Zanzibar ina siri nyingi!, watatafute Wanzanzibar wa enzi zile, wakuhadithie kisa cha Sultan fulani kumpachika ujauzito mjakazi wa mkewe. Zamani toka enzi za Utumwa, wanaume watumwa, walihasiwa, ili wasizaliane, ila watumwa wa kike wengi walifanya kazi ya ujaakazi, kwa wanawake wa Kiarabu. Miongoni mwa majukumu ya mjakazi, ni kumsaidia mama kazi zake zote!. Mila za Kiarabu zinafuata misingi ya Dini ya Kiislamu, ya wake wengi. Miongoni mwa kanuni za uendeshaji wa ndoa za wake wengi, ni kuwatendea haki bin haki wake wote sawa sawa, hivyo kupangwa kwa zamu za kulala kwa wake hao, kama ni kulala siku 3 tatu, then mume analala kwa kila mke siku tatu tatu za zamu yake.
Kila mke anakuwa na wajakazi wake, wanaopangiwa majukumu mbalimbali, wengine kumuogesha, wengine kumpikia, wengine kumtandikia kitanda, wengine kumpepea tuu, enzi hizo kilikuwa hakuna feni, etc. Sasa inapofika zamu ya mume kulala nyumbani kwa mke huyu, ikitokea ni zile "siku" ambazo mke huyo hawezi, ili yule mke asipoteze zamu zake, ilimbidi mke huyo ambaye hawezi, kumtoa mjakazi wake, amuhudumie mumewe kwa siku ambazo zamu yake imefika lakini yeye mke hawezi!. Ikitoke huyu mjakazi akashika mimba, kuna mawili, mke akiridhia, yule mjakazi nae anaolewa akiitwa suria, na mtoto akizaliwa anakuwa ni mwana Sultani!. Mke asiporidhia, mjakazi yule anauwawa kwa kutumbuliwa tumbo kiumbe kinaondolewa, mjakazi anazikwa kama mbwa, kiumbe kinazikwa makaburi za "si rizki" ya ukoo wa kisultani.
Kukatokea kisa cha Sultani fulani, alipoletewa mjaakazi, Sultani akakuta mjakazi anakolea kuliko mke, hivyo Sultani akanogewa akafika jumla!. Ikawa ikifika zamu ya mke yule, Sultani anapewa chakula chake rasmi na mkewe, lakini anadai hajashiba, hivyo kulazimisha kushibishwa na chakula cha mjakazi!. Mara zamu za mke zikaanza kubadilishwa, kwa siku mbili chakula cha mke, na siku moja chakula cha mjakazi, siku za cha mke zikaanza kupunguzwa huku za mjakazi zikiongezeka, ikawa hata zile siku mbazo mkewe anaweza sulatani anataka mjaakazi!. Kadri siku zilivyokwenda, zamu za mke huyu zikifika siku mbili mke, siko moja mjakazi, siku zikawa zinabadilika, mara siku mbili mjakazi siku moja mke, mara ikaja siku zote tatu mjakazi, mke hapati kitu, ili hali yuko fiti! (sijui mjakazi huyu alichukuliwa utumwani kutoka Tanga?!).
Hii hali ikasababisha husda kubwa na ugomvi mkubwa kati ya mke na mjakazi!. Kikawaida mke akitofautiana na mjakazi, mke huomba mjakazi yule auwawe, mke alipoomba mjaakazi auwawe, Sultani aligoma, hivyo ili kuepusha shari, mjakazi yule akahamishwa na kuwekwa eneo la masuria wa Sultani wasio na ndoa (concubines), masuria hawa huwa hawapati zamu za Sultani, hula kwao wakati wowote sultani anapojisikia kwa lengo la kupooza tuu njaa na kiu haswa wakati wa mchana!.
Huku na kule, huku na kule, mara yule mkakazi akanasa!, ujauzito wa sultani, na hapa sasa Sultani akawa hawa jinsi, siri ya ujauzito ikifumuka lazima mkakazi yule auwawewe kwa kutobolewa tumbo!. Kwa vile Sultani alimpenda kwa dhati yule mjakazi yule, aliamua kuificha siri na kuyanusuru maisha ya mjakazi yule kwa kufanya mipango wa siri, huyo mjakazi kupelekwa mahali na kuozeshwa kwa ndoa ya mkeka mahali mbali chap chap kabla siri haijafumka!. Yule mjakazi alikwenda kuolewa chap chap bila muoaji kujua kuwa muolewaji ana mizigo ya watu!.
Baadaye, mwana Sultani alizaliwa huko mjakazi alikoolewa na kulelewa kama mtoto wa kawaida kwenye familia hiyo, ila familia ile ilipata preferential treatments kwa mwana Sultani yule kulelewa vizuri ilmu duniya!. Find out huyo mwana Sultan ni nani?!, tafuta uhusiano kati ya Sultanet ya Oman, Sultanet ya Brunei na Sultanet ya Zanzibar!, find out who funds kiongozi wa chama fulani cha siasa ambaye siku zote huishi hotelini tuu, and why?!. Utapata majibu!.
Kwa taarifa tuu, kwa msiojua, CUF ilishinda 1995, ikashinda tena 2000!, pia ikashinda 2005!, na kushinda tena 2010 lakini kote huko, hawakuipa ushindi, kwa sababu!. Ila pia amini usiamini uchaguzi wa 2015, CUF itashinda tena Zanzibar, lakini bado haitapewa ushindi, kwa sababu fulani genuine!, kwa vile hizo sababu zinazopelekea CUF ishinde siku zote na isipewe ushindi, zingalipo zipo, CUF wasipojishughulisha kuzijua, wataendelea kushiiki uchaguzi wa rais kwa kukimbiza upepo!. Ningekuwa mimi CUF, kwanza ningedeal na kuzijua hizo sababu za kwa nini huwa nashinda lakini kwa nini hawanipi ushindi wangu halali?!, nikijiridhisha kuwa this time sababu za kutopewa sasa hazipo tena, ndipo niingie kwenye uchaguzi wa urais, vinginevyo uchaguzi urais wa Zanzibar ni just a wastage of time, money and resources!.
Visa vya Zanzibar havikuishia hapo, kuna kisa kingine tena cha ndugu wawili, watoto wa baba mmoja, mama mmoja, tumbo moja!. Chama fulani kikaamua kumzawadia nafasi ya urais mtoto mmoja kati ya hawa wanadugu wawili, uamuzi ukafikiwa, wa kuzawadiwa urais ule apewe kaka mkubwa. Sababu ya kumzawadia uais mtoto huyo, ni ili kuuenzi mchango wa marehemu baba yao, aliyekuwa rais wa Zanzibar, akitokea nchini Malawi!, licha ya Mmalawi huyu kutokuwa mzaliwa wala mwenye asili yoyote ya Zanzibar, lakini aliifanyia makubwa Zanzibar, hadi kujitoa uhai wake kuifia Zanzibar. Hivyo ule urais ulikuwa ni wa zawadi ya heshima ya marehemu baba yao!. Ni kweli kaka mtu akaupata urais wa Zanzibar kwa mtindo ule ule wa bao la mkono, baada ya mshindi halisi kutotangazwa. Kaka mtu huyo akahudumu urais wa Zanzibar kipindi chote cha miaka 10!. Baada ya kaka mtu kumaliza kipindi chake cha urais cha miaka 10!, mdogo mtu naye akachukua fomu kumrithi kaka mtu akijua kuwa eti urais wa Zanzibar nao uendeshwe kama usultani!. Chama kikamshauri, kwa vile aliyemaliza muda wa urais ni kaka yake wa tumbo moja, baba mmoja, mama mmoja!, hivyo kumpitisha mdogo mtu, itaonekana kuwa ni kweli chama chao kinaufanya urais wa Zanzibar ni sawa na usultani!, mdogo mtu akagoma na kuibuka na madai mazito!, kuwa eti kama urais ni wa zawadi kwa mtoto wa yule Mzee waliomuheshimu na kumuenzi, then "mtoto halisi aliyestahili urais ule ni yeye!", kwa hoja kuwa eti kaka yeke, ni mtoto tuu wa kufikia wa yule Mzee wao, akimaanisha mama alipokuja kuolewa baba yake, alikuja na mizigo ya watu wengine, ila baba alikubali yote kwa moyo mmoja na roho moja na ndio maana hata wakati alipoamua kuwasomesha wanae nchi kwao Malawi, aliwasomesha wote wawili bila ubaguzi wowote!.
Zanzibar haieshi vituko!, nataka niwashauri wajumbe wa bunge la katiba kuhakikisha Mwenyekiti wa kudumu anakuwa Mzanzibari, ili hoja ya serikali tatu ikishindwa, ije hoja ya serikali moja ndio itaimarisha haswa muungano na kuwakata kabisa hawa vilimimili na vitimbakwiri vya kutaka kuuvunja huu Muungano wetu adhimu, uliotokana na yale Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar!.
Mapinduzi Daima!.
Muunganno Milele!.
Pasco