Je, ni Halmashauri zote huhitaji fedha kutoka Serikali Kuu? Kuzipatia fedha nyingi mabilioni kila mwaka ni kuzidekeza na kuzifumba akili

Richard

JF-Expert Member
Oct 23, 2006
14,939
20,396
Juzi Rais Samia ametangaza tozo ya shilingi 100 kwa kila lita moja irejeshwe katika kodi ya mafuta.

Hapohapo wafanyabiashara wa mafuta hayo hawajalalamika bali wamefurahi maana wao wapata faida zaidi.

Licha ya kodi hiyo ya mafuta, gharama za maisha kwa ujumla zimepanda na mfumuko wa bei uko juu ambao unasababisghwa na wafanyabishara wengine wa bidhaa kama vyakula, mahoteli na hata bodaboda kupandisha nauli.

Hata mtaani kwetu hapa Kibaigwa, kumeanzishwa kodi ya shilingi elfu tano ya kuzolea taka ambayo yatakiwa kulipwa kila mwezi. Hii ya uzoaji taka imenikumbusha ni kunifanya nijiulize je Mwalimu Nyerere aliwezaje na serikali yake kuweka magari ya kuzolea taka mitaani kwenye miaka ya 80?

Mafuta ya kula nayo yameadimika ambapo mafuta ya kutoka nje yana gharama za juu kuliko yale ya ndani ambayo nayo hayatoshelezi walaji wa ndani.

Tozo zingine zaendelea katika miamala na njia zingine ambapo tozo hizi zinamuumiza zaidi mtanzania wa kawaida ambae bado ahitaji kujiinua kimaisha.

Mimi binafsi nimegundua kuwa serikali haina mfumo sahihi wa kodi ambao utairahisishia ukusanyaji bora wa mapato yake. Hali hiyo inapelekea serikali kuhaha kutafuta fedha zaidi kutoka vyanzo vingine hususan manipasa na miji.

Hii inajidhihirisha zaidi pale raisi Samia alipolalamika kwenye ziara mkoani Mara kwamba wahasibu wa ndani hawafanyi kazi zao ipasavyo na kuna ubadhilifu mkuwa wa fedha katika halmashauri.

Sasa nauliza je miji kama Da-es-Salaam, Tanga, Moshi, Arusha, Mwanza, Kahama, Morogoro, Iringa, Mbeya na miji mingine yenye hadhi ni lazima ipate fedha kutoka serikali kuu za kujiendesha?

Manispaa za miji hii zina majukumu ya kuhakikisha fedha za mapato zaelekezwa katika uboreshaji wa miundombinu kama barabara, shule, na vituo vya huduma za afya.

Lakini kuna huduma zingine muhimu kama polisi na zimamoto ambazo huitaji kuendelezwa kwa maana ya kujenga vituo zaidi vya polisi na vya zimamoto. Zidhani kama ni jukumu la serikali kuu kupeleka fedha za kuhudumia polisi na zimamoto ambapo askari wake tayari wanalipwa mishahara.Tumeshuhudia moto ukiunguza na kutekekeza baadhi ya maduka na masoko katika miji kdhaa hapa nchini jambo linochangiwa na ukosefu wa huduma za zimamoto ambazo zina vifaa imara.

Hali kadhalika vitendo vya uhalifu kama uporaji na uvunjaji katika sehemu mbalimbali kumechangiwa na kukosekana kwa vituo vituo vidogo vya polisi.

Mapato yatokanayo na ukusanyaji wa kodi mbalimbali na tozo kadhaa katika manispaa za miji hiyo ndizo zingelekezwa katika huduma nilozitaja hapo juu. Serikali ingeendelea na tozo zake kubwakubwa katika makampuni ya simu, biashara kubwakubwa, na fedha za gawio, pamoja na mapato yatokayo TRA.

Serikali ina njia nyingi sana za mapato kuanzia ushuru wa uingizaji magari, ushuru wa reli, ushuru wa utoaji leseni za udereva, ushuru wa mizani, kodi ya mapato (wafanyakazi na watumishi), tozo ya miamala, tozo ya mafuta, kodi ya viwanja vya ndege, kodi ya majumba, kodi ya viwanja na kodi zingine lukuki.

Isitoshe kodi ya viwanja na kodi ya majumba yapaswa kupelekwa kwenye manispaa na miji ili iwe kodi ya maendeleo katika sehemu hizo. Kuna vyanzo vya mapato vya serikali kama bandari, ushuru wa barabara, viwanja vya ndege (zikitua) na zingine ambazo kama zikiwa zimepangwa uzuri serikali haiwezi kukosa mapato ya kutosha kuzidi trillioni 3!

Sasa wana JF naomba niulize, Je serikali kwanini isiziachie manispaa na miji kujiendesha yenyewe kupitia mpango maalum (yaani pilot project) kisha kuona ni manispaa au mji gani wafanya uzuri katika kujiendesha wenyewe na kujidhibiti na kisha kuwa kila mwaka kunatolewa tuzo au awards?

Hii yaweza kuwa motisha katika kuleta chachu ya maendeleo katika manispaa na miji na kisha kueneza maendeleo hayo katika miji mingine ilo nyuma kimaendeleo.

Huko baadae twaweza kusema kwamba manispaa na miji yaweza kujiamulia masuala yake kama kuifanya nafasi ya meya iwe ya ushindani yaai awe wa kuchaguliwa na akae kwa miaka 4 au 5.

Meya wa manispaa awe ni mtu ambae aja kuleta maendeleo mapya na mawazo mapya na kuwafanya wananchi waone manispaaa ni yao, huduma zitolewazo ni zao na fedha inotumika pia ni yao.

Manispaa nyingi zajitahidi sana katika kuboresha miundombinu ya barabara ingawa sehemu za watembea kwa miguu (pavement) bado ubunifu wake wahitaji kufikiriwa. Ujenzi wa nyumba za makazi kiholela bado wahitaji kudhibitiwa na pia manispaa nyingi bado zipo nyuma katika kujenga au kuboresha sehemu za kupumzikia yaani (recreational grounds). Lakini huduma ambayo imekosa kabisa mipango thabiti ni huduma ya uzoaji taka na kuchakata taka (recyling) ambapo suala la uchafuzi wa mazingira limekuwa la kawaida katika manispaa na mijini.

Hayo yote yahitaji fedha na fedha hizo zatokea katika vyanzo mbalimbali ambavyo manispaa na miji zimeweka na watambua vilipo.

Wananchi tunahitaji barabara nzuri, madaraja imara, na njia za wapita kwa miguu pamoja na taa za mabarabarani ili kuweka mazingira yanovutia na usalama zaidi khasa nyakati za usiku.

Ukijenga barabara nzuri pembeni utaweza kuweka sehemu za kupaki magari na kuweka tozo khasa mijini hivyo manispaa na miji kujiongezea mapato.

Niloliona ni kwamba Serikali imekosa njia au mipango sahihi ya kukusanya kodi ili kuongeza mapato yake hali inopelekea kuanza kwenda katika halmashauri ama kuzibana ziongeze mapato au kuzibana zionyeshe matumizi ya fedha ambazo serikali yazipeleza huko.

Hapohapo, manispaa na miji nao baada ya kupokea mabilioni ya fedha kutoka serikali kuu kwa ajili ya miradi ya maendeleo, huanza kufungana kamba na kuanza matumizi mabaya ya fedha hizo ambazo ukichanganya na zile walozikusanya katika njia zao za mapato huzitumbua zote pia.

Je, ni manispaa na miji zote huitaji fedha za kujiendesha au kuboresha miradi ya maendeleo au ni zile ambazo ndo zenye uhitaji zaidi khasa miji midogo na wilaya changa?
 
Mtazamo mzuri sana.

Nami naona sahihi sana kuziacha wilaya zijiendeshe, serikali kuu iwe regulatory organ vitu visije vika escalate.

Viongozi wachaguliwe, na mfumo wa kuwawajibisha uwe rahisi.

Back
Top Bottom