Ni njia nzuri ya kuomba msamaha ukweni pale unapokuwa umewakosea

Mboka man

JF-Expert Member
Aug 22, 2020
478
1,638
Bila kupoteza muda naomba niende kwenye uhalisia wa Mada kuna kosa kubwa nimelifanya ukweni nalo ni kuzungumza uongo ambao umepelekea Baba mkwe kunikasirikia sana.

Uongo wenyewe ni kwamba niliahidi kutoa mahari kiasi nilichopangiwa lakini finally nilishidwa kutimiza baada ya kutoa kiasi kidogo cha pesa kuliko walivyotarajia hali iliompelekea ukweni kuniona mimi ni muongo, msanii na muhuni hali iliyompelekea binti kusimangwa Sana familia yao.

Lakini pia mbali na yote kuna taarifa nimepewa nahitajika ukweni familia kwa sasa ninawaza nifanyaje na njia ipi sahihi naweza itumia kuomba msamaha.
 
Kama haya ni ya kweli basi familia ya ukweni kwako inajidharirisha!,watu wengi huwa hawajui swala huwa si mahali swala ni kwamba unampeleka binti yako mahali sahihi..?

Unaweza weka mahali kubwa au ukataka ulipwe mahali yote lkn kikaenda kuumana huko,mahali ni swala la kupita tu ila maisha ya ndoani haya ndo yakuangalia zaidi maana hii ndio kesho ya mtoto wako na wajukuu wako.
 
Tatizo ni huu umaskini wetu na kukosa maarifa ndoman unakuta familia nyingne zinafanya watoto wakike kam sehemu ya kupata fedha
 
Back
Top Bottom