Unatumia njia gani kuwasaidia ndugu na jamaa zako pale kipato chako kinapokuwa chini ya mahitaji yako ya muhimu?

Heaven Seeker

JF-Expert Member
May 12, 2017
478
1,046
Heshima kwenu Wakuu.

Nimebahatika kuishi Nchi za wenzetu kwa Mabeberu, kiasi fulani nimejifunza mambo kadhaa.

Sisi Wabongo tunaishi maisha ya ujamaa, yaani kugawana kidogo tunachokuwa nacho ili kila mtu apate japo mkate. Hali hii inatokana na ukweli kuwa idadi kubwa ya sisi wabongo bado maisha yetu yapo chini sana hivyo idadi ya wategemezi kwenye familia zetu bado ni kubwa sana hivyo tunaishi kwa kutegemeana.

Hata hivyo, hali ni tofauti kwa wenzetu mabeberu. Nadhani hii inatokana na kuwa, wao kiwango cha ukosefu wa ajira ni kiasi kidogo sana, hivyo kila familia ina uwezo wa kujiingizia kipato chake na kumudu gharama za maisha. Jambo lingine ni kuwa, wenzetu hawana maisha ya kijamaa kiviile. Yaani ni yeye na familia yake full stop. Mnaweza kuwa mnaishi nyumba moja ila mkawa mnasalimiana tu hakuna stories zaidi ya hapo. Msamiati wa kukopana pesa sijauona, ukiwa na shida unaweza kuomba msaada kwenye serikali ya jimbo lako. Kwa nchi kama Sweden, serikali ya mahali unapoishi inaweza kugharamia gharama za kuishi kwa vijana wasiokuwa na ajira ama kupoteza ajira. Unaweza kupata pesa ya kujikimu na ukalipiwa rent. Hi ni kwa raia pekee. Siyo kama sie wakuja.

Nirudi kwenye mada sasa.

Vibwagizo kidogo

1. Nilipokuwa nasoma wakati flani, kutokana na maisha yetu ya uduni, nilikuwa nikiomba masaada kwa ndugu yangu (binamu) hapa na pale ili kukidhi mahitaji muhimu. Huyu binamu yangu, kwa maoni yangu, alikuwa na unafuu kidogo wa maisha kwa maana ya kuwa na ajira, nyumba yake na kiusafiri. Hivyo kwa kuwaza kwangu kipindi hicho nikajua atakuwa na maisha bora na ana mpunga wa kutosha. Chakushangaza, wakati mmoja nikamuomba msaada nilikuwa chuoni wakati boom limekata akawa amenitumia kiasi cha pesa kidogo sana kuliko nilivyotarajia. Niwe muwazi kuwa nilifadhaika, nikasema, yaani kweli binamu ananitumia elfu 10 tu kweli? na nimemweleza kuwa nina shida na sina kitu kabisa?

2. Huyohuyo binamu yangu, wakati nipo mdogo kwa shangazi yangu, nilikuwa nashangaa, iweje tunaishi maisha magumu pale home pengine pesa ya kula inakata na wakati yeye ana kazi huko Dar na anakula maisha? (mawazo yangu). Na pesa ilipokuwa inakata, binamu alikuwa hatumi pesa mpaka Shangazi apige simu na akipiga alikuwa anatuma kiasi kidogo sana. Kwakweli niliwaza sana nikajisemea kuwa kwanini watu waliofanikiwa kupata vijisenti hawatumi pesa kwa wazazi wao mpaka waambiwe? Ina maana hawajui wajibu wao?

3. Kumbe buana, yale yalikuwa nawazo ya utoto tu. Ukubwani sasa nimegundua kuwa Binamu yangu alikuwa ameajiriwa na pengine kipato chake kilikuwa cha kawaida sana na kutokana na majukumu ya familia yake na maisha ya mjini tena Dar, basi kipato chake si chochote kivile kumudu maisha na kutuma mapesa mengi kwao kama nilivyokuwa nawaza nikiwa mdogo.

4. Mawazo yangu hapo juu, yametokana na ukweli kuwa, pamoja na kipato changu kuongezeka karibia mara mbili ya kipato changu cha awali, nimegundua kuwa hata mie wazazi wangu sijawatosheleza kwa kuwasaidia mahitaji yao kwa kiwango cha kuridhisha sana. Yaani wanaishi maisha yenye unafuu kidogo ila bado wana ganga ganga tu. Pamoja na kujitahidi kutokuwa mbinafsi na kuishi maisha ya kawaida, bado naona kabisa hata msaada wangu wa kwa ndugu na jamaa bado ni kidogo sana pamoja na kipato changu kuongezeka kidogo. Najua huwezi kumfurahisha kila mtu na huwezi kuacha kulaumiwa, ila naamini wapo watu wanaoniona kama mtu niliyefanikiwa na nimeshindwa kuwasaidia. Kumbe bado naganga ganga tu.

Naomba nijielekeze kwenye hoja ya msingi baada ya vibwagizo hapo juu.
Naomba kulizungumzia kundi la wale ambao vipato vyao huweza kugharamia mahitaji ya msingi kama chakula, mavazi na kulipia kodi ya nyumba ama pengine anaishi kwenye nyumba yake. Kundi hili baadhi ya watu huliita kama middle class family. Kwa uchunguzi wangu, kundi hili lina mzigo mkubwa kwenye jamii maana jamii yetu hasa wale wanaotoka kwenye extended families na jamaa zao hawawezi kumudu mahitaji muhimu, hulitazama kundi hili kama kundi lenye unafuu kimaisha, hivyo hutegemea kupata msaada kutoka kwao. Hata hivyo, kutokana na kipato chao kulingana na matumizi, tena yale ya lazima tu, kiukweli kundi hili hujikuta kwenye changamoto kubwa kimaisha na kushindwa kukidhi matarajio ya jamaa zake na kuonekana kama mtu mbinafsi, hivyo hutupiwa lawama kwa kiasi kikubwa ilihali vipato vyao pengine vinatosheleza tu kula chakula na kulipia kodi ya nyumba.

Je, wewe kama kipato chako kina balance na matumizi yale ya lazima pekee, yaani chakula, mavazi na makazi. Huwa unatumia njia gani kusaidia ndugu na jamaa zako ambao wana maisha duni na wana matarajio makubwa kutoka kwako? Kumbuka nazungumzia mtu ambaye akipata kipato chake kinalingana na matumizi kwa mwezi husika na hawezi kufanya hata savings. Nyongeza, namzungumzia mtu ambaye si mbinafsi, ana moyo wa kuwasaidia wahitaji ila uwezo wake upo chini zaidi ya kile anachotakiwa kufanya katika jamii yake. Wahitaji wanaweza kuwa ndugu wa karibu wa tumbo moja, mabinamu, wajomba, mashangazi, baba mkubwa, mama mkubwa, rafiki wa karibu sana n.k.

1) Je, ni sahihi kukubali lawama kwa muda flani ili ubakie kwenye mapambano kwanza na usitoe msaada mpaka utoboe kwanza kufikia hatua ya kipato kuwa juu ya gharama za maisha? Natambua kuwa kadri kipato kinavyoongezeka mtu anaweza kuchagua maisha ya juu zaidi hivyo isifike siku ambapo atabakiza savings na kuwasaidia wahitaji, ila hapa nazungumzia wale ambao wana nia ya dhati ya kuwasaidia jamaa zao na pengine wangependa kuridhika na maisha waliyonayo hasa anapokuwa amefikia kwenye lifestyle inayomwezesha kula na kubakisha savings kila mwezi.

2) Au Je, kama maisha ya swali hapo juu ni ubinafsi, unadhani ni sahihi kupunguza gharama za maisha yako ili ukubali kurudi nyuma kidogo ili kubakiza savings, ziweze kuwasaidia jamaa zako wanaokutegemea? Kama kweli tunataka kutekeleza msemo wa kwamba kutoa ni moyo na si utajiri..?

3) Je, jambo hilo namba 2 hapo juu ni practical in real sense?

Nini maoni yako? Karibu ku-share mawazo ili tuelimishhane..
 
Tunapambana Mungu anatusaidia tunapata rizki lakin Hatuna uwezo wa kuwasaidia ndugu kiasi Cha kufanya watoke kwenye umasikini wakati na sisi bado tupo kwenye umasikini

Cha kufanya ni kimoja tu wasaidie wale ndugu wa chache tu waliopambana na wewe kipindi ukiwa hauna kitu na uachane kabisa na ndugu ambao wanajisogeza kwako kwakua wameona una kazi,biashara au una hafadhali kidogo ya maisha.

Walio kujali wakati hauna kitu na ww jitahidi kuwajali ila Cha kwanza jijali wewe mwenyewe jitafutie makazi yako, na ufungue/uboreshe biashara yako maana siku ukiyumba kiuchumi watasema ulikua na kazi, ulikua na biashara, ulikua na pesa lakin huna Cha maana ulicho fanya Leo hii unaishi kwa shemeji unalala sebleni kama baiskeli na kuvizia ugali

Mwsho wa yote ili ufanikiwe inahitajika uwe na roho mbaya maana hata ukiwa mwema sana huwezi kusaidia kila mtu
 
Inaonekana una roho nzuri hongera sana... kuna mambo mawili ya kuchagua 1. kuwa na huruma wakati ukiwa maskini ili uendelee kuwa maskini zaidi kwa sababu kwa mfano uwez kumuinua mtu ambaye wewe na yeye wote mmekaa chini.
2. uwe bandidu sasa ili uwe na maisha mazuri baadae.
NACHUKIA SANA UMASKINI
 
Mahitaji ya mwanadamu hayana kikomo,kadri unapopata rasilimali pesa,ndivyo nayo yanaongeza..Sasa ukiongezea na ya ndugu,jamaa na marafiki unaweza pata picha wengi wetu tunaishije.

Toa kadri ya uwezo ambao hautakuumiza..Maneno na fikra za watu juu yako haziepukiki,yawe hasi au chanya..
 
Watu tupunguze kuomba omba pia waweza mwona mtu yuko safi kumbe naye ana budget zake Kali na mengineyo Mimi wakati nasoma nilikuwa Hadi najilipia ada kwa bumu langu na sikuwahi kusumbua mtu tena saa nyingine nilikuwa Nampa mwenye uhitaji, kuliko kuomba omba hela ni heri ubuni wazo uombe kamtaji uanze kujishughulisha hyo itaondoa umaskini
 
Upo sahihi hata mie nilifanya hivyo. Tena nilikuwa natumia boom kulipia ada inayobakia maana sikupata 100% loan. Ila kuna wakati maji yalikuwa yanazidi unga. Nakumbuka kuna siku nimewahi kulala njaa nikiwa chuo kama siku moja hivi. Hali ilikuwa tete.
 
Nichangie hapa, maana mada ni nzuri sana na ninayaona haya waziwazi kwangu mimi.

1. Unatakiwa uamini kitu kimoja (Kwetu Waislam) sio kila aliyepata kazi basi ni kwa ajili ya maendeleo yake. Mara nyingi tunapata kazi au pesa kupitia riziki ya watu wanaotuzunguka ambao kwa namna moja ama nyingine wameshindwa kusoma, kuwa na afya au changamoto yoyote ile, ndipo Mungu hukupa wewe nafasi ili uweze kusaidia hao. Kwahiyo kaa ukijua sio kila aliye na pesa basi Mungu kampangia yeye, kuna wakati mungu hupitisha riziki za ndugu zako kwako wewe.

2. Tuna mila, desturi na tamaduni zetu kama waafrika, mfano, wakati wa ujauzito wako unakuta ukoo mzima walimsaidia mamako katika kuilea na hata kufanikisha uzao wako. Na hata ulipokuwa mdogo ulilelewa katika mazingira ya ujamaa uliokomaa kama huo, ambapo kinachopatikana ni cha familia au ukoo na sio chako peke yako. Hivyo ni jukumu lako kujua mila na desturi zetu kabla ya kuamua chochote kwenye familia yenu.

3. Ni kawaida sana kwa sisi waafrika na ambao tunaotoka extended family kutoa msaada wa pesa kuliko msaada wa kumtafutia kazi mtu, hali hii hupelekea kuombwa pesa mara kwa mara na hata kujiona unaonewa sana. Hata Wazungu wanasaidiana sana tu, nimejionea hayo kwa macho yangu nilipokuwa UK, then Germany na hata Brazil wanasaidiana sana tu. Utofauti wao ma sisi ni kwamba wao hawana familia kubwa kama sisi. Unakuta mzungu ana watoto wawili au watatu tu. Hali hii humpunguzia mzigo mkubwa wa kuhudumia familia yake.

TUJE NAMNA GANI NATUMIA KUSAIDIA NDUGU ZANGU.

Kwanza nikiri nimetokea familia Duni sana hapa TZ, familia ambayo ilistahili kusaidiwa na TASAF, Familia ambayo imewahi kusaidiwa chakula na Serikali sio mara 2 au 3. Nimesoma kwa shida sana, Mama yangu alikuwa anauza mgahawa mkoani MTWARA. Wajomba zangu walevi, na wavuta bangi na Unga, mama zangu wadogo hawakuwa na elimu na hivyo kuhangaika tu na maisha. Nilijitoa mimi mwenyewe kuamua nikomae na shule nikiamini nitaikomboa familia yangu, hivyo familia ile ilikuwa ina jukumu la kunipa chakula, madaftari nk huku akili yangu ikiwaza mafanikio na uchungu wa kuondokana na umasikini ule uliotopea.

Mara baada ya mafanikio kadhaa, i started to buy them a monthly food. Ninahakikisha kila mshahara unapoingia ninanunua chakula cha ile familia yetu, na ukweli ni gharama ndogo sana sema vijana hatuna moyo wa kukumbuka tulipotoka ( Unga Kg 25 ni 24000, mchele 30 kg 60000, mafuta ya kupikia 10000, maharage Kg 6, Gesi, pamoja na pesa za roba za mkaa as you know familia zetu. Ni around 150k) pia nimejitahidi watoto wa dada zangu, mama zangu wadogo wako kama 10+ nimewakatia bima TOTO AFYA KADI natumia kama 1 M per year plus madaftari ya mwaka nzima nayaweka nyumbani ili kuwapunguzia gharama hizi. Mara nyingi ukiwapa chakula kila mwezi unakuta kuna mwezi vyakula vinakutana hivyo kufanya mwezi unafata kutonunua tena.

Kama unaweza kupangilia vizuri matumizi unaweza kuwasadia ndugu zako kwa ustadi tu. Mpaka hapa tayari nimewatafutia kazi ndugu zangu ili kupunguza utegemezi wapo JWTZ wapo 2, Polisi 1, na kuna mmoja yeye nilipambana mpaka sasa yuko Nje anapiga misha na kwa sasa amenipunguzia mzigo sana sana tu.

Tuwe tunalenga kusaidia vitu vya msingi huku tukiwaambia hali ya umasikini si nzuri na tunapaswa kushikamana kama ukoo kuondoa umasikini huo.

Now familia ina nyumba nzuri ya familia yenye uhakika umeme + maji nk. Najisikia furaha nikienda Mtwara kumcheki bimkuwa akiwa katika hali ya furaha muda wote akikumbuka jitihada alizozifanya.

THE END.
 
Chukia UMASKINI, wapende MASIKINI…. umaskini sio dhambi japo sio jambo jema.
 
Mkuu ahsante sana kwa inputs zako. Umeniongezea mambo muhimu sana siku ya leo.
Ila naomba kuuliza maswali yafuato.

1) Wakati umeanza kujipatia kipato chako, ulikuwa unaweza kutosheleza mahitaji yale ya msingi wakati huo?
2) Kama jibu ni hapana hapo juu, uliwezaje kuwasaidia ndugu na jamaa zako wakati huo ambapo kipato chako kilikuwa chini ya mahitaji yako ya msingi?
 
Hapana kwa mwanzoni sikuweza kupata mahitaji muhimu.
Nilivyogundua pesa haitoshelezi niliamua kukumbuka maisha niliyokulia as kama role model wa maisha yangu, hivyo nikaopt kujibana as if sina kazi ili niweze kuendana na hali halisi ya nyumbani na familia yetu. Hali hiyo nilidumu nayo kwa miaka mi3 mpka nikawa stable kiuchumi.
Hapa ndipo vijana wengi wanafeli, akishaajiriwa TRA, TPA nk anataka apate gari ndani ya miaka 3 ya mwanzo hali inayoongeza gharama za matumizi na kupelekea kutowasaidia waliokusaidia.
KUMBUKA, AFRIKA NI LAZIMA KUWASAIDIA NDUGU ZAKO NA SIO OMBI.
 
1. Kwa maana hiyo Mkuu unaweza kukubaliana nami kuwa si rahisi kuwasaidia watu wako wa karibu endapo kipato chako kipo nchini ya mahitaji yako ya msingi?
2. Kama unakubaliana na hoja hapo juu, Je, itakuwa sahihi kwa mtu kuamua kujifungia mwenyewe mpaka afanikiwe kwanza (awe stable) ndio aanze kuwainua na jamaa zake?

Hongera sana kwa kuwa stable baada ya miaka 3 tu ya kuanza kujipatia kipato chako. Wengine inachukuwa muda kweli. Nia unakuwa nayo na unaishi maisha ya kujibana, ila bado hali inakuwa hairuhusu. Na hapa ndipo lawama zinakujia nyingi hasa kwa wale waliokusaidia.

Nyongeza; uliweza vipi ku-handle stress za lawama za wale ambao wanadhani walikusaidia na bado hujaweza kuwasaidia?
 
Lazima uwasiadie mkuu, mimi nilipogundua nina kipato kidogo lkn familia yangu ni duni sana nami nikaamua niishi maisha yale ya chini zaidi ya kipato ili niwape mwanga wenzangu. Huwezi kuwa tofauti na mila na desturi zetu za kiafrika.
 
Ishi vile nafsi yako inavokutuma Maisha hayana formula!!!!saidia kutokana na sauti ya ndani inavokuongoza!!!hivyo usije ukabeba majukumu yasiyo kuhusu maishani mwako!!hivyo tu!!usije ukawa disappointed siku moja!!!
 
Mtu anayekuwa DISAPPOINTED na NDUGU ZAKE NI HAJIELEWI. Hao ndio watakuuguza pamoja na UTAJIRI WAKO ndugu ndio msaada wako, hakuna mtu aliuguzwa na MARAFIKI ZAKE. Jitambue kama kijana, we've a lot to do in this world lkn kubwa WAPENDE NDUGU ZAKO. WAO NDIO WATAZOA MAVI YAKO WAKATI UKO HOI KITANDANI.
Ukisaidia ndugu umejisaidia wewe mwenyewe.
 
Unauhakika na usemacho kijana?sasa ni kuambie ndugu zako wa kweli ni wanao tu!!na Mama yako mzazi akiwa bado upo hai!!wadogo zako au kaka au dada wajali kiasi tu LAKINI don't count too much on them!!wanamajukumu na familia zao ndio kipaumbele chao sio wewe!!!Nakuambia with personal experience not with words!!hapa kwangu nimeishi na ndugu wawili kutoka familia yetu na familia ya mke wangu nimeona ni Total mess!!!nasaidia kiasi LAKINI siwekezi nguvu zangu nyingi kwao Sana najali Mama Sana wao watapambana coz sio walemavu na wala sio vichaa!!!Huwa na waambia hakuna cha bure wala cha kupewa mtaji ni afya zao tu wachape kazi!!labda wanafunzi kidogo ndio nawajali kwao matumizi tena madogo ya muhimu tu na hivyo sitarajii makubwa wala fadhila Toka kwao!!!Nimesaidia moja juzi ananitishia Maisha na familia yangu kisa nimemwmbia aende kwake familia yake inamuhitaji yeye anataka akaye kwangu abweteke anachojua ni mitungi na mikasi!!!MISAADA inapumbaza waafrika badala ya kuwasaidia ipo siku utalea watoto wa ndugu zako kisa hawawajibiki ipasavyo!!!!with personal experience not by hate or illusions!!!
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom