Premij canoon
JF-Expert Member
- May 27, 2018
- 1,115
- 2,490
Salaam wanajukwaa,
Pole na mitikasi na mihangaiko ya kila siku, natumai sote ni wazima wa afya njema. Kama kichwa cha habari kinavyojieleza, katika uhangaikaji nimefanikiwa kufikisha kiasi cha milioni ishirini (20,000,000), nahitaji kufanya biashara ya spare za pikipiki kwa jumla na reja reja nipo nje kidogo ya Dar mkoa wa Pwani (Bagamoyo)
Naomba ushauri kwa wazoefu wa hii biashara... Je, milioni 20 itaweza kujitosheleza? Ikiwa ni pamoja na kwenda China, kununua mzigo, kuusafirisha hadi kufika TZ.
Kwa taarifa za awali nilizopata ni kwamba:
• Nauli GO & RETURN makadirio ya juu $1800 (Inaweza kupungua).
• Chakula & Malazi $35 per day. Nitatumia siku 3 tu kununua mzigo nakuukabidhi kwa kampuni ya usafirishaji kisha kurudi TZ ili kuepuka kupunguza mtaji kwa gharama kubwa za chakula & malazi! Hivyo $35 kwa siku 3 itakua $105 (Tsh 250,000)
Naomba kwa wazoefu kunisaidia mawazo na ushauri kwa huu mtaji wangu je, utajitosheleza kwenye biashara tajwa? kwa kuuza jumla na rejareja?
NB: Nafahamu kuna corona kwa sasa, hivyo nipo hapa kupata ushauri na kupata taarifa muhimu kwa sasa, hali itakapotulia ndipo natarajia kwenda.
NATANGULIZA SHUKRAN