Ni pesa gani huwa unazikumbuka ukifulia?

Dunamist

JF-Expert Member
Aug 13, 2018
474
682
Binafsi huwa nazikumbuka sana

- Ngawira zangu nilizolipia gym wakati ningeweza kupiga zangu push ups home na jogging nikachoma calories kama kawaida, na
- Zile nilizolipa car wash kuosha kamkweche kangu wakati ningeweza kukapiga maji mwenyewe home alone kakang'aa kama kawaida

Wewe je!
 
Kitendo cha kuajiri mtu wa kunipikia na kufua wakati nilikuwa na nafasi ya kufanya mwenyewe. Nilikuwa na kaduka kadogo nikaweka mfanyakazi ningeweza kukaa mwenyewe dukani. Sasa nimefulia, napika na kufua mwenyewe
Ndugu inaonekana awamu hii imekufanya vibaya sana
 
Acheni uswahili inamaana mpaka sahivi hakuna aliewatumiaga wale jamaa wa hiyo hela tuma kwenye namba hii!!!
Inamaana biashara yao haikwenda sawa au mnaona aibu tu wana jf..?
Hatutakucheka we sema tu..😅
 
Acheni uswahili inamaana mpaka sahivi hakuna aliewatumiaga wale jamaa wa hiyo hela tuma kwenye namba hii!!!
Inamaana biashara yao haikwenda sawa au mnaona aibu tu wana jf..?
Hatutakucheka we sema tu..😅
Jf kila mtu yuko smart na yuko vema kimaisha mkuu, hahahahhh
 
Back
Top Bottom