Ni njia ipi bora ya kuifanya biashara changa iweze kustawi kwa kasi?

mshale21

JF-Expert Member
Apr 8, 2021
2,049
4,904
Wakuu natumai hamjambo!

Naomba mwenye skills na experience katika biashara anisaidie mawazo, namna ya kuinua na kuifanya biashara changa iweze kustawi vizur na kwa kasi!

Tuweke utani pembeni, naomba michango yenu ya kimawazo.

Natanguliza shukran!
 
Ukitaka biashara yako ikue kwa HARAKA zaidi,

Ukishatoa matumizi yote,
Kwa sikU Hutakiwi kutumia zaidi ya 10% ya faida yote uloingiza kwa sikU

Inamaana,
Kwa mfano umeuza laki 1, na ukapiga hesabu zako ukakuta faida yako Ni elfu 10.

Basi
Kama umeingiza faida ya 10,000 kwa sikU,
Hupaswi kutumia zaidi ya 1,000 kwa iyo sikU husika Kwenye matumizi yako yote ya binafs na familia.
 
Ukitaka biashara yako ikue kwa HARAKA zaidi,

Ukishatoa matumizi yote,
Kwa sikU Hutakiwi kutumia zaidi ya 10% ya faida yote uloingiza kwa sikU

Inamaana,
Kama umeingiza faida ya 10,000 kwa sikU,
Hupaswi kutumia zaidi ya 1,000 kwa iyo sikU husika.
Asante Sana mkuu, napoamkia mishemishe kesho lipo kwenye utekelezwaj!

Barikiwa Sana!
 
2. Ukitaka biashara yako ikue kwa HARAKA

Hakikisha malipo ya mishahara ya wafanyakazi wako kwa mwezi
Yawe yanaweza kulipwa na 10% ya faida yako ya sikU ndani ya robo ya kwanza ya mwezi (yaani sikU 8)

Inamaana,
Kama unaingiza faida ya 100,000 kwa sikU, Basi 10% itakua Ni sh. 10,000
Kwaiyo ndani ya sikU 8, itakua Ni sawa na 80,000

Kwaiyo,
Kama biashara yako inaingiza faida ya laki 1 kila sikU,
Gharama za mishahara yako kwa mwezi hazitakiwi kuzidi 80,000
 
2. Ukitaka biashara yako ikue kwa HARAKA

Hakikisha malipo ya mishahara ya wafanyakazi wako kwa mwezi. Yawe yanaweza kulipwa na 10% ya faida yako ya sikU ndani ya robo ya kwanza ya mwezi (yaani sikU 8)....
Mkuu haya madini nmeyameza Kama yalivyo, ntafanya hivyo hivyo mkuu!
 
Kama Hali ya kibiashara Ni ngumu sana,

Na eneo ulilopo gharama za maisha ziko juu sana na matumizi yanakubana Sana.

Basi hakikisha matumizi yako yote kwa siku, yasizidi 5% ya JUMLA ya mauzo yako yote kwa siku.

Inamaana,
Kama dukan KWAKO unauza JUMLA ya 1,000,000 kwa sikU nzima

Hakikisha matumizi yako yote ya ofisi, binafsi na ya familia hayazidi sh. 50,000 kwa sikU nzima.
 
Kwenye biashara,
Ukifeli Kwenye kubalansi mapato yako na matumizi yako.

Basi Kwenye game tunakusahau HARAKA Sana.

Utajiona unauza sana,
unazungusha Sana ila hukui na Ela huioni.

Nidhamu ya pesa ndio msingi wa mafanikio.

Kamwe,
Usihofu Wala USIOGOPE KUITWA BAHILI,
maana Siri ya mafanikio iko humo humo Kwenye ubahili.
 
Weka bidhaa zenye quality nzuri + reasonable price. Kwa kuanza usitake faida kuubwa

Jali wateja wako na uwahudumie vizuri ili kesho warudi tena

Fanya marketing ya product/service zako, usitegemee wateja wa eneo moja

Uwe mbunifu katika biashara yako

Muhimu ya yote uwe mvumilivu, biashara zina changamoto nyingi + kukatishwa tamaa hasa na watu wa karibu yako. Pambana bila kujali vikwazo huku ukiamini utafanikiwa.
 
Nyongeza,
Ukitaka biashara yako ikue HARAKA,

Kama vihela kidogo vipo,

Jifunze kutengeneza connection na watu muhimu Kwenye biashara yako.

Watu muhimu Namaanisha,
-madalali
-wakuu wa vituo vya polisi OCD,rpc n.k
-maafisa biashara
-maafisa TRA
-Wazee wa chama.

Connection zinaweza husisha rushwa ndogo za kubrashia viatu Kama bia, nyama choma, nyongeza ama bonus wakinunua KWAKO, kushiriki kwa kuchangia Kwenye shughuli zao za kijamii Kama misiba, harusi, vikoba n.k

Hii inasaidia siku likitokea la kutokea, unakua na backup ya kukusaidia.

Kwa lugha rahisi,
Hii inakua Ni Kama BIMA YA BIASHARA YAKO.
 
Weka bidhaa zenye quality nzuri + reasonable price. Kwa kuanza usitake faida kuubwa

Jali wateja wako na uwahudumie vizuri ili kesho warudi tena....
Mkuu nashukur kwa ushaur wako mzuri!

Ila Ni tips zipi ambazo zitaniongoza kufanya marketing ya service ninayoitoa?
 
Mkuu nashukur kwa ushaur wako mzuri!

Ila Ni tips zipi ambazo zitaniongoza kufanya marketing ya service ninayoitoa?
Inategemea aina ya service zako na wateja husika.

Mf. Kama wateja wako wakubwa ni maofisini na mashuleni basi wafate ukajitangaze (kwa kuacha business card au kipeperushi kinachoelezea service zako)

Social networks pia ni njia nzuri zaidi ya kutangaza biashara yako... Tengeneza profile ya biashara, weka picha nzuri na maelezo ya kutosha.... Promote matangazo yako uyalipie ili yawafikie watu wengi zaidi
 
Kwenye biashara,
Ukifeli Kwenye kubalansi mapato yako na matumizi yako.

Basi Kwenye game tunakusahau HARAKA Sana.

Utajiona unauza sana,
unazungusha Sana ila hukui na Ela huioni.

Nidhamu ya pesa ndio msingi wa mafanikio.

Kamwe,
Usihofu Wala USIOGOPE KUITWA BAHILI,
maana Siri ya mafanikio iko humo humo Kwenye ubahili.
Mkuu, haya madini si mchezo yaani umepita mule mule kwny uti wa mgongo wa biashara yoyote ile!
 
Lakini mkuu ungetuambia kua unafanya biashara gani na upo mkoa gan, pengine ingesaidia sn mtu mwny uzoefu ktk field hyo aweze kukusaidia!
 
Wakuu natumai hamjambo!

Naomba mwenye skills na experience katika biashara anisaidie mawazo, namna ya kuinua na kuifanya biashara changa iweze kustawi vizur na kwa kasi!

Tuweke utani pembeni, naomba michango yenu ya kimawazo.

Natanguliza shukran!
Juju
 
Kwenye biashara,
Ukifeli Kwenye kubalansi mapato yako na matumizi yako.

Basi Kwenye game tunakusahau HARAKA Sana.

Utajiona unauza sana,
unazungusha Sana ila hukui na Ela huioni.

Nidhamu ya pesa ndio msingi wa mafanikio.

Kamwe,
Usihofu Wala USIOGOPE KUITWA BAHILI,
maana Siri ya mafanikio iko humo humo Kwenye ubahili.
Mkuu huko sahihi kabisa ubahili na savings ndo mafanikii ya kukuza kipato. Nilishaletaga uzi humu jinsi navyobeba boksi masaa hadi zaidi ya 16. Na nilikuwa nimepanga kwenye shared apartments. Kuna wakati nilikuwa naingiza kama 3000 euros au dollars kwa wiki mbili. Nilikuwa naendaga kuchukua chakula wanapotoa bure. Getto langu ni kitanda tu na meza na kiti. Toka 2012 hadi 2020 April hela niliyosave siyo mchezo. Kitu kinachonimalizia hela ni sigara na mmea. Nikijitahidi kupungu nitasave zaidi lazima nitumie kama laki 6 ya bongo kwenye haya makitu. Denmark ndo nchi inalipa high wages kwa wabeba boksi skendinevia ikifuatiwa na norway
 
Back
Top Bottom