Ni Nini Kinampa Mwanaume Heshima Katika Jamii?

Ni Nini Kinampa Mwanaume Heshima Katika Jamii?

sifa kuu ya mwanaume ni uwajibikaji tuu
yaani kukiwepo na matatizo anareact vipi
mwanaume ni yule anaeleta solution ya matatizo kwa jamii inayomzunguka
mfano kama ni elimu ahakikishe watoto wanapata elimu nzuri,wanavaaa fresh ,wagonjwa wanatibiwa,watu nyumbani mashavu yamewatoka yaani watu wanamzunguka wanaenjoy maisha
kama hata mwanaume ana mabilioni , watu hawaenjoy huyo sio au ni mcha mungu analala madhabahuni watoto wamepauka na kusinyaa njaa,wazazi hawapati hata hela ya dawa huyo sio,awe anaendesha range ndugu zake hawasomi hata huyo sio
yaaani unatakiwa ukiwa mwanaume watu wakufurahie kweli waseme ili jembe kweli


Mkuu uwajibikaji wa mtu utaufahamu vipi unapokutana naye kwa mara ya kwanza? Kama huyo mtu ndo kwanza naonana nahye, ni nini kitakufanya umpe heshima zaidi kuliko mwingine au vice versa?
 
"kiasi cha pesa na jinsi ya kuzitumia" kwanini usiheshimiwe!!!!!

Kwa hiyo Pesa ndo Sabuni ya roho na inaleta heshima?

Je matajiri lakini pia ni mabahiri wana nafasi gani katika kuheshimiwa?
 
in random order
  1. money
  2. honesty
  3. reliability/dependability
  4. Godliness
  5. respectul to others+himself
  6. good in bed
  7. aweze kuji-control emotion zake

Kwa ufupi ni kuwa na pesa na Kumcha Mungu (2,3,4,5)? Na pia awe mzuri katika mapenzi?
 
Kuipenda familia yake na jamii husika inayo mzunguka hili ndilo siraha ya mwanaume katika jamii

Mkuu, utakapoonana naye siku ya kwanza, na hujui lolote juu ya hayo uliyoandika, ni kitu gani kinamfanya aheshimiwe?
 
Superman kwanza kabisa swali lako lina pande mbili kuu na hapa naomba nilielezee as mwl aswaaaaaa! upande wa kwanza ni mwonekano wa mara ya kwanza na upande wa pili n mwonekano subsequent(mara nyingine)

nikianza kwa mara ya kwanza kabisa mm as mwl nikikutana na mwanaume yeyote awe mdogo ama mkubwa, tajiri ama maskini sitoweza kubagua eshima yangu kwake nooooooope. nitampa heshima staili as a man/gentle man. iwe nimekutana naye sokoni anabeba mizigo, iwe ni bandarini mshusha maboks kama Asprin, iwe ni ofcn mfunga tai kama rais nidham yangu itakuwepo kwake very fairly na wala sitajali nimemkuta kwenye daladala ama akipiga debe. ndivyo nilivyo na sijui ni kwann.

kwangu mm, eshima kwa mwanaume ni kitu cha kwanza kabisa kabisa ninapokutana nae na hii iko ata kwa wanafunzi wangu nawaeshsimu sana as ni wakaka wakubwa na wadogo.

sasa kimbembe kiko hapa kwa subsequent meeting............
kwenye maisha mwanadamu yyte yule husifiwa jambo moja kubwa nayo ni NIDHAMU kwenye maisha yake ya kila siku.
nidhamu hii hukaa kwenye mambo mengi sana kama vile uvaaji, uongeaji, matumizi ya hela , matumiz ya muda, kwenye staree, name anything nidhamu laziima iwepo.

hivyo basi yyte aliye na nidhamu kama mwanaume kwangu humfanya awe na heshima sana sana sana

Mkuu, umeongea katika Mktadha wa wewe kama wewe. Lakini je, jamii inayokuzunguka wote wana mtazamo kama huo? Kama siyo ni nini wengi wanaangalia?
 
Hakuna jibu sahihi.
Jamii itakuhesimu qa jinsi wewe unavyoijenga hiyo jamii.
Mhubiri anadai hekima ya maskini iliukomboa mji lakini hatakubuqa qani hana fweza.
Hivyo hekima ni bora kuliko utajiri.

Bazazi anaitafuta hekima.
​


Nimekusoma Mkuu.

Na je utakapoonana naye siku ya kwanza, ni nini kionyesho kitakachokufanya umpe heshima?
 
Mkuu, utakapoonana naye siku ya kwanza, na hujui lolote juu ya hayo uliyoandika, ni kitu gani kinamfanya aheshimiwe?

Upendo wa kweli unaonekana mkuu hauna kificho, huwa husikii huyu kijana au yule mzee ni mtu wa watu kwa sababu gani ni Upendo tu mkuu
 
28066_118693974965445_1121361860_n.jpg


Hawa nao kitaa wanaheshima zao

Duh Mkuu, hata kama ni cha Kwashakoo?
 
Heshima ya mwanaume katika jamii inaletwa na HEKIMA aliyonayo muhusika. Mwanaume mwenye hekima atakuwa na heshima kwa wengine iwe amekutana nao kwa mara ya kwanza au mara nyingi, iwe anawafahamu au hawafahamu. Ukiheshimu wengine heshima hiyo inarudishwa kwako.

Mwanaume mwenye hekima atatumia pesa (bila kujali kiasi) yake vizuri, atavaaa mavazi yanayodhaniwa na jamii husika kuwa ni ya heshima na atakuwa smart (milegezo a.k.a kata k haitahusika), atafanya mazoezi ili hata akiwa na kitambi basi kisiwe kitambi maradhi, atakuwa mcha Mungu, ataitunza familia yake na kuijali jamii inayomzunguka (atashiriki katika shughuli za kijamii) na mwisho hata awe na cheo kikubwa kiasi gani kama hajui kuwa cheo ni dhamana na kukitumia hicho cheo kwa kutoa huduma/kusaidia/kuongoza walio chini yake kwa hekima, hicho cheo hakitampatia heshima yoyote zaidi ya kuogopwa tu.
?

Mkuu Hekima unayosema inayobeba mambo yote ni kama ya Suleimani? Au una maana kuwa Mcha Mungu?
 
Back
Top Bottom