
 
Pitia kidogo kwa Mama Anne Kilango.
"Thina wathiwathi na kiwanda cha Tangawidhi, tudhalishe tu tutaudha kwa yueth-dola"
 
Back
Top Bottom