Zanzibar ina hadithi nyingi na siri nyingi!, za mapokeo, nikimaanisha ni maneno na vijineno vya mitaani ambavyo hayana uthibitisho Wala having uthibitisho ila ni hadithi tuu za mapokeo
Moja ya mapokeo haya, eti kwenye ile milingoti ya Bait Al Ajab, kila mlingoti ndani ni hollow, katikati aliwekwa mtu hai mtumwa akiwa amesinama!.
Kuna kisa cha Sultan fulani na mjakazi wa mkewe. Zamani toka enzi za Utumwa, Watumwa wanaume walihasiwa, ili wasizaliane, na watumwa wa kike wengi walifanya kazi ya ujaakazi, Miongoni mwa majukumu ya mjakazi, ni kumsaidia mama kazi zake zote!. Mila za Kiarabu ni za ya wake wengi. Miongoni mwa kanuni za uendeshaji wa ndoa za wake wengi, ni kuwatendea haki bin haki hao wake wote sawa sawa, ikiwemo kupangwa kwa zamu sawa za kulala kwenye nyumba za wake hao, kama ni kulala siku 3, then ni siku tatu kila nyumba.
Sasa inapofika zamu ya mume kulala nyumbani fulani, ikitokea mke hawezi, ili mume asikose haki yake, ilimbidi mke huyo kumtoa mjakazi wake, amuhudumie mumewe kwa zamu hiyo. ( Hili lilifanyika hata kwa Nabii Ibrahim, mkewe Sarah umri ulivuka bila kujaaliwa kupata mtoto, hivyo akamtoa mjakazi wake, mtumwa wa Kimisri, Hagir, ndipo akazaliwa Ismail).
Ikitoke huyu mjakazi akashika mimba, kuna mawili, mke akiridhia, yule mjakazi nae anaolewa akiitwa suria, na mtoto akizaliwa anakuwa ni mwana Sultani!. Mke asiporidhia, mjakazi yule anauwawa.
Kukatokea kisa cha Sultani fulani, alipoletewa mjaakazi, Sultani akapendezewa zaidi na mjaakazi akanogewa akafika jumla!. Ikawa ikifika zamu ya mke yule, Sultani anapewa chakula chake rasmi na mkewe, lakini anadai hajashiba, hivyo kulazimisha kushibishwa na chakula cha mjakazi!.
Hii hali ikasababisha husda kubwa na ugomvi mkubwa kati ya mke na mjakazi!. Kikawaida mke akitofautiana na mjakazi, mke huomba mjakazi yule auwawe, mke alipoomba mjaakazi auwawe, Sultani aligoma, hivyo ili kuepusha shari, mjakazi yule akahamishwa na kuwekwa eneo la masuria wa Sultani wasio na ndoa (concubines), masuria hawa huwa hawapati zamu za Sultani, bali Sultan huja kwao kujipumzikia wakati wowote wa asubuhi, mchana au jioni Sultani anapojisikia kujipumzisha kupooza tuu njaa na kiu haswa wakati wa mchana, akisubiria mlo wa usiku.
Huku na kule, huku na kule, mara yule mkakazi akanasa!, hapa sasa Sultani akawa hawa jinsi, siri lazima itafichuka, na mjakazi itambidi auwawe Kwa vile Sultani alimpenda kwa dhati yule mjakazi yule, aliamua kuificha siri na kuyanusuru maisha ya mjakazi yule kwa kufanya mipango wa siri, huyo mjakazi kupelekwa mahali pasipo julikana kabla siri haijafumka, na huko kuendelea na maisha yake kama mtumwa huru.
Mjaakazi yule alijuja kuposwa akaolewa na kuendelea na maisha mapya!. Familia hiyo ni top secret ila tafuta uhusiano kati ya Sultanet ya Oman, Sultanet ya Brunei na Sultanet ya Zanzibar!, Utapata majibu!.
Kwa taarifa tuu, kwa msiojua, CUF ilishinda 1995, ikashinda tena 2000!, pia ikashinda 2005!, na kushinda tena 2010 lakini kote huko, wanashinda lakini hawapewi ushindi, kwa sababu!. Ila pia amini usiamini uchaguzi wa 2015, CUF itashinda tena Zanzibar, lakini bado haitapewa ushindi, kwa sababu fulani very genuine!, kwa vile hizo sababu zinazopelekea CUF ishinde siku zote na isipewe ushindi, zingalipo zipo, CUF wasipojishughulisha kuzijua, ni sababu gani, wataendelea kushiiki uchaguzi wa rais kwa kufanya kazi bure, ni kama kukimbiza tuu upepo au kutwanga maji kwenye kinu, lakini mwisho wa siku, hawapati Kitu .Ningekuwa mimi CUF, kwanza ningedeal na kuzijua hizo sababu za kwa nini huwa nashinda lakini kwa nini hawanipi ushindi wangu halali?!, nikijiridhisha kuwa this time sababu za kutopewa sasa hazipo tena, ndipo niingie kwenye uchaguzi wa urais, vinginevyo uchaguzi urais wa Zanzibar ni just a wastage of time, money and resources!.
Visa vya Zanzibar heveshi, kuna kisa kingine tena cha ndugu wawili wa tumbo moja, watoto wa kiume wa baba mmoja, mama mmoja, tumbo moja!. Baba yao alifanya makubwa, Chama fulani cha siasa kikaamua kumzawadia nafasi ya urais kaka miubwa kati ya hawa wanadugu wawili. Sababu ya kumzawadia uais mtoto huyo, ni ili kuuenzi mchango wa baba yao, aliyekuwa rais na kuifia nchi yake kishujaa. Japo baba yao alitokea nchini nyingine, licha ya kutokuwa mzaliwa wala mwenye asili yoyote ya Zanzibar, lakini aliifanyia makubwa Zanzibar, hadi kujitoa uhai wake kuifia Zanzibar. Hivyo ile zawadi ya urais kwa mwanaye ulikuwa ni wa zawadi ya heshima ushujaa wa baba yao!. Ni kweli kaka mtu akaupata urais kwa mtindo ule ule wa bao la mkono, baada ya mshindi halisi kutotangazwa. Kaka mtu huyo akahudumu urais wa kipindi chote cha miaka 10!. Baada ya kaka mtu kumaliza kipindi chake cha urais cha miaka 10!, kitu cha ajabu sana, eti mdogo mtu naye akaibuka, akachukua fomu kutaka kumrithi kaka mtu akijua kuwa eti urais wa Zanzibar nao uendeshwe kama usultani!. Chama kikamshauri, kwa vile aliyemaliza muda wa urais ni kaka yake wa tumbo moja, baba mmoja, mama mmoja!, hivyo kumpitisha mdogo mtu, kumrithi kaka mtu, itaonekana kuwa chama chao kinaufanya urais kama usultani!, mdogo mtu, akaelezwa kakaye kapewa tuu urais kwa hishma ya baba yao, lakini bado akagoma na kusisitiza kugombea kwa hoja kuwa eti kama urais ni wa zawadi kwa mtoto wa yule Mzee Shujaa, waliomuheshimu na kumuenzi, then "mtoto halisi aliyestahili urais ule ni yeye!", Kiukweli Zanzibar haieshi vituko!,
Nataka niwashauri wajumbe wa Bunge la Katiba kuhakikisha Mwenyekiti wa kudumu anakuwa Mzanzibari, ili hoja ya serikali tatu ikishindwa, ije hoja ya serikali moja ndio itaimarisha haswa huu muungano wetu adhimu kwa kuwakata kabisa hawa vilimimili na vitimbakwiri vya kutaka kuuvunja huu Muungano wetu adhimu, uliotokana na yale Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar!.
Mapinduzi Daima!.
Muunganno Milele!.
Pasco