Makonda anafanya maonesho kuliko kazi

Sean Paul

JF-Expert Member
Jun 16, 2013
807
2,106
Moderator hamjanitendea haki uzi wangu kwenda kuunganisha na uzi wa Makonda atakuwa Waziri/Rais. Mada yangu ni tofauti.

Naomba niulize swali kabla sijasahau.
Je, CCM, kinyago walichokichonga wenyewe kimeanza kuwatisha?

Nimekuwa mfuatiliaji wa siasa za nchini kwetu na kwa kiasi fulani, naona mambo yanakwenda ndivyo sivyo. Muda si mrefu tumepata kutangaziwa uteuzi wa Paul Makonda kama katibu wa Itikadi na uenezi wa Chama cha Mapinduzi. Kwanza naomba ku declare interest kabisaaa. Mimi sijawahi kumuelewa Makonda katika utendaji wake, si ki chama wala serikali.

Akili yangu imekataa kabisa. Neno langu si sheria nami si lolote wala chochote katika chama na serikali lakini mimi kama raia wa kawaida, kwa maoni yangu, Makonda havimtoshi viatu vya uenezi. Hata alipokuwa Kamishna wa Mkoa wa Dar es Salaam (Mkuu wa Mkoa) alikua na tabia kama hizi anazofanya sasa.

Makonda amekuwa na tabia ya kuongea bila kujali maslahi, utu na vyeo vya watu wengine. Kwa jicho lingine ni mtu anayependa kutrend kwenye media.

Siku si nyingi sana tangu ateuliwe ameshakuwa gumzo kwa kauli na matendo yaliyo nje ya mipaka yake ya kazi.
Novemba 1 akiwa Dodoma, alimwita kamishna wa Mkoa, Rosemary Senyamule jukwaani huku akiamuri "kimbia hapa" kisha anampa maagizo.

Kamishna yule anatoa majibu kuwa suala husika limeshafika kwa Makamu wa Rais, ila yeye akasema Kamishna wa Iringa na Dodoma wapigiane simu wapate majibu. Kisha anampigia Alfayo Kidata wa TRA anamhoji nakumpa maagizo. Huu ni mfano tu, lakini keshafanya vitu mfano wa haya kwa Anthony Mavunde, waziri wa madini na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Swali rahisi, kayapata wapi mamlaka haya? Kihulka Makonda ni kama vile hajui mipaka yake. Mimi siamini kama hajui, usikute ndio siasa yenyewe anatufanyia. Maana kwenye suala la Mavunde ni kama vile alikua anajua Mavunde atakwenda Geita kesho yake naye akampigia kumwambia afike Geita kesho. Ni kweli alikua hajui, au ndio siasa?

Mara kapanda punda, mara kapanda tipper, mara kaingia na ngamia......kwa maoni yangu mimi, Makonda anafanya maonesho kuliko kazi.
Sean.
 
Bashite ni zero brain. Anajitahidi kutafuta kila njia ku-compensate asicho nacho, lakini kwa bahati mbaya, ndiyo anazidi kujianika zaidi na kumwonesha kila mwenye akili timamu, amepungukiwa nini?

Mtu hutumia kile alicho nacho ili kupata maisha. Mtu hawezi kutumia akili, kama hana akili. Ndiyo maana jamaa anajitahidi sana kutumia nguvu, kwa sababu ndicho pekee alichojaliwa.
 
Aisee........
 
Lakini kwanini wenye mamlaka wakampa uteuzi? Walitafuta watu wakakosa?
 
Moderator hamjanitendea haki uzi wangu kwenda kuunganisha na uzi wa Makonda atakuwa Waziri/Rais. Mada yangu ni tofauti.

Naomba niulize swali kabla sijasahau.
Je, CCM, kinyago walichokichonga wenyewe kimeanza kuwatisha?

Nimekuwa mfuatiliaji wa siasa za nchini kwetu na kwa kiasi fulani, naona mambo yanakwenda ndivyo sivyo. Muda si mrefu tumepata kutangaziwa uteuzi wa Paul Makonda kama katibu wa Itikadi na uenezi wa Chama cha Mapinduzi. Kwanza naomba ku declare interest kabisaaa. Mimi sijawahi kumuelewa Makonda katika utendaji wake, si ki chama wala serikali. Akili yangu imekataa kabisa. Neno langu si sheria nami si lolote wala chochote katika chama na serikali lakini mimi kama raia wa kawaida, kwa maoni yangu, Makonda havimtoshi viatu vya uenezi. Hata alipokuwa Kamishna wa Mkoa wa Dar es Salaam (Mkuu wa Mkoa) alikua na tabia kama hizi anazofanya sasa.

Makonda amekuwa na tabia ya kuongea bila kujali maslahi, utu na vyeo vya watu wengine. Kwa jicho lingine ni mtu anayependa kutrend kwenye media.
Siku si nyingi sana tangu ateuliwe ameshakuwa gumzo kwa kauli na matendo yaliyo nje ya mipaka yake ya kazi.
Novemba 1 akiwa Dodoma, alimwita kamishna wa Mkoa, Rosemary Senyamule jukwaani huku akiamuri "kimbia hapa" kisha anampa maagizo. Kamishna yule anatoa majibu kuwa suala husika limeshafika kwa Makamu wa Rais, ila yeye akasema Kamishna wa Iringa na Dodoma wapigiane simu wapate majibu. Kisha anampigia Alfayo Kidata wa TRA anamhoji nakumpa maagizo. Huu ni mfano tu, lakini keshafanya vitu mfano wa haya kwa Anthony Mavunde, waziri wa madini na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Swali rahisi, kayapata wapi mamlaka haya? Kihulka Makonda ni kama vile hajui mipaka yake. Mimi siamini kama hajui, usikute ndio siasa yenyewe anatufanyia. Maana kwenye suala la Mavunde ni kama vile alikua anajua Mavunde atakwenda Geita kesho yake naye akampigia kumwambia afike Geita kesho. Ni kweli alikua hajui, au ndio siasa?

Mara kapanda punda, mara kapanda tipper, mara kaingia na ngamia......kwa maoni yangu mimi, Makonda anafanya maonesho kuliko kazi.
Sean.
CCM wana saccos mna Wasiwasi sana.
 
1 ya chapisho zuri sana, ikiwapendeza ccm wasikushambulie wachukue kama somo!

Ngoma I kivu ma sana ……
 
Nchi ni yetu sote hii. Hivi mnadhani mnamkomoa Lema au Mbowe?
Mnamkomoa shangazi yako huko Mwanhuzi, Simiyu.
😂😂😂😂😅😆ona sasa mimi nilizani tunazungumzia UTETEZI WA KITAIFA kumbe ni hao uliowataja.

Hao bana sina neno nao mana wanajua why wapo hapo na bila kuwepo hapo ni kisanga.

Kichwa chako kilivyo mbofumbofu na mlivyofunzwa na hao unaowatetea badala ya taifa mnajikiaje mnapowaweka kama wakazi wa SIMIYU kama sehemu ya watu wa hovyo kimaonesho wanafaa???
 
Whatever the case, nchi ngumu yetu tunaishi sote.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom