Ni nini kinachosumbua Maalim Seif?

Ni nini kinachosumbua Maalim Seif?

Wanaofikiria ngono muda wote wanavaa msuli hahahahahaha....kurahisisha kazi. Zaaneni mjaze Zenji muishi majini:sly::sly:

Baada ya utandawazi na mambo mengi kubadilika na maarifa na uelewa wa juu na analogia kufungwa na kuanza kwa digitali anataka zanzibar ijitegemee na Sultani apewe heshima na mwarabu awe huru kama kwao

Usijidanganye hata kidogo hakuna sultani wala muarabu anae fikiria kurudi znz.hizi fikra zako ziondowe au jaribu kufanya upya huo utafiti wako ulio kupa jibu hilo uliloliandika. Ninauhakika huijui historia ya znz na hata ya Tz unasikia tu maneno ya kwenye pombe .ndio unanukuu halafu unatuletea humu.
 
Haiwezekani dume zima linalomuogopa mkewe linabaki kujificha ficha kwa muda wa miaka 50?litakuwa hilo dume lina mushkel,kama dume (tanganyika)kweli hasa jitokeze.

ndo utamu wa kutumia akili, litaendelea kujificha na kula mambo tuuu....kwa raha zake...
na hata mpige vipi kelele, mshakuwa koloni,hamwezi ondoka mpaka Tanganyika iridhie, na isitoshe baadhi yenu mnapewa chai na kashata mnasahau malengo yenu...
 
Wazanzibar wapewe mamlaka kamili na hilo ndo analitekeleza seif.
CCM mnaumiza kichwa kwa kitendawili ambacho tiari Wazanzibar wamekitegua! kama mmeruhusu watambulike kama nchi ndani ya muungano kwann wasijulikane umoja wa mataifa? kwann wasipate wawakirishi ktk mataifa mbalimbali? kwann wasitembeze bakuri kama URT? kwann wasiwe na sarafu na BOT yao na sera ya uwekezaji watakayoisimamia na kuitekeleza wao ilhali wanatambua mipaka ya nchi?
Mwaka jana Shein na Seif wameingia mkataba na SHELL wa utafti wa mafuta ktk visima/vitaru3, eti mnazuga kuwakoromea wakati katiba yao tayari inaruhusu tafti za raslimali zitakazowanufaisha jamhuri ya watu wa Zanzibar.
Mnang'ang'ana kuwapakata wakati wanambeleko yao?
Muungano uvunjwe, unapoteza uharali wa kujadili maendeleo ya Watanganyika.
Badala ya kujadili Katiba yenye tija kwa mtanganyika mioyo yetu imefura kwa jaziba na attacks zidi muundo wa serikali za muungano.
 
Zanzibar in a siri nyingi!, tafuta kisa cha Sultan kumpachika ujauzoto mjakazi wa mkewe, ili kuficha siri, huyo mjakazi alikwenda kuozeshwa mahali mbali chap chap!, baadaye, mwana sulatan alizaliwa huko mjakazi alikoolewa!. Find out huyo mwana sulatan ni nani?!, tafuta uhusiano kati ya Sultanet ya Brunei na Sultanet ya Zanzibar!, find out who funds CUF and why?!.

Kwa taarifa tuu, CUF ilishinda 1995, ikashinda tena 2000!, pia ikashinda 2005!, na kushinda tena 2010 lakini kote kwa nini hawampi ushindi?!.

Visa vya Zanzibar havikuishia hapo, kuna ndugu tena wengine wawili, watoto wa baba mmoja, mama mmoja, tumbo moja!. CCM ikaamua kumzawadia urais kaka mkubwa, kisa ni kumuenzi baba yao aliyoifanyia makubwa Zanzibar, hivyo ule urais ulikuwa ni wa zawadi ya heshima ya marehemu babsa yao!. Baada ya kaka mtu kumaliza kipindi chake cha urais cha miaka 10!, mdogo mtu akachukua fomu kumrithi kaka mtu!. Chama kikamshauri, kwa vile aliyemaliza ni kaka yake wa tumbo moja, baba mmoja, mama mmoja!, hivyo kumpitisha mdogo mtu, itaonekana kama usultani!, mdogo mtu akagoma na kuibuka na madai mazito!, kuwa eti kama urais ni zawadi kwa mtoto wa yule Mzee waliomuheshimu, then "mtoto halisi aliyestahili ni yeye!".

Zanzibar haieshi vituko!, nataka niwashauri wajumbe wa bunge la katiba kuhakikisha Mwenyekiti wa kudumu anakuwa Mzanzibari, ili hoja ya serikali tatu ikishindwa, ije hoja ya serikali moja ndio itaimarisha haswa muungano na kuwakata kabisa hawa vilimimili na vitimbakwiri vya kutaka kuuvunja huu Muungano wetu adhimu, uliotokana na yale Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar!.

Mapinduzi Daima!.
Muunganno Milele!.
Pasco

hahaha!! kila nukta nilikua nikicheka sana kwa jinsi historia yako ya uongo na propaganda uluvyoiweka vizuri, anyway ila kumbuka kwamba Maalim seif sio wa kwanza kudai hakki ktk Muungano huu, sasa sijui Mzee Jumbe utamtungia historia ya uongo kwa kiasi gani, maana yeye pia ameingia kweny makucha ya Muungano tena bila ya kumshiriki Maalim seif!
kwang mimi kama wew ni Mzanzibar basi nitakuweka kwa wale wahafidhina wa Kisonge maana hizo ndio propaganda zao sijui wanamdanganya nani zama hizi...?
lakin kama wwe ni Mtanganyika nitaamin kwamba ile organization ya propaganda ya CCM chini ya babu Nyerere imekujaza kasumba vyakutosha, lakin umeshindwa kusoma a lama za nyakati, maana kwa sasa propaganda kama hizo hassa kwa Wazanzibar ambao kila cku wanasikia historia yao iliyojaa heshma na neeema daima hutupilia mbali kasumba kama hizo, maana hazina ukweli wala ushahidi wa kitaalamu,
sikukatazi kusema hivyo, maana wenzetu nasikia munalipwa kwa kueneza kasumba hizi, ila kaka yangu jarubu kutumia akili, ulimwengu wa sasa watu hupambana kwa hoja sio viroja!!
 
Kaka jua kwenye siasa hakuna Adui wa Kudumu wala Rafiki wa kudumu ni dynamic na si static.
 
Fumu, mimi binafsi sipendi ushirikiano wa kubembeleza mtu tuwe na uhusiano. Najua asilimia kubwa ya Wa-Zanzibar hawataki Muungano, na sipendi kabisa kuona wanaendelea kuwa katika kitu wasichokitaka. Nadhani hata huku bara watu wameshoshwa na vituko vya Zanzibar, na hakuna anaewataka. Tuwabembeleze kwani sie tunafaidika nini na Zanzibar ati? Kama ni mafuta huenda tunayo mengi kuliko yanayoweza kuwa Zanzibar, na wala hamna uhakika kama kweli yamepatikana.

Ila utashi wangu ni kwamba, ikiwa tunakubaliana kuvunja muungano basi mambo yafuatayo yanzingatiwe;

1. Ili kuzuia uwezekano wa kuja kunyanyaswa hapo baadaye, Watanzania bara waliko Zanzibar warudi kwao bara na wale walioko bara warudi kwao Zanzibar. Serikali zitakubaliana jinsi ya kuwarudishia mali zozote zisizohamishika walianzazo huko, ikiwa watashindwa kuziuza. Wale walioona kati ya Watanzania Bara na Visiwani wataruhusiwa kuchagua wanataka kuishi wapi.

2. Tanzania bara, ambayo iliacha kutumia jina Tanganyika huko nyuma iwe na uhuru wa kuendelea kutumia jina Tanzania ikitaka, kutokana na "branding" ambayokwa kiasi kikubwa imefanywa na Tanzania bara, na pia kwa kuwa Tanzania bara kuendelea kutumia jina Tanzania hakutaiathiri Zanzibar kwa namna yoyote. Tanzania inaweza pia kuchagua jina lolote jingine.

3. Mpaka wa baharini kati ya Zanzibar na Tanzania bara uwekwe kwa kufuata kanuni ya "international midline"

4. Utaratibu wa visa kati ya Tanzania Bara na Visiwani uanze mara moja ili kudhibiti muingiliano wa watu usio na uaratibu

Kinachoshangaza mara zote linapokuja suala la kudai usawa kwa Zanzibar katika muungano, licha ya kinachoitwa USOMI wa watanganyika wanakuwa VILAZA bila shaka kwa ujumla wake kuna vitu vimewaathiri. Dhulma, ufisadi, kukosa ustaarabu na dharau. Kwa nini ndugu yangu UNAWAZA MALI TU? za Wazanzibari na kwa nini mmekuwa na fikra kwamba muungano ukivunjika itakuwa ni ugomvi baina ya TANGANYIKA NA ZANZIBAR. Acheni vitisho na maapizo hapa ishu ni muungano wa USAWA na ikiwa hamuutaski hakuna ulazima. wala msidhani wazanzibari WATAACHA KUDAI haki zao kwa woga wenu. Nikwambie tu safari imeanza zamani sasa tuko katikati kuelekea mwisho isip[okuwa kuna watu wachache CCM wenye maslahi wanatuchelewesha nadhani hili unalijuwa?. Kuhusu kumshambulia maalim seif haisaidii wako maalim Seif wengi na wameshatayarishwa wengi zaidi hata aondoke leo kijiti anabeba mwengine? jiulize masuali haya. Ilikuwaje Zanzibar ikafanya mabadiliko ya katiba 2010 ilihali ni kiongozi wa CCM Zanzibar ( rais) aliyesimamia? jee yule naye alikuwa maalim Sief? . Mwaka huu mmeaza kuadhirika mara jina TANZANIA liwe ndio TANGANYIKA yaani mnaumbuka tu zile MISSION zenu zimevurugika kuimeza na kuimeza Zanzibar kwa malengo yenu yaliyojificha na kila siku zikipita yanadhihirika. Wazanzibari si wajinga wataendelea kuwafundisha siasa na ustaarabu kumnanga MAALIM SEIF HAISAIDII njoo na UZI mwengine UTAJIBIWA.
 
Kama vile yesu alivyokuwa!.midevu mireeefu! Kama Nabii Musa!

Wakati wenzake kina Dr na kina mrema!
Shavu lainiiiii.kama dodo!

Teh teh teh teh!

Acha upumbavu jadili mada, bichwa kubwa kama Tembo lakini ubongo wa Sisimizi.
 
Kinachoshangaza mara zote linapokuja suala la kudai usawa kwa Zanzibar katika muungano, licha ya kinachoitwa USOMI wa watanganyika wanakuwa VILAZA bila shaka kwa ujumla wake kuna vitu vimewaathiri. Dhulma, ufisadi, kukosa ustaarabu na dharau. Kwa nini ndugu yangu UNAWAZA MALI TU? za Wazanzibari na kwa nini mmekuwa na fikra kwamba muungano ukivunjika itakuwa ni ugomvi baina ya TANGANYIKA NA ZANZIBAR. Acheni vitisho na maapizo hapa ishu ni muungano wa USAWA na ikiwa hamuutaski hakuna ulazima. wala msidhani wazanzibari WATAACHA KUDAI haki zao kwa woga wenu. Nikwambie tu safari imeanza zamani sasa tuko katikati kuelekea mwisho isip[okuwa kuna watu wachache CCM wenye maslahi wanatuchelewesha nadhani hili unalijuwa?. Kuhusu kumshambulia maalim seif haisaidii wako maalim Seif wengi na wameshatayarishwa wengi zaidi hata aondoke leo kijiti anabeba mwengine? jiulize masuali haya. Ilikuwaje Zanzibar ikafanya mabadiliko ya katiba 2010 ilihali ni kiongozi wa CCM Zanzibar ( rais) aliyesimamia? jee yule naye alikuwa maalim Sief? . Mwaka huu mmeaza kuadhirika mara jina TANZANIA liwe ndio TANGANYIKA yaani mnaumbuka tu zile MISSION zenu zimevurugika kuimeza na kuimeza Zanzibar kwa malengo yenu yaliyojificha na kila siku zikipita yanadhihirika. Wazanzibari si wajinga wataendelea kuwafundisha siasa na ustaarabu kumnanga MAALIM SEIF HAISAIDII njoo na UZI mwengine UTAJIBIWA.

Chadema hawachukui nchi na kitachowakosesha ni vitu viwili:

1. UKRISTO WAO DHIDI YA UISLAM
2. UMAJIMBO WAO DHIDI YA ZANZIBAR NA MAJIMBO YA TANGANYIKA YENYE WAISLAM WENGI
 
tafuta cd ya mkutano alioufanya juzi tibirizi pemba maalim seif eddy moyo mansour abubakar na jusa utajua wazanzibar nini wanachokitafuta nenda makao makuu ya cuf utapata cd zake kaangalia then utajua nini wanachokitafuta hizi sio zama za porojo
 
Baada ya utandawazi na mambo mengi kubadilika na maarifa na uelewa wa juu na analogia kufungwa na kuanza kwa digitali anataka zanzibar ijitegemee na Sultani apewe heshima na mwarabu awe huru kama kwao

Mwiba kooni mtakufa na Zanzibar kinywani. Pasco waombe Mods wakuongezee uwezo wa kuweka likes :thumbup: kwa wingi.
 
Last edited by a moderator:
mimi nampenda maalim seif kwa misimamo yake atisha amemshindwa nyerere na wenziwe itakuwa nyie vijana wa jamii fourm mnavyomchafua mbele kwa mbele simba wanyika maalim seif sharif hamad hadi uikomboe znz na mungu akujalia umri mrefu na siha njema usirudi nyuma ushaingiza bega moja na mguu mmoja ktk serikari 2015 unamalizia bega jingine na mguu wachina wanasema mwendo wa mail 1000 huanza na moja.cheki dvd za mikutano ya maalim seif utajua nini anachokisimamia tv hawatoi mikutano yake ni mkakati maalum huo.
 
nimependa proposal yako, kwa upande wangu mimi ni muumini wa Jina Tanzania kuliko jina Tanganyika, yaani ukifungua moyo napenda muungano na jina Tanganyika viende kwao - ila Jina Tukufu Tanzania libaki, nafunga na kuomba kwa ajili jina TAMU lenye utu na la kiafrika,la kizalendo, wengi wetu tumezaliwa Tanzania hio Tanganyika ya kikoloni ya akina Mtikila, Warioba and et al wabaki nalo wao wenyewe, tuanze Kampeni ya kuokoa jina la Tanzania Bara


Tanganyika ya kikoloni ya akina Mtikila, Warioba and et al wabaki nalo wao wenyewe, tuanze Kampeni ya kuokoa jina la Tanzania Bara

Kwa hiyo Mafia, Songosongo, Nyuni,Kilwa, Kibaazi virudi kwao Zanzibar enh?

Wewe endelea kuzaliwa katika nchi ya Kusadika «Tanzania Bara» wazee wako waendlee waishi kwao Tanganyika.
 
Mafuta yapo mkuu ila kinachogomba ni katiba ya jamhuri iliyoyaweka kuwa ya muungano wakati ya Zanzibar imeyaondoa kwenye muungano. Wanavyodai wanasubiri katiba mpya itamke wazi kuwa mafuta si ya muungano ili wataanza kuyachimba.
 
Hebu tuacheni tupumue, hatulitaki hili dubwasha liitwalo muungano, Watanganyika mnachekesha, nyinyi mmejaaliwa ukubwa wa ardhi lakini badi mnaingangania Zanzibar. Kaeni na Tanganyika yenu tuachieni Zanzubar yetu tuchachoka na chokochoko zenu

Utakuta unabwabwaja hivi lakini upo bara umekimbia kazi ya kuzamia baarini kukamata pweza. nasubiria siku ya muungano ukifa tuanze kuwatimua.
 
Utakuta unabwabwaja hivi lakini upo bara umekimbia kazi ya kuzamia baarini kukamata pweza. nasubiria siku ya muungano ukifa tuanze kuwatimua.

Hawa si wamejazana huku Tanganyika, ooh tunataka Zanzibar yetu, rudini huko kwenu ndiyo mpige kelele. Ni vyema muungano ufe leo kila mtu akae kwake.
 
Mtasema sana ,ila talatibuni ,Maalim kwa taarifa yenu anagombea tena ,yaani kibara tunasema mpaka kijulikane ,sasa mwanasiasa anaejua siasa ni yule anaezungumza kwa hasira ,na huyo ndie anaepata wasikilizaji kwani huwakoleza vibaya sana,kama utachunguza siku hizi wengi wa wanaopanda kwenye jukwaa la kisiasa wote karibuni wameanza kufuata nyayo za Maalim Seif ,kwani ni ngangari ndio inayosikilizwa na Zanzibar wameweza na sasa wametia mguu mmoja ndani ya Ikulu.

Na kuhusiana visa mnavyoviita vya siri ,mkianzia kwa Mfalme mpaka hapa tulipo ,inawezekana huko kuna visa vikubwa sana hivi mliangalia ITV jana ,jamaa kabaka mtoto wa miaka saba huko bara ,habari zimepelekwa polisi eti polisi wametoa dhamana na jamaa anavuruga mitaani na visa hivyo ni vingi huko kwenu ,kwani ukiwa na hela utafanya visa kibao tena vya
hali ya juu.

Kuhusu Jumbe huna unalolijua ,kafukuzwa na Nyerere au Seif ? Hivi wakati wa Nyerere Seifu angeweza kumfukuza au kumsaliti mtu na akafukuzwa au kuondolewa wadhifa wake ?

Kuhusu Muungano aloo kusema kweli hakuna anaeutaka mwanzo ilikuwa huko Zanzibar tu lakini leo hii hata huko Bara kelele ni hizo hizo ,Muungano hawautaki ,kwani ni njia ambayo WaCCMwanaitumia kukaa madarakani ,subirini tu mtasikia hili bunge la Katiba linavunjika kabla ya kufikia mwisho kwani hakuna anaetaka serikali mbili isipokuwa wahafidhina wachache wa CCM,huenda wakaachiwa hilo bunge wafabricate na kufanya wanavyotaka wao.

Hata mwl JK Nyerere aliwahi kusema kuwaambia wa TGK katika moja ya hotba zake akanena Wazanaki wanasema “ UBUBISUBISU OBUWERE EKIRO KIRIMBURA” akiwa na maana ya MFICHAFICHA MARADHI KILIO KITAMFICHUA.

Sasa Tatizo lao ni lile lile wanaogopa vivuli vyao lakin siku zote Hakhi inasimama na Batwil Inapotea. Hakuna marefu yasiyo na ncha.

Tuombe Kheir Znz huru iyoooooooo.



 
Back
Top Bottom